mtechnical
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 238
- 570
Mi nawalaumu KATAA NDOA, kwa kampeni yao hiyo.No offense broh, kiuhalisia unaweza Kuta wewe ndio ndio kuna uwalakini kwenye uanaume wako. Why nasema hivyo?
Ndoa ni utaratibu ambao binadamu wameweka ili kuinteract, kuzaliana nk. Kuoa/kuolewa ni jambo muhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu, lakini sio jambo la lazima. Hivyo mtu ana hiari ya ama kuingia kwenye ndoa au la. Sasa inapotokea mtu akaamua kutumia uhiari wake kuamua, alafu wewe unasema ana walakini kwenye uanaume wake, jua ni wewe ndio una huo uwalakini.
Siwasupport wenye kampeni ya kataa ndoa, ila siwalaumu maana ni hiari yao. Huwezi jua walikumbwa na nini.
Tofautisha ndoa na mahusiano ya kimapenzi. Mtu anaweza kujihusisha na mapenzi bila kuwa kwenye ndoa.
Kama wao wameumizwa na ndoa wakae kwa kutulia wasituharibie kizazi.
Hebu fikilia kizazi cha watoto wanazaliwa nje ya ndoa na kukosa malezi ya baba na mama ( familia).
Tutajikuta tunajenga kizazi cha hovyo sana tukiendekeza hawa kataa mdoa.