Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

pop paap alf inapotea? ndo nini sasa jamani
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Mahakama imerejea.

Lissu anaingia, na nyuma wanafuatia Majaji.

Karani wa Mahakama anashika maikrofoni kutangaza kesi.

Mawakili wa Serikali wanapelekewa maiki.

Wakili wa Serikali, Ajuaye Zegeli, anasimama: “Waheshimiwa Majaji, kolamu inabaki vilevile. Tupo tayari kuendelea na maswali ya dodoso kwa shahidi wa utetezi.”

Jaji Ndunguru: “Mshtakiwa, upo tayari?”

Lissu: “Nipo tayari, Waheshimiwa Majaji.”

Jaji Ndunguru: “Nakukumbusha, upo chini ya kiapo. Tuendelee.”

Anasimama Nassoro Katuga: “Waheshimiwa Majaji, naomba kielelezo namba D15, ushahidi wa PW16.”

ACP Amini Mahamba.

Nassoro Katuga: “Sasa shahidi, iambie Mahakama kama ni ushahidi wako mbele ya Mahakama hii tukufu kwamba wapelelezi hawakukupa nafasi wala kukuuliza maana ya maneno yaliyoandikwa katika hati ya mashitaka.”

Lissu: “Ndiyo, huo ni ushahidi wangu.”

Nassoro Katuga: “Iambie Mahakama, wakati PW1 anatoa ushahidi akieleza kwamba ulipoletwa kwake alikupa nafasi ujieleze kwa nini asikushitaki kwa uhaini...”

Lissu: “Rudia swali.”

Nassoro Katuga: “Katika ushahidi wako ulisema hawa Polisi hawakukahoji wala kukuuliza maana ya maneno yako?”

Lissu: “Hawakunihoji.”

Nassoro Katuga: “PW1 hakukuhoji kwamba ulikuwa unamaanisha nini?”

Lissu: “Hakunihoji.”

Nassoro Katuga: “Alipokwambia anataka kukushitaki kwa uhaini, ulijibu nini?”

Lissu: “Kwa sababu walikuwa wameshanikamata na wamenishitaki kwa uhaini, nikawaambia tutakutana Mahakamani.”

Nassoro Katuga: “Kuna wakati gani mtu anaitwa mshtakiwa na mtuhumiwa?”

Lissu: “Nilikuwa nimeshakamatwa na kushitakiwa.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…