Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani leo Agosti 28, 2026

TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kama mkutano nje ya Sekretarieti na watia nia walialikwa, ni kina nani wengine?

Mnyika: Tulialika viongozi wakuu wa Chama na waandishi wa habari.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ukisema ulialika viongozi wakuu wa Chama, unamaanisha kina nani?

Mnyika: Namaanisha Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Antipas Lissu, Makamu Mwenyekiti Bara, John Wegesa Heche, Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Mzee Saidi, na viongozi wakuu wengine ambao ni sehemu ya Sekretarieti, ambao ni Katibu Mkuu na manaibu wake.

Lissu: Waeleze Majaji, huo mkutano unaouita wa ndani ulifanyikia wapi?

Mnyika: Ulifanyikia Makao Makuu ya CHADEMA, Mikocheni, Mtaa wa Daima, Nyumba Namba 31.

Lissu: Waandishi wa habari wa vyombo vipi ambao mliwaalika, kwa kumbukumbu zako?

Mnyika: Tuliwaalika wote kwa ujumla, na walialikwa na Brenda Jonas Rupia.

Nilielekeza vilevile itolewe taarifa ya habari kwa umma ya wazi.

Ambayo ilitolewa tarehe 27 mwezi Machi, ambayo ilitolewa na Brenda Rupia.

Ambayo ilialika waandishi wa habari, lakini pia iliutaarifu umma kuhusu kikao hicho.

Lissu: Wakati wewe na Sekretarieti yako mnafanya yote haya, Mwenyekiti wako alikuwa wapi?

Mnyika: Alikuwa katika ziara Kanda ya Nyasa, akiendelea na Operesheni ya Katiba Mpya.

Lissu: Kanda ya Nyasa ni wapi?

Mnyika: Inajumuisha Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe na Rukwa.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo ziara ya Mwenyekiti ilitumia muda gani?

Mnyika: Nakumbuka ilianza tarehe 23 mwezi Machi hadi kabla ya tarehe 03 Aprili.

Lissu: Waeleze Majaji kama Mwenyekiti wa Chama alishiriki maandalizi yoyote?

Anasimama Job Mrema: Waheshimiwa Majaji, tunaona shahidi anavyoongozwa kwa taratibu za in-chief zinakiukwa.

Tunaomba Bwana Tundu Antipas Lissu akumbushwe namna ya kuongoza mashahidi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
hapa kuna kesi ya uchechezi sio uhaini
Hata kesi za uchochezi pia ni kesi za kijinga zinazotumika kama tool za kuwakandamiza wapinzani, nchi za kijinga jinga ndio zimebaki na kesi za uchochezi. Sheria ya kesi ya uchochezi zilikuwa adapted kutoka tawala za kikoloni.

Nchi zenye akili zilishafutilia mbali ujinga unaoitwa uchochezi, Sababu una contradict na demokrasia + uhuru wa kutoa maoni, Kwa Africa Ghana ni mfano wa nchi zilizofuta makosa ya uchochezi 2001.

Na sisi tutafika huko lazima, lakini until then wacha watawala waitumie…
 
We kichwa nazi uhaini unatangazwa kwenye mikutano ya hadhara?
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

Lissu: Waheshimiwa Majaji, shahidi akikuwa anasema anachokumbuka, wala siku mwambia ajikumbushe.

Kama Wakili wa Serikali naona ni shida, naondoa tu, tuokoe muda.

Jaji Ndunguru: Ni sahihi mshtakiwa kuondoa kwa sababu shahidi ameshadoma unachomuuliza.

Lissu: Sasa shahidi, baada ya ushahidi ambao umeutoa mpaka hapa ulipofikia, je, hii tuhuma kwamba mimi ndiyo niliyeandaa mkutano na kualika waandishi wa habari, wewe unaionaje?

Mnyika: Waheshimiwa Majaji, hii ni tuhuma ya uongo na ni tuhuma ya kubambikiza tu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kama mlipokuwa mnawaalika waandishi wa habari, palikuwa na maelekezo waje na nini na kitu gani?

Mnyika: Hapakuwa na maelekezo yoyote kwamba waje na nini au na kitu gani.

Lissu: Umetolewa ushahidi katika Mahakama hii kuwa waandishi wa habari waliokuja katika mkutano wa JAMBO TV. Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kulikuwa na maelekezo kwamba waje na kamera.

Ajuaye: Waheshimiwa Majaji, tunachokiona ni mshtakiwa anamlisha ushahidi shahidi wake.

Lissu: Naomba ueleze kama mliwaelekeza waandishi wa habari kuja na kamera.

Jaji Ndunguru: Rudia tena swali, ukishatumia neno "kama" ni kwamba unapendekeza jibu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, mliwaelekeza waandishi wa habari waje na vifaa gani?

MAHAKAMA: Kicheko.

Jaji Ndunguru: Nafikiri bado hapo kuna maelekezo, neno "vifaa".

Lissu: Wacha niachane na hilo swali, maana linanipotezea muda.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama palikuwa na maelekezo kwa waandishi wa habari juu ya namna ya kutumia vifaa vyao.

Lissu: Sasa wafafanulie Waheshimiwa Majaji utaratibu uliotumika wa waandishi wa habari kurusha huo mkutano.

WEJA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
..
 
Skript zilikuwa poa. Labda dairekta alikosea tu kupanga matukio..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…