Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Wanama siwatetei kwani sheria za nchi zimebadilika?

Hivi unaijua sheria?
 
Chaliifransisco hao wahalifu sungusungu unaowatetea hawana mamlaka ya kuua hata kidogo...

Kazi yao kumkamata mhalifu na kumpeleka katika vyombo vya sheria...usitetee upumbabu...

Nchi yetu ya kistaarabu hatujafika hatua ya kuuana kama wanyama.
Wewe mama huyo mwanao kibaka alitoa wapi mamlaka ya udokozi toa ujinga wako hapa[emoji35]umekazana mamlaka mamlaka mamlaka ya konyooo
 
Kwa Suchak wewe umekuwa mahakama, kibaka amekuibia wewe?

Hata kama kibaka sheria za nchi zinasemaje? Usijitoe ufahamu chefuuu!!....
 
Sura ya kibaka kabisa hiyo. Ata meno ya mbele hana.
Lady Mwali atasema alipata ajali ya bodaboda.

Ukikuta mtu/watu wanajitetea kwa kung'ang'ania neno "sisi Watanzania", ujue wana lao jambo (wageni haramu).
Wahenga walisema ' MTOTO MPUMBAVU, NI MZIGO KWA MAMA YAKE'
 
Nyinyi ropokeni tu...kaeni mkijua mnachofanya ni unyama wa Hali ya juu...unawezaje kumuua binadamu mwenzako kama unaua paka?

Kama mna hasira nendeni kuua wauza madawa ya kulevya,wala rushwa na wahujumu uchumi.
Kama mtu anauza madawa na mimi situmii madawa naweza kusema hainihusu sana,kama mtu ni fisadi ila hajanifisidi mimi naweza kupotezea tu,mtu anayeitwa mgujumu uchumi hata sijui anafananaje! Ila kibaka mchoma visu na mpora mali huyu ananihusu 100% ntamuua hakika!!maana hata yeye akinipatia nafasi ataniua!! Kama una mwingine ambaye ni kibaka ningekuomba utusaidie kumuua nwenyewe! Kama huwezi basi sisi tuta muua,na tukishamuua utupe pole na pongezi,maana hata wewe wanaweza kukuua siku moja,japo nipo ghana/acra nimefarijika kujua kwamba kuna kibaka ameondolewa leo mtaani kwangu,ndugu zangu watakuwa na amani mno,na mimi pia.
 
Kiongozi, nikuambie tu, kwa watu ambao tumewahi kutana na hao vibaka! sio rahisi kuwatetea, wanaharibiana maisha sana!
Binafsi nimewahi kuchezea visu vya kutosha mwilini!

Sasa mtu kama huyo unadhani naweza kumtetea eti sheria imsaidie! hapana! vibaka wasumbua mnoo! na kama hujawahi kutana nao! zidi kumuomba Mungu akuepushe!

Ukionaga mwizi anachomwa moto, jua ameshalostisha watu kadhaa, afu amekanywa hakusikia, na huko kwenye sheria ni kama hakuna mafunzo kwake!
 
CCM oyeee.... tulieni kuongoze nchi - miluzi mingi...
 
Tatizo la kujichukulia sheria mkononi ni kwamba unaweza kumhukumu mtu ambaye hana hatia. Wanaoshutumiwa huwa hawapewi nafasi ya kujitetea. Ndio maana zimewekwa mahakama ili ziweze kutoa haki bila kuongozwa na jazba au hisia kali. Huyu raia ameshauwawa hatuwezi tena thibitisha kama kweli alikuwa mwizi au la…

Kwa maelezo yaliyotolewa hakukutwa katika tukio bali aliitwa kwa simu kisha akauwawa… mbinu ambayo inafanana kidogo na ile ya wale wasiojulikana. Nao bila shaka wanaamini kwamba wakina Mdude na wenzake ni wahalifu na wanastahili kuadhibiwa nje ya sheria. Hatuwezi kukemea watu fulani wanapochukua sheria mkononi na kuwatesa watuhumiwa wakati sisi pia tunafanya hivyo hivyo kwenye jamii zetu.

Tunaona kibanzi kwa wale lakini hatuoni boriti machoni mwetu
 
Mastakiraka una hoja dhaifu sana.Sheria za nchi zinasemaje?

Hivi kila mtu aamue kujichukulia sheria mkononi itakuwaje?

Muhimili wa mahakama una kazi gani?
Weak state inapelekea watu kujiamulia wenyewe maana serikali yao imefeli. Serikali imeshindwa kutulinda ikiwemo kutatua tatizo la vibaka ...sasa wananchi wameamua kudeal na hao wasumbufu mmoja mmoja. Kama ulivyoshauriwa waonye hao vijana mtaani kwako maana watamalizwa. Na hiyo mitaa yenu si ndo yenye panya road?? Wataisha
 
samweli sungusungu wa mtaa wa mburahati na mfahamu vizuri maana mburahati kumezidi sana.
na huyu dogo ni hatari na mtoto wa mzee jongo

kuna mwenzake anaitwa elly kishoronga
Kumbe ni kibaka mzoefu na amepata halali yake sasa huyu mama anamsumbua nini rais wakati Ana mambo ya msingi ya kufanya.
 
Back
Top Bottom