Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Hahaha πŸ˜‚
Ningekua yeye ningejikita kwenye uhaini. Lakini sijui kwanini Lissu kaamua kujitetea mwenyewe. Hiyo case ni nzito na tena ya uonevu. Angekuwa na wakili wake kwa maoni yangu angejitetea vizuri zaidi.
Tundu Lissu ni mwanasiasa anajiamini na anaamini kwenye uwezo wake kuliko mtu mwingine yoyote, namna atakavyojitetea mwenyewe ni tofauti na mtu mwingine atakavyomtetea ndio maana akaamua ajitetee mwenyewe.
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 22
Nilipakiwa na RCO Mkunja, namkumbuka. Alikuwa mkatili sana, na nilikuwa namwambia, β€œUsijali, Afande, yataisha.”

Namkumbuka alikuwa awe shahidi, ila hawajamleta hapa. Nilikuwa nije nimseme mbele yenu hapa.

Nilibebwa usiku usiku, na mimi siyo mzima sana.

Nikaletwa Dar es Salaam, nikapelekwa Shimoni. Na pale Shimoni kuna mbu wakubwa kama nzi wa chooni, wana supply ya damu muda wote, lazima wanenepe.

Nilikaa mule kuanzia alfajiri hadi majira ya saa 6 na saa 7, nikapelekwa kwa Deputy ZCO, George Bagyemu (PW1). Ndiyo aliyeniambia nakabiliwa na shtaka la uhaini na shtaka la pili, kuchapisha habari za uongo.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, mimi siye niliyeandaa mkutano.

Na kuhusu uchapishaji, shahidi pekee wa kuona mwenyewe na shahidi pekee aliyesikia maneno yangu, na kwa mujibu wa sheria yetu ya ushahidi, The Best Witness ni PW17 pekee.

Wengine wote hawakuwepo katika mkutano.

Na PW17 ndiye aliyesema yeye ndiye amechapisha.

Yeye ndiye amepeleka kurasa za Jambo TV za X na Instagram.

Yeye na wenzake walifanya hivyo kwa kamera 3 za Sony HXR-100, kama sikosei.

Kwa hiyo, kwenye uchapishaji, PW17 amekuja kusema yeye ndiye amechapisha.

He did everything, na siyo mimi.

Kuhusu nani aliyemwalika, amesema siyo mimi.

Aliambiwa na Mkurugenzi wake, John Marwa, β€œNendeni mkakave mkutano wa CHADEMA.”

Na John Marwa, kwa maneno yale, anasema aliambiwa na Brenda Rupia.

Haya maneno walikuwa wanayajua polisi na waendesha mashitaka.

Maelezo haya ni ya tarehe 8 Aprili 2025, na walikuwa nayo tangu tarehe hii 8. They knew it.

Nani aliyeandaa mkutano na nani aliyewaalika?

Wananishitaki na kunituhumu kuhusu mkutano ambao wanajua umeandaliwa na Afisa Habari wa chama, na wananishitaki kuhusu kuchapisha wakati wanajua aliyechapisha.

Walichotaka ni mshitakiwa kwa kosa lisilo na dhamana aende magereza. All they want.

Mapolisi wanasemaga, β€œMpe kesi ya kichwa, akakae gerezani.”

Sasa mimi nimepewa kesi ya kichwa, nikakae gerezani, na wamefanikiwa.

Kwa ushahidi huu, mimi siyo muhaini.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, nilizungumza kitu gani?

Wanawaleteeni maneno ya nusu dakika tu, hawasemi masaa 3 niliyazungumza.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, nilizungumza kuhusu masuala ya matatizo ya Tume ya Uchaguzi na Katiba yetu.

Nilizungumza juu ya masuala ya sheria zetu za uchaguzi na matatizo yake katika utekelezaji, uchaguzi baada ya uchaguzi, uchaguzi baada ya uchaguzi.

Na matatizo ya muundo wa Tume. Niliwaambieni hii ni Tume ya Rais, na kwa sababu ni Tume ya Rais, ni Tume ya CCM.

Na mifano nikiwapa kuhusu aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu Agustine Ramadhani, alitaka kugombea Urais 2015.

Watu wakamwambia, kama ilivyokuwa kwa Jaji Mark Bomani, kwamba wewe ulikuwa Jaji Mkuu, je, umekuwa CCM lini?

Na Jaji Mkuu Agustine Ramadhani alikuwa Meja Jenerali wa Jeshi, je, amekuwa lini CCM?

Kwa sababu wote hao ni CCM.

Waheshimiwa Majaji, tupo Dar es Salaam, na Dar es Salaam ni mkoa wenye watu wengi kuliko yote, una majimbo 10 ya uchaguzi.

Zanzibar, ambayo haina hata moja ya tano ya wakazi wa Dar es Salaam, ina majimbo 50.

Why? Kwa sababu Tume haina utaratibu bora wa namna ya kutengeneza majimbo ya uchaguzi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Chawa unayemsema ni Mimi? Wala sipo upande wa serikali hata kidogo. Niliona tu utetezi wake ungejikita kwenye kosa. Lakini wadau wamefafanua vizuri kwamba pale anaeleza mshtakiwa ni nani. Na I agree it make sense.
Kwenye hili jukwaa Kuna upuuzi Fulani upo yaani ukiwa upo kinyume kimtazamo moja kwa moja unaonekana utakuwa kwenye upande mwingine either ni Serikali au Upinzani kitu ambacho ni wrong wengine hawana vyama vya siasa tunahitaji kubishana kwa hoja ni moja kati ya sehemu ya kujifunza na kupata maarifa mapya.
 
Exactly πŸ’―. Pia hakuna haja ya kumshambulia mtu kisa mawazo yake! Utasikia huna akili! Mbulula etc
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 23

Kwa sababu utaratibu bora tuliotengenezewa na wakoloni unaosema mbunge awe na uwakilishi wa wananchi uliondolewa.

Badala yake, wanaangalia milima, mapori na eneo la kijiografia. Matokeo yake unakuwa na utaratibu wa wabunge ambao hauna uwiano, na hilo ni jambo la Kikatiba moja kwa moja.

Nikawaelezea watia nia wangu juu ya utaratibu mzima wa uandikishaji wa wapiga kura.

Watu wengi ukiwauliza kama watu wana haki ya kupiga kura, watasema ndiyo, kwa sababu ipo katika Ibara ya 5 ya Katiba.

Kwa nini hawajaweka katika sheria? Huwezi kwenda Mahakamani ukasema umenyimwa haki ya kupiga kura.

Kuna mmoja alienda Mahakamani kuwa amenyimwa haki ya kupiga kura, Mahakama ikamfukuza.

Kwa sababu nchi yetu haina sheria inayosema hivyo juu ya haki ya kupiga kura.

Kupiga kura ni utaratibu uliowekwa na Tume ya Uchaguzi.

Daftari la wapiga kura ni ujinga mtupu, hakuna haki ya kupiga kura mle.

Wameanzisha Daftari la Wapiga Kura kuiba kura za CCM.

Mfumo wetu wa kupiga kura umeharibiwa na CCM.

Haya ndiyo nilikuwa naongea na watia nia.

Nilizungumza na watia nia juu ya matatizo ya mfumo mzima wa nomination of candidates, juu ya engua-engua ya wagombea.

Wagombea wanaenguliwa na huwezi kuishitaki Tume mpaka mara baada ya uchaguzi.

Na kwa mtu ambaye amefanya kesi nyingi za uchaguzi kama mimi, hakuna namna Tume ikishatangaza mtu, kuishitaki na kushinda.

Waheshimiwa Majaji, katika ripoti moja wapo ya watazamaji wa uchaguzi, TEMCO, wamesema haijawahi kutokea katika nchi hii mgombea hata mmoja wa CCM kuenguliwa.

Kwa sababu gani? Tume ni ya CCM.

Kwa hiyo, hutakaa usikie mgombea wa CCM ameenguliwa. It has never happened.

Nikizungumza juu ya matatizo ya mfumo mzima wa kampeni za uchaguzi.

Waheshimiwa Majaji, kwa sisi ambao tumeshiriki katika uchaguzi, tunapoenda katika kampeni ukiwa mgombea wa upinzani, ushindani tu siyo na CCM, bali unashindana na polisi, watendaji wa vijiji na kata, maafisa tarafa, ma-DC na ma-DSO na wakurugenzi, pamoja na mfumo mzima wa kiserikali.

Watakuvurugia mikutano yako, watafanya kila aina ya uchafu na kuhakikisha kila namna kampeni haifanyiki sawasawa.

System nzima ipo stacked, na mfumo wa uchaguzi ukishinda, hujashinda CCM peke yake; mara nyingine umewashinda mahakimu.

Kwa sababu mahakimu wanatakiwa waapishe wagombea, na mahakimu wanajificha wasiapishe wagombea wa upinzani.

Aliyekuwa mgombea wetu wa Jimbo la Mrimba, anaitwa Suzan Kiwanga wa Mrimba, anarudisha fomu, akakuta Mkurugenzi kafunga ofisi, hayupo.

Ilipofika saa 11, Mkurugenzi kajitokeza, kasema, β€œUmechelewa, Mama,” na mgombea wa CCM kapita bila kupingwa.

Kwa hiyo, mfumo mzima wa uchaguzi umekaa kuipendelea CCM.

Mimi nimegombea urais, nimepigwa mabomu na polisi Kilwa Kivinje, Tarime, Mugumu Serengeti.

Nimesimamishwa kampeni na Tume siku 10.

Kuna wakati Magufuli alikuwa anakata pumzi, wanabidi waanze kumpepea-pepea. Hivi mimi nimesimamishwa kampeni kwanza.

MAHAKAMA KICHEKO πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 

Nabii Lissu katika ubora wake!
Huyu hata wakimuua atakuwa ameshatimiza wajibu wake kwa Tanganyika!
 
Aliyekuwa mgombea wetu wa Jimbo la Mrimba, anaitwa Suzan Kiwanga wa Mrimba, anarudisha fomu, akakuta Mkurugenzi kafunga ofisi, hayupo.

Ilipofika saa 11, Mkurugenzi kajitokeza, kasema, β€œUmechelewa, Mama,” na mgombea wa CCM kapita bila kupingwa.
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 24

Waheshimiwa Majaji, nikizungumza na watia nia katika uchaguzi, kuna kitu kinaitwa maadili ya uchaguzi.

Kama vile ni kweli wanapenda maadili, wanatumia maneno matamu matamu kama kweli wanapenda maadili.

Wanaopigwa faini, wanazuiwa kampeni ni wapinzani.

Na ni wapinzani wa ukweli, maana kuna wapinzani wengine ni majina majina tu.

Ukiwa CHADEMA, β€œanhaaa, utakiona.”

Nikazungumza na watia nia kuwa hayo maadili, kwa sababu ya kutuchapia wakati wa kampeni, na hatukusaini.

Matokeo yake Tume hii ikatangaza kwamba kwa sababu hatujasaini maadili, eti CHADEMA imefungiwa miaka 5 kugombea. Kwa sheria gani?

Nikazungumza na watia nia kuhusu vyombo vya dola wakati wa uchaguzi, wote wanakuwa CCM.

Wakati wa uchaguzi ule, TEMCO ilishapigwa marufuku na Magufuli, waangalizi wa ndani walikuwa REDET.

REDET imekaa ki-CCM, lakini waliandika ukweli kuhusu vyombo vya habari kupendelea CHADEMA.

BBC walilipishwa milioni 10 na TCRA kwa kosa la kufanya mahojiano na mimi wakati wa kampeni.

Hawa Jambo TV ambao wanasema nimechapisha habari yao wamefungiwa mara nyingi sana kwa kufanya mahojiano.

Tunιœ€θ¦ sheria ya vyombo vya habari inayosema FAIR ELECTORAL COVERAGE.

Sheria inayosema pawe na usawa katika coverage ya vyombo vya habari.

Nilizungumza na watia nia namna ya kurekebisha utaratibu wa coverage ya kampeni, pawe na fairness ya kusikika.

Nikizungumza na watia nia masuala yanayohusu siku ya uchaguzi.

Hilo somo nimezungumza everywhere.

Kuhusu swala la Jumapili ya uchaguzi na matatizo yake. Wakati ule uchaguzi tulikuwa tunafanya siku ya Jumapili.

Ukiwa mshamba mshamba, unashinda na wanamtangaza mtu wa CCM.

Ukifanya vurugu, unakutana na FFU na baadaye utakutana na hawa Mawakili wa Serikali.

Mimi nilimaliza uchaguzi kwangu, nikatangazwa baada ya siku 4.

Wakati huo palikuwa na polisi anaitwa Wankyo.

Baada ya kumwambia Mkurugenzi, β€œNaondoa polisi,” ndipo Mkurugenzi akanitangaza mshindi.

Hayo ndiyo matatizo ya wagombea ubunge na udiwani nchini Tanzania.

Na nilizungumza nao matatizo baada ya uchaguzi.

Kwa sababu mimi ni mtaalamu wa migogoro baada ya uchaguzi.

Nikawaambia, Mahakamani hapawezekani.

Wataharibu uchaguzi nchi nzima, ila hutakaa kuona majimbo 5 uchaguzi umerudiwa.

The law is impossible. Utaratibu wa Mahakama ni mgumu sana.

Kuna ripoti ya Judiciary ambayo inasema utaratibu ni mgumu sana katika Mahakama zetu kutengua matokeo ya uchaguzi.

Niliwapitisha kote huko kuwa tunahitaji mabadiliko katika Election Petition.

Election Petition ni kesi za madai, lakini proof ni beyond reasonable doubt.

Nchi za kidemokrasia zilishaondoa hiyo beyond reasonable doubt kwa sababu uchaguzi unavurugwa kitaifa kwa majimbo 265.

Mahakama zipo wapi za kusikiliza kesi 265 za uchaguzi na Majaji wapo wapi?

Kwa majimbo yote hayo 265?

Nilawaambia hii ndiyo reform tunayodai na kuhamasisha Watanzania wadai kwa ku-boycott if needs be.

Na nilisema kingine very controversial kwamba sisi tunadai mabadiliko, kwa miezi hii michache hatuwezi kupata vyote hivi.

Nilisema kwamba tupo tayari kusubiri kwa kuahirisha uchaguzi usifanyike mwaka huu, tufanye mwakani ili tupate mabadiliko ya maana.

Ndani ya chama wakaniuliza, β€œTuwaache waendelee kuwa madarakani?”

Nikawajibu, β€œNdiyo, kama tunataka kupata mabadiliko ya maana.”

Badala yake wakanijibu kina Wasira, β€œHaiwezekani, uchaguzi upo Kikatiba.”
(Huku Lissu akimuigizia sauti yake Wasira.)

MAHAKAMA KICHEKO.

Tungeweza kuepusha vifo vya watu wetu wengi sana. Jaji Chande anasema watu 500, lakini nani ajuaye kwamba kuna maelfu wengine wamekufa?

Tungeweza kuahirisha uchaguzi na watu wetu wasingekufa.

Wanasema ulisema tutakinukisha, ulisema utahamasisha uasi.

Inabidi usikie maneno yote haya, siyo maneno ya kunyofolewa.

β€œOooh, unatishia Serikali.” Hakuna katika maneno neno β€œSerikali” na hawajaleta pia katika hati yao ya mashitaka.

Wanasema lengo lilikuwa ni kutishia Serikali. Neno wamelitoa wapi na walizungumza na nani akawaambia ni Serikali?

Hiyo inayoitwa nia ya kutishia Serikali haikuwa ya kutishia Serikali, bali ilikuwa ni kuwaelezea watia nia wa chama changu matatizo ya uchaguzi ili waweze kuelewa na kuunga mkono msimamo wa chama wa No Reforms, No Election.

Sikuzungumza kuhusu Serikali, bali kuvuruga uchaguzi.

Na mimi ni mwanasheria, nimezungumza kuvuruga uchaguzi kwa sababu hakuna kosa la kuvuruga uchaguzi.

Nimezungumza kukinukisha kwa sababu siyo kosa kisheria.

Wangetaka, wangeniuliza ulikuwa na maana gani. Mimi ni mtaalamu wa masuala ya uchaguzi.

Dhumuni lilikuwa ni kuwaelewesha Watanzania nchi nzima.

Na tulipeleka kila sehemu, hadi Kenya kwa Raila, Shura ya Maimamu, kwa Jaji Warioba.

Haikuwa siri.

Waheshimiwa Majaji, mimi siongozi chama cha conspirators, naongoza chama cha wapigania haki.

Waheshimiwa Majaji, sidhani kama nina muda.

Tutakapokutana kesho kutwa, nataka kuwapitisha kwenye ushahidi ulioletwa.

Nataka niwaonyeshe kama huo ushahidi ukiletwa, kama unatosha kunyonga mtu.

Waheshimiwa Majaji, naomba niishie hapa. Napendekeza tuahirishe hadi Jumatano.

Nashukuru, Waheshimiwa Majaji, kwa kunisikiliza.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA MWISHO


Jaji Ndunguru: Hatujasikiliza upande wa Serikali kama wanataka tuendelee.

Lissu: Ni sawa, ila mimi kwa leo nimekata pumzi. Tuahirishe hadi kesho kutwa.

Wakili wa Serikali: Kwa sababu anasema mwenyewe amekata pumzi, basi tuahirishe tu.

Majaji wanateta.

Jaji Ndunguru: Kesho tumia kuongea na shahidi wako wa kwanza ili kesho kutwa umalize.

Tuendelee na DW2.

Jaji Ndunguru: Natumaini utamaliza ndani ya saa 1 ushahidi wako.

Lissu: Siwezi kuahidi saa 1.

Jaji Ndunguru: Masaa 2 je?

Lissu: Labda masaa 3.

Jaji Ndunguru: Basi naahirisha kesi hadi kesho kutwa.

Afande: HIGH COURT!

Magereza wanamfuata Lissu kizimbani.

Majaji wanatoka.

Asanteni Tukutane jumatano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…