Kibongo Bongo wafanyakazi hawazijui Sheria za kazi. Wananyanyasika sana bila kujua haki na wajibu wao

amshapopo

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2014
Posts
1,834
Reaction score
4,161
Habari,

Ni ukweli usiopingika kwa ajira hizi tunazofanya bila kujua haki na wajibu wako ni kazi sana kutoboa. Wafanyakazi walio wengi hawajui haki na wajibu wao katika kazi wanazo zifanya. Mfano Sheria ya Kazi inasema mfanyakazi anatakiwa kufanya kazi masaa nane, yanayozidi baada ya hapo inatakiwa kulipwa overtime. Lakini ukiangalia kwenye kampuni nyingi na mashirika ya umma Sheria hizi hazizingatiwi. Boss anaweza kupanga mda wake anavyojisikia na wafanyakazi wakafuata bila shurti bila kujali haki zao zinapotea. Unakuta siku kama ya leo ni Maulid ila boss akaamua muende kazini bila kuwa na allowance yoyote na usipoenda kazi huna😂😂😂. Kweli kwa mfanyakazi kutoboa kibongobongo ni kazi sanaaa

Muwe na siku njema!
 
Kweli ila ukiuliza utapewa sababu , mara nyingi wanakuambia wamejumlisha kweny mshahara hizo overtime .

Muda wa ziada/overtime hauko sawa kila mwezi, ni lazima ionyeshwe kwenye mshahara wako kama kipengele kinachojitegemea(umefanya masaa ya ziada ya thqmqnu gani kila mwezi), baada ya hapo itajumlishwa kwenye mshahara.

Hii itasaidia pia kujua kiasi cha masaa ya ziada uliyofanya kwani pia yana ukomo wake kisheria kwa mwezi.
 
Habari,

Ni ukweli usiopingika kwa ajira hizi tunazofanya bila kujua haki na wajibu wako ni kazi sana kutoboa. Wafanyakazi walio wengi hawajui haki na wajibu wao katika kazi wanazo zifanya. Mfano Sheria ya Kazi inasema mfanyakazi anatakiwa kufanya kazi masaa nane, yanayozidi baada ya hapo inatakiwa kulipwa overtime. Lakini ukiangalia kwenye kampuni nyingi na mashirika ya umma Sheria hizi hazizingatiwi. Boss anaweza kupanga mda wake anavyojisikia na wafanyakazi wakafuata bila shurti bila kujali haki zao zinapotea. Unakuta siku kama ya leo ni Maulid ila boss akaamua muende kazini bila kuwa na allowance yoyote na usipoenda kazi huna😂😂😂. Kweli kwa mfanyakazi kutoboa kibongobongo ni kazi sanaaa

Muwe na siku njema!

Kabla ya kudai muda wa ziada/overtime, ni vyema kujua pia kuna muda wa mapumziko kwa wale wanaofanya kazi kwa zaidi ya saa tano. Mfano: unaweza kukuta saa za kazi ni 81/2, nusu saa ni mapumziko na chakula.
 
Muda wa ziada/overtime hauko sawa kila mwezi, ni lazima ionyeshwe kwenye mshahara wako kama kipengele kinachojitegemea(umefanya masaa ya ziada ya thqmqnu gani kila mwezi), baada ya hapo itajumlishwa kwenye mshahara.

Hii itasaidia pia kujua kiasi cha masaa ya ziada uliyofanya kwani pia yana ukomo wake kisheria kwa mwezi.
Ndugu yangu hawana huo muda kabisa , nimefanya kazi tunaingia saa moja mpaka 12 jioni, almost masaa 11 tena mpaka jumamosi .

Wnasema ndio kazi zao wala hamna muda wa ziada
 
1: Una mkataba wowote wa hiyo kazi?
2: Je huwa mnapata chakula(ili uondoe huo muda wa chakula)?
3: Unasaini kila unapoingia na kutoka kazini?
4: Mwajiri hatakiwi kujitengenezea sheria yake nali kuboresha kwa kuzingatia sheria mama ya kazi.
5: Kama una namba moja na tatu hapo juu, pata ushauri wa kisheria kwa mwanasheria kuangalia nafasi yako kwenye sheria ya kazi.
 
Hiyo serikali kma unabisha uliza watumishi wengi tu wanapitia hiyo .
 
Masaa nane au yasizidi masaa 12 kwa siku na masaa hayo yafanye jumla ya masaa yasiyozidi 45 kwa wiki.
 
Habari,

Ni ukweli usiopingika kwa ajira hizi tunazofanya bila kujua haki na wajibu wako ni kazi sana kutoboa. Wafanyakazi walio wengi hawajui haki na wajibu wao katika kazi wanazo zifanya. Mfano Sheria ya Kazi inasema mfanyakazi anatakiwa kufanya kazi masaa nane, yanayozidi baada ya hapo inatakiwa kulipwa overtime. Lakini ukiangalia kwenye kampuni nyingi na mashirika ya umma Sheria hizi hazizingatiwi. Boss anaweza kupanga mda wake anavyojisikia na wafanyakazi wakafuata bila shurti bila kujali haki zao zinapotea. Unakuta siku kama ya leo ni Maulid ila boss akaamua muende kazini bila kuwa na allowance yoyote na usipoenda kazi huna😂😂😂. Kweli kwa mfanyakazi kutoboa kibongobongo ni kazi sanaaa

Muwe na siku njema!
Ni kweli kwamba wafanyakazi/watumishi wanapigwa sana kwa sababu hawajui sheria na kutokujua huko pengine sio kosa lao kwa sababu hawajasomea sheria kwa undani sana.

Nafikiri wale wataalamu wetu waliosomea na kubobea ktk sheria wanajukumu la kutoa elimu kwa jamii (wafanyakazi /watumishi) kupitia njia mbalimbali kama jukwaa hili la JF ili kuwawezesha kutambua haki na wajibu zao ambazo zipo kisheria.

Pia maofisa utumishi (Human resource officers) wana nafasi kubwa kusimamia haki na wajibu wa wafanyakazi/watumishi na sio kuwa upande wa mwajiri tu.
 
Back
Top Bottom