Pre GE2025 Kijana, Ushirikina na Uchawi hautakusaidia kupata nafasi ya Uongozi wa Kisiasa

Pre GE2025 Kijana, Ushirikina na Uchawi hautakusaidia kupata nafasi ya Uongozi wa Kisiasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Zaidi sana utapoteza muda na fedha zako, tena kwa fedheha sana, ukiwa na elimu ya madigrii kadhaa ya kitaaluma wakati mganga hata darasa la saba hajamaliza.

Mganga hawezi na wala hana uwezo wa kukupatia uongozi wa wananchi, bali atakutisha tu kwa kukuhimiza kufanya bidii kutafuta kura kwa wananchi kwa masharti magumu, huku akiwa anakukoromea kwa ukali na vitisho, bidii ambayo ungeweka tu mwenyewe na ukafanikiwa.

Uvivu wako katika kutafuta uongozi wa kisiasa na tamaa zako za kupata uongozi bila kuweka bidii ya ushawishi wa sera na mipango mikakati yako kwa wananchi, visikuchochee ukatumbukia kwenye dhambi hii ya ushirikina na uchawi na pengine kupelekea hadi kusababisha vifo na mauaji kwa binadamu wenzako.

Kwa njia hiyo, huwezi kudumu, huwezi kuwa na amani, wala kufurahia uongozi wako ikiwa kuna roho na damu za wasio na hatia ulizodhulumu zinakulilia kwa uchungu kila uendako.

Uongozi na mamlaka za wanadamu vinatoka kwa Mungu, sauti ya wengi sauti ya Mungu, ukimtumainia na kutegemea Mungu katika nia na dhamira zako njema atatufanikisha.

Uganga, uchawi na ushirikina unakupoteza mchana kweupeee na elimu yako.

Pambana kwa bidii na haki utatoboa tu.

Dominika Njema.
ccm inawenyewe na uchawi nisawa na samaki na maji,labda wewe ni mshika filimbi tu hujui lolote
 
ccm inawenyewe na uchawi nisawa na samaki na maji,labda wewe ni mshika filimbi tu hujui lolote
mimi nmeshauri wanasiasa vijana wenzangu jambo ambalo sijaona umihimu wake kwa wengi...

Mimi nina mshukuru Mungu, nimevuka salama kumtegemea yeye pekee,
na sasa bafanya siasa za jimboni, kitaifa na kimataifa kwa uhakika kwasababu Mungu yupo pamoja nami ndani yangu daima :pedroP:
 
Ukiwa mwana ccm na hujawahi kwenda kwa mganga au wewe siyo mchawi basi utaishia kudeki vyoo, kuvishwa kofia na kulishwa ubwabwa kama zombie na kete kubwa ya ccm ipo kwenye nguvu ya dola na ulozi na ndo maana mwenge huzunguka nchi nzima kumwagia watz uvumba kwa kisingizio cha kukagua miradi lakini huo mwenge hauna macho, hauongei, hauandiki, hauna amri! Vyoote vinafanywa na binadamu sasa kwanini huyo binadamu asiende kuangalia huo mradi? Sasa kama umetumwa na vigogo wa ccm ili kupumbaza vijana basi umepotea.
Duh yawezekana ametumwa mana wameona watu wameamka japo sio wengi bado kazi kubwa inaitajika kuwatoa watu kwenye kupumbazwa ili watawaliwe kindezi, mfano mzuri ni nyomi la kwa mwamposa, wale wote ni mapunguani wanaitaji kuzibuliwa akili waamke kwenye usingiz mzito wa kupumbazwa..
 
mbona uliemtaja mrahisi sana,

miongini mwa nielie kua nikipambana nae,

alikua na shanga nyeupe mkononi na shingoni, hizi alijitahidi kuzificha zosionekane lakini akijisahau unaziona tu live,

lakini pia nilidokezwa kwamna na kwenye korodani na kwenye mshedede pia, alikua amepavisha shanga nyeupe kulingana na mwembwe za mnganga alie mrubuni:pedroP:

lakini mwisho wa siku akapigwa chini mapema kabisa kwenye nchujo wa chama, sasa sijui kama tayari alikua amesha ua mtu asie na hatia kanbla maskini ya Mungu dah?
Changa la.macho ..stori za vijiweni hizi ..
 
Ooh kwahio ukitaka kumchomoa pale jimboni inabidi na wewe uwe mtu wa kazi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kiboko yake Joseph Muhagama, walitifuana alipoona anashindwa, ndo akaamua wagawane jimbo, na kuzaliwa Jimbo la Madaba ambalo mbunge ni Jose.

Yule kila mda wa uchaguzi, hataki mtu atokee kumchallenge, anamzimisha kivyovyote. Na safari hii tumesikia mke wa Majaliwa anakuja kugombea kulee, za chini chini zinasema anataka wagawane jimbo, kuwe na Peramiho kusini na Peramiho kaskazini.

Sasa tunasubiri kuona.
 
Naam, lazima haya mambo uyajue, kuna kulishwa uchawi kwenye chakula, lazima fundi akuwekee mambo kama chakula kina sumu au uchawi sahani ipasuke. Safari nyingine kabla ya kusafiri unapata early warning system za yajayo. Zile zinazomfanya Lissu acheke cheke akikutana na Malkia wa Sheba (mama kizimkazi), baadae akitoka anaenda kutukania ikungi.

Au vidono, ile ya kuzuia risasi isikuue, hata Lissu ilimsaidia pale Dodoma
aise kumbe mambo mazito namna hiyo?

hiyo ya chakula nilishuhudia kwa rafiki yangu wakati tukisoma seminary, yeye alikua akilelewa na mama wa kambo.
siku hiyo tukuwa tunaoshi parokiani , tukaenda kuitembelea familia yake, hatukumkuta babake mzazi nyumbani, ispokua tulimkuta mama yake wa kambo...

akatuandalia chai,
kumbuka shuleni na parokiani tulikatazwa na kusisitizwa sana kujizuia kula mtaani, lakini kwakua ilikua nyumbani hatukua na hofu wala nguvu ya kukataa kula,tulikua na amani kabisa...

basi tukakaribishwa mezani na kila moja wetu akapewa kikombe chake kilichojaa chai na vitafunwa pembeni...

nilishangaa rafiki yangu kikombe aliponyanyua chake na kutaka kunywa chai ile, kabla hajakifikisha kinywani mwake, alikua aketetemeka mikono na asiweze kukufujisha kunywani mwake,

alijarinu mara mbili,
mara ya tatu kikamponyoka na chai ikamwagika na kile kikombe kikapasuka na kusambaratika kama vile kimerushwa kutoka angani......

mama alikua akitetemeka mno pia,
alimpatia kikombe kingine na hali haikua tofati na ya mwanzo, na sasa chai ilimchafua nguo zake na tukalazimika kuondoka kurjea parokiani....

tulipokua tukieleza mazingira haya kwa wakongwe walitueleza kwamba hapo kuna mazingira ya kishirikina lakini pia kuna nguvu za Mungu :pulpTRAVOLTA:
 
Ana uheshimiwa gani huyo kapuku..! Hana hela. Na hajui hela inatafutwaje.
mie sitafuti hela, wala sitaki jela kwa mgongo wa wananchi wanyonge ninao watumikia kwa bidii sana, kwa uaminifu saa bila kuchoka, kunung"unika hali ngumu, wala kukata tamaa hata kidogo...

mihimu hawa wananchi wanapata maendeleo wanayoyataka kwanza na wanafurahi, ndipo nami nione kama kuna kakitu kidogo, nami nione kama kananifaa na familia yangu...

hata hivyo,
nafurahi mang"ombe yana afya ni nzuri sana, chakula na maji yapo ya kutosha, na huko shambani mavuno yanatia moyo sana, si kwangu tu pekeyangu bali wakulima wote nchini...

kongole nyingi sana kwa mh.Rais Dr.Samia Suluhu Hassan, kupitia huyu waziri kijana makini na mchapakazi sana wa Kilimo Hussein Bashe, kamaa ameleta mageuzi ya kilimo kwakweli.

mwaka huu tumevuna aise dah :KasugaYeah::KasugaYeah:

Asant Mungu kubariki kazi za mikono yetu, asanti kuonekana mashambani kwa wakulima nchini...
 
Changa la.macho ..stori za vijiweni hizi ..
yes,

ndio mimi siwezi kubabaika na ushirikina wala uchawi,
Neema na Baraka za Mungu zimeambatana na kuandamana tangu hatua ya kwanza kuingia kwenye siasa,

kwahivyo nimejiskia kuwashauri bure, vijana wenzangu wenye dhamira za kuingia kwenye siasa kumuamini na kumtegemea Mungu zaidi ya ushirikina na uchawi:pulpTRAVOLTA:

ukiona unafaa sawa, ukiona haufai na shauri yako pia...
 
Uchaguzi uliopita nilitia Nia na kuchukua fomu ya Ubunge.. Siku mbili kabla ya kikao cha uteuzi aliyeibuka mshindi alikusanya zaidi ya nusu ya wajumbe... Akawaambia kila mjumbe atapewa laki tatu.. Hizo laki tatu zilitolewa na mganga wa kienyeji kwa sharti kuwa kama hutampigia kura Bora laki tatu yake uiache.. Na kweli jamaa walimpigia kura na akashinda.. Ushirikina Bado una nguvu sana katika siasa zetu..
Yaani akawachota kirahisi hivyo? Aiseee
 
Back
Top Bottom