Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Mastakiraka una hoja dhaifu sana.Sheria za nchi zinasemaje?

Hivi kila mtu aamue kujichukulia sheria mkononi itakuwaje?

Muhimili wa mahakama una kazi gani?
Kama unazijua sana sheria za nchi anzisha taasisi yako ya kutetea haki za wezi/vibaka.
Sheria za mtaa zinasaidia kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani.
Tunaiacha mahakama ijishughulishe na Kesi kubwa kubwa kama za Ugaidi, Ufisadi etc.
 
Wanatusumbua sana hao,,, wanakaba wazi wazi kabisa alafu mama zao wanawatetea,,, mi nikajua labda huyo dogo anakaa mbezi, kumbe mabibo,, huyo kibaka tu,, maeneo kama mabibo,mburahati,kigogo, manzese, tandale, mwananyamala, Argentina na kagera mikoroshini haya ni maeneo korofi kwa tabia hizo za wizi vijana wadogo kabisa,,, na ndio maana raia wamechoka na kujichukulia maamuzi kwa kuwa hata wakipelekwa vituoni wazazi wao wanawawatetea,, sasa tutafanya kama tulivyofanya kipindi cha komando yosso,, msako nyumba hadi nyumba.
Hivi komando Yosso alikuwa nani hasa?
 
Hiyo haijalishi mama PGO ya mtaa inasema kama ni kibaka lazima auliwe mapema kabla hajaleta madhara makubwa

Kwasababu nyie wazazi wake kile kipengele cha PGO hamkutekeleza kinachosema umlee mtoto wake ktk maadili mazuri kabla hajakomaa
Wazee hii PGO mnavyotambaa nayo [emoji23][emoji23][emoji23]
 
denda nowdays katulia..pamoja na Roja mtambo wote wapo Calm..mkuu unaweza ukawa jirani yangu ww.
Hao wote wana sema wao ndio wakaamua kuwa wezi,baada ya kukaa jela karibia miaka 7 now denda katulia ila huyo roja alipelekwa tena jela sijui kama katoka,mitaa hiyo ss hivi niki but ndio .......
 
Hao wote wana sema wao ndio wakaamua kuwa wezi,baada ya kukaa jela karibia miaka 7 now denda katulia ila huyo roja alipelekwa tena jela sijui kama katoka,mitaa hiyo ss hivi niki but ndio .......
Mkuu unagusa mle mle..sema Niki sahv katulia..Jela imemfunza..na Hata Shaban babu nae kidogo alichipukia ila sahv katulia.
 
Ngoja siku wakupole Simu huku wakikuchoma kisu cha kalio ndio utajua hujui
Miaka ya nyuma walikua wakipigwa wezi nilikua siwezi kusogea,na ilikua aipiti muda naona matukio ya kupigwa wezi roho ilikua inaniuma sana wanachofanyiwa,ila baada ya kuniibia kama mara 2 tena tukio moja nyumbani usiku,sijawahi kukutana na tukio na mwizi akipigwa na siku nikikuta sehemu anapigwa mwizi na nikathibitisha ni mwizi kweli,atajua kama hajui aisee
 
Raisi ata ingilia mamb ma ngapi ndo maana kukawepo na viongozi wengine eg Dc.RC waziri wa ulinzi .....




Ila dgo kwenye picha kakaa kiwizi
 
Umenena vizuri, umesema Kuna mtu anaitwa samwel ameshiriki kwenye mauaji hayo, sasa kwann usimpeleke mahakamani maana ni bora zaidi kuliko ulivyomtaja humu jamii forum.
 
Mheshimiwa raisi, Mama Samia Suluhu Hassan, sisi wanawake tuna Imani sana na wewe, tutakupa kura zetu zote za urais mwaka 2025 ila kuna mambo machafu sana yanayofanyika katika serikali yako.

Sisi wanawake wa Tanzania tumesikitishwa sana na mauaji ya kijana mdogo mkazi wa kata ya Mabibo kitongoji cha Soweto yaliyofanywa na watu wanaojiita Sungu sungu.

Kijana huyo anaitwa Jumanne Jongo.Ameuawa kikatili sana kwa kukatwa miguu na mikono.

Cha ajabu wauaji wa kijana huyu wanajulikana na hawajakamatwa hata mmoja.Taarifa nilizokuwa nazo bado wameahidi kuua vijana wengine wanaowahisi vibaka.

Genge hili la mauaji ya vijana linaongozwa na watu wanaojiita Sungu sungu kutoka kata ya Jitegemee ,Mabibo wilaya ya Ubungo.

Haya sio mauaji ya mara ya kwanza,huko nyuma sungu sungu hao wa Jitegemee wameshawahi kuua vijana wengi kwa kisingizio kuwa vijana hao ni vibaka.Hata kama ni vibaka kwa nini wasiwakamate na kuwapeleka Polisi?

Kwa nini sungu sungu wanajichukulia sheria mkononi?

Mh.Rais nchi yako ni nchi inayofata utawala wa sheria, iweje wapumbavu wachache watie doa uongozi wako?

Taarifa nilizokuwa nazo mauaji hayo yanapata baraka kutoka katika uongozi wa serikali ya mtaa wa Jitegemee chini ya mwenyekiti Kilema.

Hivi OCD wa Kinondoni hana taarifa ya tukio hili? Mpaka sasa hivi amechukua hatua gani? Anapata kigugumizi kipi cha kuwakamata wauaji hao wakiongozwa na mpumbavu mmoja anayeitwa Samwel?

Kwa taarifa yako mh.rais sisi wanawake wa Mburahati na Jitegemee tumeguswa sana na kifo cha huyu kijana, tunatafakari mara mbili mbili kuwa wanachama wa CCM.

Embu ukiwa kama rais tumia mamlaka yako kushughulikia suala hili.Maana sisi wanawake wenzako tuna wasiwasi sana kuhusu maisha ya watoto wetu wanaouawa kila kukicha na hawa watu walio juu ya sheria wanaojiita Sungu sungu.

Kuna hoja kwamba huyu kijana alikuwa kibaka,lakini sheria inasemaje? Kwani hukumu ya kibaka mauaji?

Chonde chonde mh.Rais fanyia kazi suala hili ikibidi mwajibishe kamanda wa Polisi wa Kinondoni kwa kushindwa kuwakamata hao wauaji wa huyu kijana.

Mbona hana neno?
 
Miaka ya nyuma walikua wakipigwa wezi nilikua siwezi kusogea,na ilikua aipiti muda naona matukio ya kupigwa wezi roho ilikua inaniuma sana wanachofanyiwa,ila baada ya kuniibia kama mara 2 tena tukio moja nyumbani usiku,sijawahi kukutana na tukio na mwizi akipigwa na siku nikikuta sehemu anapigwa mwizi na nikathibitisha ni mwizi kweli,atajua kama hajui aisee
Mimi waliweka ndole wakaiba simu yangu nilinunua haikukaa hata siku 3 nililia mpaka presha ilipanda toka siku ile nawachukia mno.
 
Back
Top Bottom