TANZIA Kibaha Vijijini: Diwani Mteule wa CCM Kata ya Kikongo afariki pamoja na wajukuu zake wawili baada ya nyumba yao kuchomwa moto

TANZIA Kibaha Vijijini: Diwani Mteule wa CCM Kata ya Kikongo afariki pamoja na wajukuu zake wawili baada ya nyumba yao kuchomwa moto

Ni diwani mteule kata ya kikongo wilaya ya kibaha,bi Fatma Ngozi kupitia CCM Amekufa pamoja na wajukuu zake wawili baada ya nyumba yao kuingia moto waliokuwa wamelala.

Source: Mwananchi fb page

Mteule diwani alale anapostahili
 
Jiwe anajitayarishia mazingira magumu mno sasa.
Leo tena...

Kamanda wa Polisi Pwani, Wankyo Nyigesa amethibitisha kuwa Diwani Mteule Kata ya Kikongo Kibaha Vijijini (CCM), Fatuma Ngozi na wajukuu zake wawili wamekufa baada ya nyumba yake kuchomwa moto usiku wa kuamkia leo.


Huu mfumo tunaoingia wa chama kimoja, Mungu atulinde.

Diwani mteule Kata ya Kikongo Kibaha Vijijini (CCM), Fatuma Ngozi na wajukuu zake wawili wamekufa baada ya nyumba yake kuchomwa moto usiku wa kuamkia leo, Kamanda wa Polisi Pwani, Wankyo Nyigesa amethibitisha. #MwananchiUpdates

Tanzania tunakoelekea ni giza nene.

Sad. Watanzania tumefikishwa hapa!

Poleni wafiwa. Watanzania tumeingizwa kwenye tanuru la moto kwa uchoyo wa mtu mmoja.

Wana tafuta justification uharamia walioufanya Zanzibar na Tanzania bara.
 
Daaah jaman udiwani tu watu washamtendea uovu huo.
 
Mkuu umekosea kiswahili kidogo, kuuawa maana yake ni mtu anahusika kuutoa uhai wako mfano kupigwa bunduki ,kupigwa mawe nk,kwa huyo diwani kafariki kwa ajari ya moto
Na wewe umekosea mkuu, sio "kupigwa bunduki" Ni "kupigwa risasi"
 
[emoji1630]NEWS ALERT

Diwani Mteule Kata ya Kikongo Kibaha Vijijini (CCM), Fatuma Ngozi na wajukuu zake wawili wamekufa baada ya nyumba yake kuchomwa moto usiku wa kuamkia leo,Kamanda wa Polisi Pwani,Wankyo Nyigesa
IMG_20201109_160034.jpg
 
Pole sana kwa wafiwa.
Polisi wawasake wahalifu halisi wawatie kwenye mikono ya sheria.
 
Nyumba imechomwa au imeungua?

Polisi wetu na zimamoto ni mavi ya kuku, washafanya uchunguzi au kwakuwa ni diwani wa CCM basi atakuwa amechomwa?
 
Labda hitalafu ya umeme jambo hili pia tuliangalie kwa makini wasije kamatwa watu ambao hawakuhusika kabisa na tukio hilo
 
Kauli ya viongozi inaonesha nyumba ya diwani haiwezi kuungua isipokuwa kwa kuchomwa moto! Tatizo la viongozi kuwa na mtazamo hasi na wapinzani.
 
Diwani mteule wa kata ya Kikonko mkoani Pwani mh Fatma na wajukuu wake wawili wamefariki dunia baada ya nyumba yake kuchomwa moto na watu wasiojulikana.

RC Ndukilo amesema kuna msako mkali unaendelea wilayani Kibaha kuwasaka wauwaji.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Innalillah wainaillahi rajuun.Vyombo vya usalama vifanye kazi yake na wahusike wafikishwe kwenye mkono wa sheria. Mwenyezi Mungu aepushie mbali lisiwe ni tukio la kisiasa.
 
Back
Top Bottom