Pre GE2025 Kijana, Ushirikina na Uchawi hautakusaidia kupata nafasi ya Uongozi wa Kisiasa

Pre GE2025 Kijana, Ushirikina na Uchawi hautakusaidia kupata nafasi ya Uongozi wa Kisiasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
My son you can't void witchcraft, katika hii dunia yenye mambo mengi, visible and invisible!
Those great men, posses a great power!
I can confirm to you gentleman without fear of contradictions kwamba, through God you can be a very influential and powerful political leader as I am, in my constituent and in certain decision making institutions:pedroP:
 
Lazima uwe na kioo cha kuwachunguza watu wanaokupinga. Unakaa ofisi binafsi unaangalia mmoja mmoja, wanavyokutana na kupanga vikao. Siku nyingine unawafata pale pale walipokaa
kioo cha kuwazoom sio:pedroP:
 
zaidi sana utapoteza muda na fedha zako, tena kwa fedheha sana, ukiwa na elimu ya madigrii kadhaa ya kitaaluma wakati mganga hata darasa la saba hajamaliza...

mganga hawezi na wala hana uwezo wa kukupatia uongozi wa wananchi, bali atakutisha tu kwa kukuhimiza kufanya bidii kutafuta kura kwa wananchi kwa masharti magumu, huku akiwa anakukoromea kwa ukali na vitisho, bidii ambayo ungeweka tu mwenyewe na ukafanikiwa...

uvivu wako katika kutafuta uongozi wa kisiasa na tamaa zako za kupata uongozi bila kuweka bidii ya ushawishi wa sera na mipango mikakati yako kwa wananchi, visikuchochee ukatumbukia kwenye dhambi hii ya ushirikina na uchawi na pengine kupelekea hadi kusababisha vifo na mauaji kwa binadamu wenzako....

kwa njia hiyo,
huwezi kudumu, huwezi kua na amani, wala kufurahia uongozi wako ikiwa kuna roho na damu za wasio na hatia ulizodhulumu zinakulilia kwa uchungu kila uendako...

uongozi na mamlaka za wanadamu vinatoka kwa Mungu..
sauti ya wengi sauti ya Mungu..
ukimtumainia na kutegemea Mungu katika nia na dhamira zako njema atatufanikisha...

uganga, uchawi na ushirikina unakupoteza mchana kweupeee na elimu yako..

pambana kwa bidii na haki utatoboa tu 🐒

Dominika Njema..
Hii aisome Hamisi Kigwangwala aka mzee wa makafara itamsaidia sana.
 
Mheshimiwa kwamba hauna mganga anaekusetia dish lako kwa wapiga kura huku??? Acha basi kututania......
let me make it clear,
ni kwavile tu sikumalizia story yangu yahttps://www.jamiiforums.com/threads/kwa-mara-ya-kwanza-nathubutu-kugombea-ubunge.2205618/

kuna sehemu kulikua na masuala yaho ya kishirikina na uchawi, lakini haikua ngumu kwangu kuyakabili na kuyateketeza kwasababu na kuvuka jaribu hilo,

Mungu alie hai alikua ndani yangu, na kila nilipopata ugumu au wepesi wa safari yangu kutafuta uongozi wa kisiasa, nilimshirikisha, niliambatana, na kuandamana nae kimwili na kiroho anifanyie wepesi na urahisi wa kupita, na hatimae niliikamilisha safari yangu iliyojaa uzito na majaribu mengi na ya kipekee sana, na kwakweli, kwa Neema na Baraka za Mungu nikamaliza salama:pulpTRAVOLTA:
 
Haya mambo ni magumu sana
 

Attachments

  • IMG-20240707-WA0004.jpg
    IMG-20240707-WA0004.jpg
    49.8 KB · Views: 3
Unadhani kina Jenister wapo mjengoni toka wakiwa mabinti hadi uzee unawakuta ni kwa nguvu zao au maombi? Ushirikina na kutoa papa.
binafsi sidhani kabisa katika ushirikina na uchawi katika siasa :pulpTRAVOLTA:
 
Ukiwa mwana ccm na hujawahi kwenda kwa mganga au wewe siyo mchawi basi utaishia kudeki vyoo, kuvishwa kofia na kulishwa ubwabwa kama zombie na kete kubwa ya ccm ipo kwenye nguvu ya dola na ulozi na ndo maana mwenge huzunguka nchi nzima kumwagia watz uvumba kwa kisingizio cha kukagua miradi lakini huo mwenge hauna macho, hauongei, hauandiki, hauna amri! Vyoote vinafanywa na binadamu sasa kwanini huyo binadamu asiende kuangalia huo mradi? Sasa kama umetumwa na vigogo wa ccm ili kupumbaza vijana basi umepotea.
huo ni upotoshaji gentleman:pulpTRAVOLTA:

nimewashauri kwa dhati kabisa vijana wenzangu wenye nia, dhamira na ndoto za kua viongozi wa kisiasa nchini, kwamba ili kuongoza wananchi kwa uhakika, furaha na amani, hakikisha unatafuta na unapata uongozi kwa nguvu, bidii, haki na maarifa yako halali, aliyo kujaalia Mungu, na sio kwa mambo yaliyo kinyume na Neema na Baraka za Mungu:pulpTRAVOLTA:
 
Huyo bado mchanga kwenye siasa!

Ngoja akutane na simbachawene ampe somo yeye kadumu kwenye game kwa nguvu ipi!

Mungu anaweza kukupa nafasi lakini kanuni za kupanda juuau ku maintain ndio tatizo!

Utakuta Hadi mwamposa anaaguliwa!
mbona uliemtaja mrahisi sana,

miongini mwa nielie kua nikipambana nae,

alikua na shanga nyeupe mkononi na shingoni, hizi alijitahidi kuzificha zosionekane lakini akijisahau unaziona tu live,

lakini pia nilidokezwa kwamna na kwenye korodani na kwenye mshedede pia, alikua amepavisha shanga nyeupe kulingana na mwembwe za mnganga alie mrubuni:pedroP:

lakini mwisho wa siku akapigwa chini mapema kabisa kwenye nchujo wa chama, sasa sijui kama tayari alikua amesha ua mtu asie na hatia kanbla maskini ya Mungu dah?
 
Unaonekana hujui vitu vingi sana kuhusu hii dunia, usichanganye elimu yako ya kukaririshwa hiyo na elimu ya asili
basi hiyo ya asili ni mbaya sana yaani unadanganywa na mganga kuua binadamu mwenzako asie na hatia, ili ushinde uchaguzi na upate uongozo kweli?:pulpTRAVOLTA:

vipi uki uawa wewe sasa kwaajili hiyo au mwanao?:pedroP:
 
Neno uganga na ushirikina vilikuja baada ya dini za oppressers kuingia,ila ndio njia za asili za kiimani za waafrika,acha tufuate asili yetu usilam na ukristo ni dini za kuletewa na watesi wetu hazina jema kwetu.
kutafuta uongozi kwa kuua binadamu wengine ni njia ya uasili ya kiimani ya kinyama sana sana Africa...

kuna haja ya kuitukuza kweli?:pulpTRAVOLTA:
 
kioo cha kuwazoom sio:pedroP:
Naam, lazima haya mambo uyajue, kuna kulishwa uchawi kwenye chakula, lazima fundi akuwekee mambo kama chakula kina sumu au uchawi sahani ipasuke. Safari nyingine kabla ya kusafiri unapata early warning system za yajayo. Zile zinazomfanya Lissu acheke cheke akikutana na Malkia wa Sheba (mama kizimkazi), baadae akitoka anaenda kutukania ikungi.

Au vidono, ile ya kuzuia risasi isikuue, hata Lissu ilimsaidia pale Dodoma
 
Uchaguzi huu,,tunaenda kusaka wataalam kutoka sauzi,, wa nigeria mambo yanakua magumu,,hadi kieleweke 2025 lazima tuzame mjengoni dodoma
 
Naam, lazima haya mambo uyajue, kuna kulishwa uchawi kwenye chakula, lazima fundi akuwekee mambo kama chakula kina sumu au uchawi sahani ipasuke. Safari nyingine kabla ya kusafiri unapata early warning system za yajayo. Zile zinazomfanya Lissu acheke cheke akikutana na Malkia wa Sheba (mama kizimkazi), baadae akitoka anaenda kutukania ikungi.

Au vidono, ile ya kuzuia risasi isikuue, hata Lissu ilimsaidia pale Dodoma
Hahhaha eti anachekacheka akikutana na bimkubwa,,matusi hadi ikungi,, halafu watu wanazichukuliaga poa sana zile chai za ikulu, ila zimewatuliza wengi😀😀😀
 
Kuwa mwanasiasa nguli na kupanda vyeo vikubwa lazina uwe na malaika wenye nguvu sana pembeni yako au uwe na nguvu kubwa sana ya kwako mwenyewe ya ndani.

AU

Uwe na mauchawi yenye nguvu sana.

VINGINEVYO utaishia kuvaa magauni ya kijani tu huku wenzio wakitafuna manyama.
 
Kuwa mwanasiasa nguli na kupanda vyeo vikubwa lazina uwe na malaika wenye nguvu sana pembeni yako au uwe na nguvu kubwa sana ya kwako mwenyewe ya ndani.

AU

Uwe na mauchawi yenye nguvu sana.

VINGINEVYO utaishia kuvaa magauni ya kijani tu huku wenzio wakitafuna manyama.
Si hata watoa mtandao nao wanapanda
 
Back
Top Bottom