Kesi za ndoa na talaka 1,358 zafunguliwa ndani ya miezi 8 Dar es Salaam

Kesi za ndoa na talaka 1,358 zafunguliwa ndani ya miezi 8 Dar es Salaam

100% nikiwa mkubwa nataka kuwa kama wewe mama D

NB: Everyone anapaswa kusoma hiki ambacho umeeandika, esp. ile jinsia M
Umemsifu bure tu mama D, yeye anazungumzia imani na tamaduni zetu ndio zitadumisha ndoa, Hii ni self contradictory kwa sababu imani zetu na tamaduni zetu zinatofautiana, na zingine zinapingana waziwazi, tamaduni ipi na imani ipi ndio inayodumisha ndoa?
 
Nikadhani umeelewa. Sasa usikosoe kabla hujaelewa. Ungeuliza swali lako tu ili ujibiwe. mama D ndiyo funga kazi wa masuala hayo, msikilize utapa mume mwema (or mke kama ni mkaka)
 
Nikadhani umeelewa. Sasa usikosoe kabla hujaelewa. Ungeuliza swali lako tu ili ujibiwe. mama D ndiyo funga kazi wa masuala hayo, msikilize utapa mume mwema (or mke kama ni mkaka)
Nimeeleza sababu za kukosoa ambazo ziko katika mfumo wa swali, kama unaweza kujibu swali itakuwa vizuri, kama huwezi pia ni sawa tu.

Umemsifu na kumuweka kama role model wako, nikataka kukuonyesha kuwa huyo unayetamani kuwa kama yeye, hoja yake haina mashiko.
 
Hivi ni visingizio. Tatizo mnatafuta perfection katika character ya mwenza jambo ambalo si sahihi. Kila mtu anamapungufu ambayo yanamfanya aonekane ni tatizo kama ukiyapa uzito hayo mapungufu.
Nahisi wanawake tangu zamani walikua wanateseka ila kutokana na kukosa vipato walikua wanaona hawana pa kwenda
Sikuhizi mateso ni yaleyale yanaendelea tofauti ni kipato
Wanaona kama namudu kula na nini si nikakae tu mwenyewe?

Inasahauliwa hitaji la ndoa ambalo ni company ya mwenza na muishi vizuri

Nahisi wakikosa company mf mume vimada sana na mwenza hakuna maelewano basi inafikia tamati

Watakaodumu sana ndoani ni wale hata kama ana kipato basi ameamua kukaa kwa kuwa anapata company ya mwenza
Ama kama haipati anaona bora liende nisogeze siku tu😅
Ila kuachana nako process jmn
Mtu anakua amekuchoka kiasi gani daah
 
Maadili tu hakuna,jamii imeoza..na huanzia nyumbani,pia tangu mwanamke ajue haki zake ndoa zimekua shinda
Ina maana walikua wananyanyasika sana ama?
Ila kuna kitu upande wa wababa nako huwa hawakubali mhh
Haya ngoja tuone

Lakini zama hizi mhh
Ni kuwa makini sana
Oa mtu ambae unaona ana uhitaji na hiyo ndoa na pia jitahidi usimkere sana vipigo nk
Wanawake sikuhz spana mkononi
 
Tumeshaambiwa wanawake ni kama wanasiasa kabla ya ndoa wapole kweli ilia wakishaolewa na kupata watoto mwanaume huna thamani tena
 
Mume ama Mke ni kama vazi kwako imeandika Quran
Ukimkosa ni kama umekosa vazi/stara flani
Tustahimiliane hasa kwa yale yanayovumilika na kurekebishika

Ila ikishindikana kabisa basiii
Tusiuane
Heri kuachana
 
Tumeshaambiwa wanawake ni kama wanasiasa kabla ya ndoa wapole kweli ilia wakishaolewa na kupata watoto mwanaume huna thamani tena
Wanawake wananyanyasika na kusemwa vibaya na jamii wasipoolewa..na wasemaji hasa ni wanaume na wadanganyaji pia

Hivyo baadhi wanaingia ndoani kutoa nuksi wakati mume kapenda
Lazima kiumane
 
Wanawake wananyanyasika na kusemwa vibaya na jamii wasipoolewa..na wasemaji hasa ni wanaume na wadanganyaji pia

Hivyo baadhi wanaingia ndoani kutoa nuksi wakati mume kapenda
Lazima kiumane
Ndoa nyingi za wanawake kutoa nuksi tuu huo ndio ukweli wa mambo.
Ni shida ndio maana watu tunaamua kugeggeduana tuu
 
Hakunaga jambo kama kushindwa kuishi pamoja. Ila kuna mwenye tabia mbovu kumsumbua ambaye ana mwenendo mzuri.

Sasa nikuulize, mfano huyo dada hapo, kwa hizo tabia zake, wahisi jamii (wazazi wake,ndugu,rafiki,majirani,serikali na taasisi)ingemkazia na kumkemea na kupewa sanctions kutokana na matendo yake angeendelea kumsumbua mwenzake?!

Kama unatetea watu kuwa huru kufanya wanavyojiskia na kufuata wehu wa vichwa vyao unavyowapelekesha, then tusizungumzie kumomonyoka kwa maadili, watoto wa mitaani, rushwa serikalini, viongozi wa hovyo serikalini, uhalifu, magonjwa ya zinaa. Sababu haya yote yanachangiwa na mahusiano mabovu kati ya mume na mke, lakini zaidi yanachangiwa na mfumo mbovu wa malezi ya watoto na mazingira mambovu ya amani majumbani.
Kila mtu ana autonomy yake na maamuzi yake. Tatizo jamii yetu inapenda unafiki, watu hawaishi maisha yao, wanataka kuishi maisha ya kupangiwa na jamii. Ndiyo maana unakuta mwanamke anapigwa mpaka anataka kuuawa, lakini yupo katika ndoa tu, anaogopa aibu ya talaka, mwishowe anauawa.

Sasa mimi hapo naona talaka inaweza kuokoa maisha ya huyo mwanamke, kati ya talaka na mwanamke kuuawa, naona bora talaka.

Hata mwenye tabia mbovu naye ana haki ya kuishi na tabia mbovu yake kama anaataka.

Sasa kwa nini alazimike kuishi na mtu mwenye tabia nzuri wakati anaona hawaendani?

Mifano yako inachanganya mambo ya personal autonomy na mambo ya public responsibility/ sheria.

Rushwa serikalini ni suala la sheria, kuna sheria.

Mambo ya mke kushindwa kuishi na mume kwa sababu mume mlevi hayako clear cut kama rushwa serikalini.

Kwa hivyo, unapofananisha vitu, fananisha vinavyofanana.
 
Je? ni Fahari kwa mahakama kufungua mashauri mengi ya talaka?

nadhani kuna haja ya kutumia vyema mabaraza yetu ya usuluhishi ili kunusuru ndoa za watu.

Pia mahakama isishangilie mashauri mengi kufunguliwa mahakamani, wanao wajibu wa kutoa elimu ili kunusuru ndoa za watu.
 
Maadili tu hakuna,jamii imeoza..na huanzia nyumbani,pia tangu mwanamke ajue haki zake ndoa zimekua shinda
Mpumbavu pekee ubomoa ndoa yake kwa kupaste aonacho.
Mwanzilishi wa ndoa alitengeneza mfumo, sheria na kanuni Ili ndoa idumu kuanzia uchaguzi wa mtu sahihi, jinsi ya kuishi pamoja, malezi ya watoto, nk. Sema tu binadamu tuna ubinafsi ndio upelekea talaka.
 
Aisee!? Shida wengi wanaingia kwenye hizo ndoa wakiwa wahajakomaa kiakili wanazania wataishi daima kama walivyo kuwa wanaishi maisha ya uchumba
Kwahiyo ndo umeghairi Ile issue?
 
Back
Top Bottom