Pre GE2025 Kigaila: Rais Samia hajaanzisha mradi wowote tangu awe Rais isipokuwa mradi wa mabango ya Mama anaupiga Mwingi!

Pre GE2025 Kigaila: Rais Samia hajaanzisha mradi wowote tangu awe Rais isipokuwa mradi wa mabango ya Mama anaupiga Mwingi!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
hiyo mikopo ya t39+ bado na mapato ya ndani ndio imetumika kukamilishia miradi tu, kwa mikopo hiyo na mapato ya kodi tulitegemea alichokifanya jpm huyu mzanzibar akifanye mala nne zaidi.

kwa miradi aliyofanya mzanzibar bado hajafikia hata kwa awamu ya Kikwete sema huyu ni rais anaetembea na trend kiufupi huyu mzanzibar anaturudisha nyuma
Mkuu, unahangaika kuuliza swali hili kwa kichwa cha mccm?

Ccm inamradi wa kuzalisha wajinga, enewei..! Ngoja tuone iwapo atajibu
 
Hivi kuanzisha miradi kwa kutumia hela ya walipa kodi ni kazi ngumu kiasi gani?
Nchi hii taaluma kuhusu mikakati na mipango ya maendeleo ya taifa zilishakufa kitambo.

Sasa hivi “Rais kuanzisha miradi” ndiyo propaganda inayoeleweka na wajinga wengi sana.

Wengi hawajali kujua undani wa hiyo miradi ya maendeleo-katika mpangilio mzima wa mpango wa maendeleo ya taifa, gharama zake, na vyanzo vyake vya fedha. Wanaburudika tu kusikia viongozi wakitangaza miradi na mabilioni ya shilingi yaliyotengwa. Utafikiri ni kama shughuli ya kuwasha na kukimbiza mwenge vile.

Ndio maana ni vigumu Watanzania kuwa na uelewa kama ule uliofanya wananchi wa Kenya kuhoji na kuukataa muswada wa fedha (finance bill) uliowasilishwa pamoja na bajeti ya taifa. Walielewa athari zake kwenye uchumi wa taifa na wao binafsi. Ikabidi mpango wa maendeleo upunguzwe.

Inayoitwa “miradi ya Magufuli” peke yake imeitwisha nchi mzigo mkubwa sana wa mahitaji ya fedha za maendeleo. Na bado sana kukamilika. Inagharamiwa na mikopo mikubwa tu. Halafu watu wanatarajia Samia naye aanzishe “miradi yake” huku akitekeleza ya mtangulizi wake! Sijui kama hao watu wanaelewa financial implication yake.

Kwamba kuna ufisadi mkubwa ni dhahiri. Ukiondoa awamu ya kwanza, hadi leo hii hakuna wakati Tanzania haijawahi kuwa na ufisadi mkubwa.

Na mnapowapa watawala uhuru wa kutumia hazina ya taifa bila kuhojiwa na kuanzisha miradi wanavyojisikia ndio mnawaongezea fursa na ujasiri wa ufisadi. Mara Rais anavunja tume ya mipango, mara anakataa feasibility studies kwenye miradi mikubwa, mara anazuia ukaguzi kwenye baadhi ya miradi, mara bunge na mahakama wanatahadharishwa kutoenda kinyume na serikali! Huku wananchi wame-relax kabisa.

Tunahitajika kuwa na fikra kubwa katika mambo ya msingi ya taifa. Kuendekeza propaganda nyepesi nyepesi kunazidi kuiangamiza nchi.
 
Kaka wewe nikikuita MJINGA unaonaje??

Kama vyama vya siasa ni wasanii na wachekeshaji, vipi ofisi ya msajiri wa vyama vya siasa tuiteje?? CHOO YA STENDI "???

Na msajiri naye tumwiteje?? KINGWENDU au BAMBO??

Punguza UCHAWA na ujinga ulopitiliza mkuu, TEUZI hazitafutwi namna hiyo.
Hivi wewe una tofauti Gani na mtu ambaye hakwenda shule kabisa??

You have generated very stupid argument.😃🤔🤔🤔

Kutoka kwa mtu wa CPA???🤣🤣🤣
Jikite kwenye mada husika, usirukikie vitu. mada iliyopo mezani inayojadiliwa ni kauli ya kigaila kusema hakuna mradi wowote ulianzishwa na Rais Samia na Comment yangu ilijikita kwenye mada husika kama ulitaka kuzungumzia habari za ofisi ya msajili ungeanzishia uzi wako na ningekuja kuujadili kivingine. Tujikite kwenye mada vinginevyo tutaonekana vituko.

tuweke ushabiki pembeni tujadili uhalisia ulivyo na nitakuuliza swali: Je ni kweli hakuna mradi hata mmoja ulianzishwa na Rais Samia?

Mradi wa BBT
Mradi wa DMDP II
Mradi wa Royal Tour
Mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo
Mradi wa DP World
ni mifano ya miradi iliyoanzishwa na Samia

Au unadhani miradi ni lazima iwe 'tangible'?
 
H

Huyu nyumba aisee ni shida ,hivi Dar yote iko kwa ukarabati wa barabara ndio yeye alianzisha ? Hivi alitaka aache kukamilisha miradi aliyoanzisha mtangulizi wake ?Nyumbu hamjui jinsi nchi inavyoendeshwa .
Ukarabati wa barabara za DSM ni DMDP2 baada ya DMDP1 kukamilika.
 
Ni huu upuuzi wa kila mtu kuanzisha miradi ndio inapelekea ufujaji wa Kodi zetu na kujitwika madeni..., Ifike wakati kama nchi tuwe na short, middle na long term plans ya mambo ya kufanya..., Kama Nchi (na sio kama Chama) Rais yoyote akija yeye ni kusimamia..., Sababu naona vitu kama vilivyo vinatugharimu...
 
Jikite kwenye mada husika, usirukikie vitu. mada iliyopo mezani inayojadiliwa ni kauli ya kigaila kusema hakuna mradi wowote ulianzishwa na Rais Samia na Comment yangu ilijikita kwenye mada husika kama ulitaka kuzungumzia habari za ofisi ya msajili ungeanzishia uzi wako na ningekuja kuujadili kivingine. Tujikite kwenye mada vinginevyo tutaonekana vituko.

tuweke ushabiki pembeni tujadili uhalisia ulivyo na nitakuuliza swali: Je ni kweli hakuna mradi hata mmoja ulianzishwa na Rais Samia?

Mradi wa BBT
Mradi wa DMDP II
Mradi wa Royal Tour
Mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo
Mradi wa DP World
ni mifano ya miradi iliyoanzishwa na Samia

Au unadhani miradi ni lazima iwe 'tangible'?
Ama una elimu finyu ya "kiCCM" au huna uelewa wa maana ya miradi ya kitaifa na kimkakati.
 
Ila hawa jamaa wana hoja zisizojibika na ndio maana wanatekwa na wana maneno yanachoma kama kisu...
 
Mnasafari ndefuu Sana kama mnatofautiana wenyewe kwa wenyewe Tena public kabisa.
 
Ama una elimu finyu ya "kiCCM" au huna uelewa wa maana ya miradi ya kitaifa na kimkakati.
Nakusikitikia maana unakokotwa kama mkokoteni, kesho kigaila akikana kauli yake basi aibu itakushukia wewe ila shukuru una ID fake maana familia yako ingekudharau pia. Natamani kuona upinzani imara na wenye hoja nzito lakini si huu wa kigaila na wenzake. Miradi inatekelezwa na inakamilika, wananchi wanapongeza na mpaka hizo pongezi zinawakera, lakini anatokea mtu mmoja anasema hakuna mradi na kundi la watu linashangilia ni kweli bila kujua anayesema hivyo anawaona wajinga kiasi gani
 
Unaelewa maana ya "miradi ya kimkakati"!!??
Nimemkumbuka Rutabanzibwa, Rugunyamheto, Likwelile,Rutabanzibwa na Rugemalira.
 
Je, kulikuwa na ulazima wa kisheria wa DMDP II kuwepo baada ya awali kumalizika? kama hakukuwa na ulazima wa kisheria basi ni mpya na ni wa kwake, nafikiri unanielewa pia
Makubaliano ya awali na World Bank yalikuwa ni kuwa na awamu 3 za DMDP ambazo zitatekelezwa baada ya kila awamu kumalizika na kupata perfomance index.
Unaelewaa?
 
Unaelewa maana ya "miradi ya kimkakati"!!??
Nimemkumbuka Rutabanzibwa, Rugunyamheto, Likwelile,Rutabanzibwa na Rugemalira.
'Ni miradi mikubwa yenye vipaumbele inayotekelezwa na Serikali ambayo inalenga kuongeza ushiriki wa Watanzania (Local Content) katika sekta mbalimbali za kiuchumi. Miradi hii iwe ni ile yenye uwezo wa kutengeneza ajira kwa nguvu kazi ya ndani, na utoaji wa huduma za ndani'. usishupaze shingo mwenzako kigaila alisema hayo akiwa amelewa chakari ndio maana mnaofanya kazi ya kutetea kauli yako mtaabika
 
Back
Top Bottom