Kibarua kimeota Nyasi: Waliozoea siasa za vita Mbowe, Lissu, Rais Samia waungana kujenga nchi. Funzo kwa...!

Kama iliwezekana kufanya urafiki kati ya Seikali na Dr. Silaa (Padri ), urafiki kati ya Serikali na Mbowe (mchaga) ni rahisi zaidi!

Hizo siasa za udhaifu wa kikabila, kajadiliane na wanafunzi wenzio wa chuo cha uongozi cha CCM.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Huu urafiki wa Mbowe na serikali baada ya kufutiwa kesi inabidi tuutazame kwa umakini mkubwa. Kwa sasa nasubiri muda nione muelekeo, lakini sio siri nina mashaka makubwa.
Mku ninaamini Mkutano Mkuu utawajia na majibu mazuri kwani mwelekeo ndo utatokea hapo
 
Kwanini vijana wengi wa uvccm mnaonekana kuumizwa na kitendo cha mbowe kukutana na rais ikulu? Pia kwanini mnaonekana kuchukia pale ambapo viongozi wanaonyesha dalili za kuleta maridhiano katika Taifa?
 
Laana ya kushangilia kifo cha Magufuli itawatafuna milele Mbowe na Lisu.

Hata mwaka haujaisha saccos yao inakiona cha moto
Mke wake mwenyewe alishangilia sembuse hao ulio wataja! Ona mama ananawiri sio mchezo.
Tuache hayo, kinachofanywa sasa hivi kati ya Rais Samia na viongozi wa Chadema ndio kitu sahihi kwa taifa hili na mwanzo mzuri kuelekea maendeleo ya kweli na kuheshimu haki.
Muhimu tuu Samia asiwachekee wahafidhina walioko kwenye chama chake kwani wengi walishaingiwa na roho mchafu wa Magu.
 
Ndo maana nakuambia kikubwa ni kuwa na subira
 
Marekani kuna Siasa za Kistaarabu ? Hili neno Gutter Politics sidhani kama lilikuwa coined Tanzania au Africa...

Current Politics and Politicians world over wamekuwa ..., well... Politicians....
 
Una Mihemuko kama shivasi
 
Tuna hilo tatizo chief, kila kitu wanasubiri Rais aseme, ni wakati sasa wa kutoa hawa watu wenye mavitambi kwenye mamlaka, ni wapuuzi sana! Mimi ningekuwa hata OCD tu Makonda ningekuwa nimeshamnyoosha, ila hii mijinga inakaa eti inasubiri kauli ya Rais!!! samia ana shida sana na hawa wasaidizi wake vilaza wanaojali mitumbo yao
 
Hakuna urafiki wa Simba na Swala! Subiri uchaguzi wa 2025 harafu kitakachotokea hapo utatuambia.
Hakuna Urafiki wa CCM na Vyama vya Upinzani.
 
Amini mkuu at least hii miaka ya mama angalau tunaweza kufanya siasa za kistaarabu kwakuwa tupo chini ya uangalizi wa wenye fedha .

Haikuwa rahisi kwa mh Mbowe kufutiwa haya mashitaka.

Lazima kuna msukumo fulani nyuma ya pazia na kwa kuzingatia hilo amini kwa miaka atakayokuwepo madarakani kutakuwa na siasa za kistaarabu hata kama ni kwa kuviziana.
 
Kahangaikeni na cuf yenu iliyo mezwa na Zitto
 
Kwa ufupi mazingira tunayo enda kuyaishi ni sawa na jirani zetu wa Kenya.
 
Ebu tuwe wakweli kidogo......

Mbona ile
"Join the Chain"
imeondolewa mitandaoni ghafla baada ya ujio wa mwenyekiti Mbowe?
 
Umelenga "Bull" mkuu!
 

Mwenye kuchagua mitulinga au ustaarabu ni Samia. Si Chadema wala si CCM.

Si CCM, kwani nani ana ubavu wa kauli au msimamo upi huko zaidi ya Samia?

Si Chadema kwani Samia akisisitiza haki zote zikiwemo za hao Chadema kuheshimiwa nani atakuwa na ugomvi na hilo?

Samia ajue akiminya haki za watu ni hakika kuwa atakayokuwa akiyapata ndiyo majibu yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…