Kesi ya Uhaini ya Lissu: Heche kuendelea kutoa ushahidi Mahakamani Sept. 11. 2026

TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 14.

Lissu: Sasa Shahidi, umeeleza jitihada za chama na mazungumzo na CCM, ukaeleza matatizo yaliyojitokeza mwaka 2024, ukaeleza ya “No Reforms, No Election”, ukaeleza ya mkutano wa tarehe 03 April.

Sasa nataka ueleze ya tarehe 29 October.

Sasa waeleze Waheshimiwa Majaji, wewe ulikuwa wapi na waeleze kama ulishiriki kupiga kura.

Heche: Waheshimiwa Majaji, mimi sikupiga kura katika uchaguzi wa tarehe 29 October 2025. Nilikuwa katika kituo cha Polisi Mtumba, Dodoma, baada ya kukamatwa hapa tarehe 22 October 2025.

Nassoro Katuga: Huu ushahidi kwamba nilikamatwa, Mahakama Kuu hapa nikapelekwa Mtumba, Dodoma, nikaletwa Oysterbay nikawakuta...

Ni ushahidi unaorudiwa.

Jaji Ndunguru: Tukiacha, tuone labda kuna sehemu anaelekea.

Lissu: Wala Waheshimiwa Majaji, sina nia ya kurudia ushahidi bali najengea msingi.

Lissu: Shahidi, sasa tueleze unafahamu nini kuhusu siku ya tarehe 29 October.

Heche: Waheshimiwa Majaji, nafahamu kwamba nilipotoka Polisi nilipata taarifa nyingi zinazohusiana na kile kilichotokea tarehe 29 October—watu kuuawa kwa wingi.

Kwa mujibu wa hotuba ya Jaji Chande, ni watu 518.

Waheshimiwa Majaji, kwa rekodi tu, Jaji Chande anasema haijulikani kabisa, lakini inaweza kuongezeka.

Mzee Joseph Sinde Warioba alisema ni wengi kuliko walio uawa katika Vita ya Kagera.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, tunaangalia hilo jibu la mwisho la Shahidi. Anasema kwamba Mzee Warioba alisema...

Tukio hilo liko hivyo, itakuwa tumepokea hearsay.

Huyu ni Shahidi wa fact kwa mujibu wa kifungu cha 167.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, kuna mambo mengi sana hapa yanaongelewa kama vile ni sheria, lakini si hivyo.

Ushahidi wa hearsay ni ushahidi unaohitaji corroboration—ushahidi ambao unahitaji kuthibitishwa tu na ushahidi mwingine.

Na tatu, ana nafasi kubwa ya kuja kufanya cross-examination.

Na mwisho, Mahakama ndiyo itaamua ni ushahidi gani una mashiko.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Lissu: Asante, Waheshimiwa.

Heche: Waheshimiwa, nilikuwa naeleza kwamba hiyo ni idadi kubwa ya watu kuuawa kwa pamoja tangu Vita vya Maji Maji, mwaka 1905 hadi 1907, na vyombo vya dola.

Lissu: Shahidi, naomba ufafanue hilo ulilosema kwamba haya ni mauaji makubwa kufanywa na Serikali toka kipindi cha Maji Maji.

Heche: Nimesema hivyo, Waheshimiwa Majaji, kwa sababu nafahamu historia ya nchi yetu.

Kwa sababu Dar es Salaam watu 130, Mwanza watu 90, na Mbeya na kwingineko.

Hakuna Serikali iliyowahi kuua watu wengi...

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 15.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa mhusika yeyote kuwajibika vyovyote.

Heche: Waheshimiwa Majaji, sijawahi kusikia mtu yeyote akiwajibika kwa namna yoyote kwa mauaji makubwa ya namna hii siku ya uchaguzi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ufahamu wako iwapo kuna Kiongozi wa Serikali aliyewahi kuwajibika kwa mauaji hayo.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna Kiongozi yeyote wa Serikali aliyewajibika kwa namna yoyote.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo hotuba ya Jaji Chande imetoa jina la Kiongozi yeyote aliyetoa amri ya kutekeleza mauaji hayo.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna sehemu yoyote katika hotuba ya Jaji Chande iliyomtaja Kiongozi aliyetoa amri ya kutekeleza mauaji hayo.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, uwepo wa kesi ya mauaji dhidi ya mtu yeyote aliyehusika na mauaji makubwa hivi.

Heche: Waheshimiwa Majaji, sina ufahamu wa kesi yoyote ya mtu aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji makubwa hivi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, walio uawa ni binadamu au wanyama pori waharibifu wa mazao?

Jaji Ndunguru: Rudia swali. Limekuwa multiple choice.

Lissu: Naomba kurudia swali.

Waeleze Waheshimiwa Majaji, Shahidi, kuhusu uhalali wa Serikali kuua watu wake.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna uhalali wa Serikali kuua watu wake, tena kwa idadi kubwa kiasi kile.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, hoja yetu ya kuahirisha uchaguzi ili tupate sheria nzuri za kusimamia uchaguzi ingekubaliwa, ingekuwaje?

Heche: Waheshimiwa Majaji, hoja zetu zingekubaliwa, pasingetokea maafa makubwa kiasi hicho.

Jaji Ndunguru: Hiyo ni fact au assumption?

Lissu: Shahidi amesema kwa ufahamu wake.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, nini kilikuwa kisababishi cha kwanza alichotaja Jaji Chande cha maafa hayo?

Heche: Alisema ni madai ya muda mrefu ya Watanzania kutaka:

  • Katiba mpya;
  • Tume huru ya uchaguzi;
  • Kupambana na rushwa na ufisadi;
  • Ukosefu wa ajira;
  • Watu kutekwa nyara na kupotezwa;
  • Kutokushughulikiwa kwa masuala hayo.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Hiyo lissu alikua gerezani hao chadema walifungiwa kufanya siasa sasa mambo si yaliishia apo hata siasa hawakufanya Tena mpaka vurugu zikaja kutokea siku ya uchaguzi huoni kama viongozi ndio wamewapa hasira wananchi wao wenyewe

..Lissu alikuwa gerezani.

..Mama alikuwa huku nje na kibunda chake cha BILLION 200 kwa ajili ya kampeni.

..halafu Mama pamoja na mapesa yote hayo analalamika eti watu walihongwa kufanya vurugu Oct 29.

..sijui mnanielewaa?!
 
Alisema wapi? Acha uongo
Kama hujui kauli hii ameongea Raisi basi inaonesha ujui unachoshabikia na sio tu Raisi pekee mpaka Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba na yeye ndio alikuwa wa Kwanza kuongea kwenye press yake ya Kwanza na waandishi habari
 
Kama hujui kauli hii ameongea Raisi basi inaonesha ujui unachoshabikia na sio tu Raisi pekee mpaka Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba na yeye ndio alikuwa wa Kwanza kuongea kwenye press yake ya Kwanza na waandishi habari
Nimekuuliza swali fupi sana. Haya maneno unahororoja ya nini? Weka ushahidi wa tuhuma yako hii
 
Ile video ya mahojiano pale Wasafi kati ya Heche na Wasafi, Heche alikuwa mtulivu sana, Manara alijaribu kumkomoa jamaa ila jamaa akamtuliza na ikaonekana Manara kama fala tu.
 
 
Mbona apo wanajidhalilisha tuh Hawa viongozi Huyo Heche Kila anachoongea waziwazi kinaonekana ni kweli na ni facts tupu ni Aibu kubwa kwa viongozi watu wamekufa jamani sio jambo la kawaida alafu bado wanataka kumsingizia Lissu sio poa kabisa aisee
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 16.

Lissu: Jaji Mkuu Othuman Chande alisema nini juu ya utekaji nyara na upotezaji wa watu, kwa kumbukumbu zako?

Heche: Alisema watu wanatekwa, Waheshimiwa Majaji, kwa sababu za kimapenzi, ushirikina na sababu za kibiashara.

Lissu: Umetaja watu wa CHADEMA na CCM, akiwemo Humphrey Polepole na Kanguye wa CCM. Hili Jaji Mkuu Othuman Chande alisemaje juu ya hawa?

Heche: Hakusema lolote.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, uwezekano wa mtu kujiteka mwenyewe.

Nassoro Katuga: Sina sababu ya kuweka objection. Shahidi hatakiwi kutoa opinion na kupewa leading questions. Hili swali la mwisho kashajengewa uwezo, ndiyo anaulizwa.

Ni hayo, Waheshimiwa Majaji.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, swali langu liko very simple: Aeleze uwezekano wa mtu kujiteka.

Nassoro Katuga: Huyu siyo expert. Anachokitoa hapo ni opinion.

Lissu: Hilo naachana nalo, lisitupotezee muda.

Lissu: Shahidi, tueleze aina za utekaji alizoeleza Jaji Chande.

Heche: Hakueleza aina za utekaji. Utekaji ni mmoja tu.

Lissu: Kwenye ushahidi wako ulisema kwamba ulipotoka katika mahabusu ya polisi ulisoma taarifa nyingi za mauaji.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, hii siyo sahihi. Shahidi alisema alisikia, hakusema kwamba alisoma. Anamuuliza swali ili tukipinga, ndiyo shahidi aseme.

Lissu: Naomba nisomewe rekodi za Mahakama.

Jaji Ndunguru: (Anasoma rekodi) “Nilipata taarifa nyingi.”

Lissu: Asante, Wakili, kwa kunikumbusha. Kumbe nilipata, siyo nilisoma.

Haya shahidi, tutajie hizo taarifa ulizopata.

Heche: Nilipata taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari, kwa kusoma na kusikiliza. Nilipata ripoti kutoka kwa waangalizi wa kimataifa.

Lissu: Waangalizi wa nini?

Heche: Waangalizi wa uchaguzi.

Nilipata taarifa mbalimbali za jumuiya.

Nilipata taarifa za jumuiya za kikanda kama Afrika Mashariki.

Na taarifa za mashirika ya kidini.

Heche: Waheshimiwa Majaji, naweza kwenda short call?

Jaji Ndunguru: Sawa, tunakuruhusu.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Inaonekana unafuatalia mambo, safi sana.
 
 

Attachments

  • 6381504-457b5131fdfe1ba30241f5952f4311e0.mp4
    1.5 MB
  • IMG-20260827-WA0012.jpg
    22.3 KB · Views: 13
Asante mkuu naomba uendelee kumwaga nondo za updates.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 17.

Lissu: Watajie taarifa za taasisi za kidini ulizopata.

Heche: Nilipata taarifa za Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).

Lissu: Taarifa gani nyingine ya kidini?

Heche: Shura ya Maimamu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa kumbukumbu zako, tarehe hizi taarifa za Baraza la Maaskofu Katoliki na Shura ya Maimamu zilitolewa lini?

Heche: Ilikuwa ni mwezi Novemba mwaka jana.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ripoti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ilisema nini?

Heche: Ilizungumzia mauaji ya Oktoba 29.

Pia ilipendekeza ufanyike uchunguzi huru ili kuwabaini waliohusika na hatua zichukuliwe dhidi ya waliobainika kuhusika.

Ila ililaani matumizi ya nguvu yaliyopitiliza dhidi ya wananchi au waandamanaji.

Ilizungumzia hali ya kidemokrasia, kuhusu wananchi kunyimwa haki ya kupata viongozi wanaowataka, na ilitoa mfano kwamba hali hiyo imekuwepo tangu mwaka 2016.

Kumekuwa na manung’uniko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi kuhusu madai yao.

Ilizungumzia pia kuhusu hali ya usalama, kwamba wananchi wanaishi kwa hofu na kwamba kumekuwa na matukio ya utekaji nyara.

Lissu: Sasa shahidi, ulisema ulipata taarifa ya Shura ya Maimamu. Ilisemaje?

Heche: Shura ya Maimamu ililaani matukio ya mauaji.

Wakaeleza namna ambavyo uchaguzi ulikosa sifa ya kuitwa uchaguzi.

Ilikemea namna ambavyo vyombo vya dola vilitumia nguvu iliyopitiliza.

Lissu: Ulisema umepata taarifa za waangalizi wa uchaguzi.

Heche: Nilipata taarifa ya uchaguzi ya AU (African Union).

Taarifa ya waangalizi wa uchaguzi ya SADC.

Taarifa ya uchaguzi ya Afrika Mashariki (East African Community).

Lissu: Taarifa zote zilitolewa tarehe gani?

Heche: Zote ni za mwezi Novemba mwaka jana.

Ripoti ya East African Community

Lissu: Tuanze na taarifa ya waangalizi wa Afrika Mashariki (East African Community).

Heche: Taarifa ya Afrika Mashariki inasema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na hakuna lolote lililojitokeza.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama taarifa hiyo ya Afrika Mashariki iliona mauaji makubwa yanayolalamikiwa kutokea.

Heche: Haijasema lolote kuhusu kuwepo kwa mauaji.

Lissu: Vipi suala la kuchoma miundombinu kwenye hiyo ripoti?

Heche: Hawajasema lolote kuhusu kuchomwa kwa miundombinu.

Lissu: Wakumbushe Waheshimiwa Majaji ni nchi gani zinaunda Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Heche: Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi, Congo na Sudan Kusini.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, katika hizo nchi—Kenya, Rwanda, Burundi, Congo na Sudan Kusini—hali ya demokrasia ikoje?

Heche: Kwa nchi zote hizo, ukitoa Kenya, hali ya demokrasia katika hizi nyingine ni mbaya.

Uganda ipo chini ya Rais Museveni, ana miaka 30 na zaidi.

Lissu: Rwanda je?

Heche: Huko nako Rais alipata kura asilimia 98, zaidi ya asilimia 97.6 ya Samia.

MAHAKAMA: Kicheko.

Ripoti ya SADC

Lissu: Twende kwenye ripoti ya SADC.

Heche: Wanasema uchaguzi haukufikia viwango vya kidemokrasia kwa nchi za SADC.

Wamezungumza pia matatizo waliyokutana nayo siku hiyo ya uchaguzi, kwa sababu palikuwa na vizuizi vilivyotokana na zuio lililotangazwa mapema saa 5 asubuhi siku ya uchaguzi.

Lissu: Wamesema nini juu ya matukio ya mauaji?

Heche: Waheshimiwa Majaji, waliongelea na kusikitishwa na matumizi makubwa ya nguvu.

Walizungumzia taarifa za mauaji katika uchaguzi na siku yenyewe ya uchaguzi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…