Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Zaidi sana utapoteza muda na fedha zako, tena kwa fedheha sana, ukiwa na elimu ya madigrii kadhaa ya kitaaluma wakati mganga hata darasa la saba hajamaliza.
Mganga hawezi na wala hana uwezo wa kukupatia uongozi wa wananchi, bali atakutisha tu kwa kukuhimiza kufanya bidii kutafuta kura kwa wananchi kwa masharti magumu, huku akiwa anakukoromea kwa ukali na vitisho, bidii ambayo ungeweka tu mwenyewe na ukafanikiwa.
Uvivu wako katika kutafuta uongozi wa kisiasa na tamaa zako za kupata uongozi bila kuweka bidii ya ushawishi wa sera na mipango mikakati yako kwa wananchi, visikuchochee ukatumbukia kwenye dhambi hii ya ushirikina na uchawi na pengine kupelekea hadi kusababisha vifo na mauaji kwa binadamu wenzako.
Kwa njia hiyo, huwezi kudumu, huwezi kuwa na amani, wala kufurahia uongozi wako ikiwa kuna roho na damu za wasio na hatia ulizodhulumu zinakulilia kwa uchungu kila uendako.
Uongozi na mamlaka za wanadamu vinatoka kwa Mungu, sauti ya wengi sauti ya Mungu, ukimtumainia na kutegemea Mungu katika nia na dhamira zako njema atatufanikisha.
Uganga, uchawi na ushirikina unakupoteza mchana kweupeee na elimu yako.
Pambana kwa bidii na haki utatoboa tu.
Dominika Njema.