Kijana kamkimbia mchumba wake alietaka kumuoa baada ya kujua kwao kuna walemavu ni sawa?

Ndugu yangu hiyo laana ya mwaka 1910 uliiona wakati inatolewa [emoji3][emoji3]

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Kuna jamaa aliwahi kuwa na mahusiano na mdada mpaka wakawa wanaishi kama mume na mke bila ndoa. Bahati nzuri binti alikuwa anajulikana hadi kwa ndugu wa jamaa. Binti akapata ujauzito akajifungua mtoto albino. Jamaa alishindwa kuruka kwani mtoto sura ilikuwa ni yake kabisa. Ila ilibidi abreak up na yule dada kwa kudai kuwa kwao hawana mtu wa aina hiyo.
Basi kuna siku akamtembelea babu yake mzaa baba kijijini kwa sababu babu yake alikuwa anajua kuwa jamaa ana mke akamuuliza habari za mkewe. Jamaa akamwabia babu yake kuwa ameachana na mkewe kwa sababu amebaini kuwa amemletea kiumbe kisicho cha kawaida kwenye ukoo wao. Babu akauliza ni nini hicho? Jamaa akafungua kuwa binti amemzalia albino jambo ambalo kwenye ukoo wa halijawahi kutokea.
Babu yake kusikia hivyo alisikitika sana, akamwambia huyo mtoto uliyemkataa ni babu yangu. Babu akamweleza kuwa babu yake mzee baba alikuwa albino. Na alieleza kuwa katika familia ya babu yake walikuwa watoto watano watoto wawili akiwemo babu wa babu yake walikuwa albino.
Aliendelea kueleza kuwa babu yake huyo alioa na kuzaa watoto sita akiwemo baba wa babu yake na watoto wote walikuwa kawaida.
Babu alimwambia hiyo ni asili yao kabisa.
 
Basi sawa ikawaje sasa ndugu yangu nafuatilia kwa ukaribu kabisa

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Yeye akipata ulemavu hapo ukubwani alipo atalelewa na nani?
Suala la kupata ulemavu lipo muda wowote, Lakini kujua sehemu fulani kuna ulemavu na wewe unakwenda kujitafutia matatizo yasiyo ya lazima ni ukosefu wa akili.

Kulelewa atalelewa na yeyote tu.
 
Kwanza Afrika umtembelee mama mjamzito halafu uanze story za kumwambia mzazi kwamba mtoto ana atakuwa na shida fulani.

Watakwambia wewe ndio mchawi mwenyewe...😂
 
Angetoka kimya kimya tuu bila kuongelea ulemavu, kuna karma dunia hii na umeumbwa hujaumbika, yeyote anaweza kuwa mlemavu any minute
 
Mbona huu mjadala ni very sentive...kupitia hapa watu watajifunza ni magonjwa yapi yanarithiwa kabla hawajajiingiza wazima wazima..
Huyo nae kavurugwa..
watu kama hawa lazima wawepo ili jukwaa lisikae kizembe
 
"tatizo haliponi kwa uwezo wao"

Naelewa uchungu unaoupata kwa kauli hiyo hasa inapotoka kwa madaktari, maana binafsi ni mlemavu wa viungo

Na kwa mujibu wa madaktari sikupaswa kuishi hadi leo hii. Walinitabiria kwamba sintofika 2005

Lakini baada ya kuingia kwenye utu uzima na kulijua neno la Mungu na kulikiri hasa ule mstari usemao "lisilowezekana kwa binadamu kwa Mungu linawezekana"

Mstari ulinitia nguvu sana huo nikawa nakiri uzima kwamba"sintakufa bali nitaishi nami nitayasimulia matendo makuu ya Mungu "



Pole na usife moyo iko siku Mungu atakurejeshea furaha yako juu ya mwanao
 
Huu uzi tuwapelekee wahindi na waarabu wao watakua na majibu mazuri
 
Basi sawa ikawaje sasa ndugu yangu nafuatilia kwa ukaribu kabisa

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Jamaa ilibidi amrudie yule dada waliyezaa naye, wafunga ndoa maisha yakaendelea. Walifanikiwa kupata watoto watatu mmojawapo ndiyo huyo albino mwingine alikuwa na character za kialbino kwenye macho na ngozi kwa mbali lakini hakuwa albino. Mtoto wa tatu alikuwa kawaida kabisa.
 
Kumuacha ni sawa kabisa, probably style ya kumuacha mtu wa namna hiyo ndio inatakiwa iwe strategic.

Hata zamani wazee hawakuoa familia zenye magonjwa ya kurithi kama kifafa, familia zenye mikosi(mlango wa saba), familia ambazo wanawake hawakudumu kwenye ndoa. Walifanya sana hivyo, sio ajabu wala.
 
Mkuu ww unaonekana unaelewa sana haya mambo ya magonjwa ya kurithi..Nami naomba niulize hapa. Hivi ukoma(leprosy) nao pia huwa ni ugonjwa wa kurithi, genetically?
Isivyo bahati siufahamu kivile huo ugonjwa ila nachofahamu sio wa kurithi, kama kuna mengineyo wataalamu watakuja kujazia nyama
 
Ubarikiwe dada. [emoji120][emoji120]
 

Jitahidi jumpa juice zinazodetoxify

Na poleni sana kwa kuuguza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…