Kijana kamkimbia mchumba wake alietaka kumuoa baada ya kujua kwao kuna walemavu ni sawa?

Nimemshangaa huyo jamaa, je yeye akipata ulemavu hapo alipo afu wanawake wamkatae kimahusiano na kuzaa nae atajisikiaje?

Elimu yake haijamsaidia hata kidogo.
Si ndyo hapo nmesema jamaa Ana utoto sana
 
Dooh tena huyo ana bahati kama ilifika hadi akajifungua salama. Nyingi zikifikisha miezi mitano zinapasua eneo lililotungwa mimba anavuja damu ndani kwa ndani na wengine wanapoteza mimba na maisha kabisa.

Na zilizotunga kwenye mirija ile ikichelewa kutolewa anapata matatizo ya uzazi mbeleni maana ovary ataksyokuwa anaitegemea ni moja tu

Sio vyema kubishana na wataalamu wa afya kabisa
 
Hakuwa sahihi! Labda angefanya utafiti zaidi chanzo cha matatizo hayo ni nini?
Ulemavu siyo tatizo la kurithi!
 
Anaweza amka kesho akawa kipofu au akaoata ulemavu wowote.

Hujafa hujaumbika acheni dharau karma sometimes Ina back fire vibaya sana.
Ni kweli kabisa....Hujafa hujaumbika...

Mimi jana tu..kuna sehemu nilikuwa natoka...hakuna usafiri wowote unapita..hata boda hakuna...

Ikatokea Bajaji nikaisimamisha...kupanda Kuna mdada mzuri tu amekaa katikati na Mmama..ni mtu na Mama yake.

Kumbe yule Dada amepata Ugonjwa wa Akili...Mama yake ametoka kumchukua Zanzibar huko..Na Bajaj walikuwa wamekodi... walinibeba tu ili kunisaidia...

Yule Dada alikuwa anapiga kelele Bajaj nzima,mara anilalie, apige makofi, aimbe, anafika mahali anataka kama kuruka...Nikataka kumwambia Dereva anishushe tu...

Ghafla nikaingia Imani nikajiuliza angekuwa ndugu yangu ningevumila..Acha na hapa nivumilie..Ikabidi niwe namsaidia Mama yake kumshika akitaka kuruka..

Hii Dunia inatupasa kukaa kwa utulivu na adabu kubwa sana....Unaweza kujiona mkamilifu sababu halijakupata..ila likikupata ndiyo utajua kupatana nalo.
 
Daah na kweli kama ndio hivyo huyu kanusurika
Kabisa sio vyema maana athari zake huko mbeleni ni kubwa sana
 
Umenikumbusha baba yangu alikua anasisitiza ukipata mchumba umwambie mapema achunguze ukoo wake maana kuna magonjwa ya kurithi, tabia za kuhama vizazi, laana za ukoo na mambo muhimu kuchunguza kabla ya ndoa.
Dada yangu alikuwa anatuambia "Angalieni sana huko mnapotaka kuolewa."
 
JF Imekuwaje siku hizi ? Jarida la mipasho utoto ujinfa tuu mambo personal ....sio ile mijadala ta kukuza nchi na vision 2030 to 50 yaanii nadhani JF ya $$ subscription ni muhimu na lazimaa....
Hata hiki unachokifanya hapa ni mipasho tosha.
 
JF Imekuwaje siku hizi ? Jarida la mipasho utoto ujinfa tuu mambo personal ....sio ile mijadala ta kukuza nchi na vision 2030 to 50 yaanii nadhani JF ya $$ subscription ni muhimu na lazimaa....
thread Za Kukuza Nchi Zipo We Ignore Zisizokuhusu
 
Na huko ndo ukweli. Wakati huo mke alikuwa ni wa familia na hivyo ililazimika kufanya uchunguzi ili kuepuka yale ambayo waliona yanaweza kutokea huko mbele na kuleta kutokuelewana Kati ya familia hizi mbili.
 
Pole sana kaka ,kitu cha kumuomba mungu ni kutuepushia magonjwa familia zetu kuna siku nimetoka dar ile nafika tu home mbeya usiku wa manane dogo kazidiwa anashindwa hata kupumua aisee siku ile ndo nilichanganyikiwa ndo nilipoujua umuhimu wa gari maana dereva teski wote hawapokei siku wa tatu ndo akapokea tukamkimbiza dogo chapu had Leo naishi kwa code simu salio iwe nayo pesa ya akiba namba za watu wa usafiri zisizopungua tano ,dawa za kawaida za kutuliza maumivu kama panadol lazima ziwepo ndani sisi wenye familia lolote linaweza jiri mda wowote ni kukaa attention
 
Hii ilikuwa kazi ya Wazee zamani wanachunguza koo mbali mbali na ukitaka kuo unaambiwa kabisa pale usiende hapa nenda siku hizi tunajichukulia maamuzi wenyewe yanatukuta ya kutukuta. Jamaa yuko sahihi kabisa.....very right
Hakuna kitu kizuri kama kuoa kabila lako mana utachunguza na kupata jibu kupitia kwa wazazi....kuna familia zinarithi vitu ukioa mpka hujajua,saa ingine unakuta unazaa watoto wenye magonjwa ya kurithi
 
Maamuzi sahihi,ila alichokosea ni kumwambia...angempiga tu matukio ya hapa na pale Kila Mtu a depart na mwelekeo wake.
Mimi kuna ukoo naujua uliachiwa laana huko enzi za mababu zao miaka 1910,babu huyo alimdhulumu mjane ....babu alizaa watoto wakiume watatu na wao wakaja kuoa,ila kila tumbo wakiume mmoja chanel kichwani zilipotea wakiwa wamemaliza udsm na wanafanya kazi kabisa,laana zipo
 
Yes Kuna mambo kama yanaepukika mapema ni sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…