Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 12

Nitawaelezeni juu ya matatizo ya uchaguzi.

Waheshimiwa Majaji, tumekuwa tunafanya uchaguzi katika nchi hii tangu 1957.

Uchaguzi wetu Mkuu wa kwanza ni ule uchaguzi ulioigawa TANU juu ya zile kura 3.

Uchaguzi wa pili, 11 Agosti 1960, wa Bunge lililoleta uhuru tukapata madaraka.

Kuanzia mwaka 1960 mpaka leo tumefanya uchaguzi kila baada ya miaka 5 bila kukosa.

We have conducted elections every five years without failing.

Kabla ya 1995, ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, kati ya 1965 mpaka 1995 tulifanya chaguzi za chama kimoja.

Kuna vijana wengi hawajui nini maana ya uchaguzi wa chama kimoja.

Ukienda kufanya uchaguzi, kwenye picha ya mtu na giza unaambiwa chagua mtu unayemtaka.

Jaji Ndunguru: “Hao ambao hawajui wakasome historia.”

Lissu: “Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, mwaka 1992, baada ya kuingia katika mfumo wa vyama vingi, ulifuata uchaguzi wa 1995 wa vyama vingi.

Hapokuwa tena na kuchagua mgombea na giza.

Wakati tunaingia katika mfumo wa vyama vingi, Rais Mwinyi akiunda Tume ya Nyalali, je, Tume ya Nyalali ilipendekeza nini?

Tume ya Nyalali ilipendekeza tarehe 17 Februari 1992 na kuweka ratiba kwamba itakapofika Septemba 1993:

Moja, tuwe na Katiba mpya na katika Katiba mpya tuwe na Tume huru ya Uchaguzi.

Na Tume ya Nyalali ilipendekeza hivyo kwa sababu ilisema Katiba yetu ni ya chama kimoja na mfumo wake ni wa chama kimoja; haifai kwa vyama vingi.

Mfumo wa uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ni wa chama kimoja, haifai kwa mfumo wa kidemokrasia wa vyama vingi.

Tume ya Nyalali ikapendekeza na ratiba kwamba mpaka tutakapofika 1995...

Ikapendekeza na kitu muhimu tunachokisahau, cha kuwa na wagombea binafsi (Independent Candidates).

Mapendekezo ya Tume ya Uchaguzi, Serikali ya CCM chini ya Rais Mwinyi, wakayakataa.

Wakakataa Tume huru ya Uchaguzi, Katiba mpya na wagombea binafsi.

Waheshimiwa Majaji, Marehemu Mzee Mwinyi aliandika katika kitabu cha kumbukumbu ya maisha yake kwamba walikataa Katiba mpya na wagombea binafsi, watu wangekimbia CCM.

Ikaleta ugomvi kati yao na Nyerere.

Waheshimiwa Majaji, kilichotokea katika hiyo sheria ya mabadiliko ya Katiba iliyoleta vyama vingi vya siasa...

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA


NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Twende mkuu
 
Kati ya wewe na hao majaji waliotulia wanamsikiliza na wanachukusa notes kabisa, mbumbumbu wa sheria ni nani??
hao wanamsikiliza kwa makini huku wanasikitika,

wanatamani walau wapate hata kapointi ka moja kwa jinsi muungwana anavyojipotezea muda mrefu kumbwelambwela vitu useless kama kawaida yake.

in fact siku inaweza kwisha na pasiwepo cha maana ameeleza 🐒
 
Tofauti Kati ya Mwl Nyerere na Tundu Lissu ni ndogo Sana.
Huyu jamaa ni Nyani Mzee
 
Kama hufuatili kaa kimya au uondoke. Kitu hukitaki ila umekazana kufuatilia. Kweli wewe punguwani.
muerevu tuliza mihemko,
mbona mtuhumiwa mwenyewe pamoja na kueleza vitu nonsense hana mihemko?🐒
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 13

Iliyoleta neno Tume ya Uchaguzi, ambayo siku hizi mnaita Tume Huru ya Uchaguzi, siyo sawa. Jina lake kwa mujibu wa Katiba ni Tume ya Uchaguzi.

Mabadiliko haya yameifanya Tume ya Uchaguzi kuwa Tume ya Uchaguzi ya CCM kuliko ilivyokuwa mwanzo.

Ikafanya wajumbe wa Tume kuwa wateule wa Rais.

Kabla ya hapo, Spika ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.

Baada ya hapo, Jaji wa Mahakama Kuu ndiye anakuwa Mwenyekiti wa Tume, ila anateuliwa na Rais.

Mwanzo, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi alikuwa anateuliwa na kamati, baada ya mabadiliko akawa anateuliwa na Rais.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi anateuliwa anayekaa ki-CCM, ki-CCM.

Sheria ya Uchaguzi ya 1985 imefutwa na Sheria ya 2024.

Iliwafanya wasimamizi wa uchaguzi kuwa wakurugenzi wa Halmashauri, ambao wote ni wateule wa Rais.

Juzi Nassoro Katuga alisema watumishi wote wa Serikali wanafanya kazi kwa niaba ya Rais, kwa hiyo wote hawa wanafanya kazi kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM.

MAHAKAMA: KICHEKO.

Nassoro Katuga: “Nimesikia, Waheshimiwa Majaji, shahidi kanitaja, nisije nikatajwa kama shahidi baadaye.”

MAHAKAMA: Kicheko.

Lissu: “Hilo haliingii, kaka.”

Nataka kusema kwamba Tume ikawa Tume ya CCM.

Yote haya yamesemwa na Tume ya Warioba.

Moja ya kazi bora kabisa ya utafiti wa Kikatiba kuhusu uchaguzi.

Hawa wote wanateuliwa na Rais na wengi ni wanachama wa CCM.

Na kwa sababu hao ni CCM, ndiyo maana aliyekuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi wakati wa Magufuli mwaka 2020, leo ni Mbunge wa CCM.

Matokeo ya mfumo huu yakaanza kujitokeza mara moja katika uchaguzi wa 1995.

Waheshimiwa Majaji, Tume ya Uchaguzi kwa muda mrefu ilikuwa na makao makuu Dar es Salaam, pale jirani na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Katika uchaguzi wa mwaka 1995, vifaa vya uchaguzi havikupelekwa kabisa katika vituo vya kupigia kura.

Tume ikavuruga uchaguzi wa Dar es Salaam kwa kumhofia Augustine Lyatonga Mrema.

Mauaji yakatokea Zanzibar kwa Tume kuvuruga uchaguzi mwaka 1995.

Nimewaambia, mwaka 1995 nilikuwa mgombea ubunge.

Kelele za mabadiliko zilikuwa kubwa sana mwaka 1995, na nimewaambia nimefanya utafiti kuhusu uchaguzi kwa miaka 4.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Huyu Jamaa kazi nzuri aloyofanya iliyotukuka ndio inayompa Neema na Amani ya kuendelea kuishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…