Kijana wa Kiume kufanyiwa Graduation kubwa hadi kukodisha ukumbi

Kijana wa Kiume kufanyiwa Graduation kubwa hadi kukodisha ukumbi

Unafanya Graduation kubwa halafu unaishia kuwa mbeba zege kitaa.

Inaleta huzuni Sana labda awe wa mboga Saba na connection za uhakika
Pale kidimbwi, watu wanaagiza chupa ya moja ya pombe kwa gharama ya 1.5m (Milion moja na laki tano).
Kama hauna hela utabaki unalalamika sana.
Tafuta hela mkuu, uache makasiriko.
Mzungu anatoka Uingereza kuja Tanzania kuangalia Tigwa
 
Afadhali hiyo amesita kutafuta GPA , saa ingine nako analazimishwa na waandaaji


Swala ni hivi mwanaume unaandaa sherehe kusherehekea birthday na mc juu vyakula vimepikwa kwa uzuri . nyie aaah hapana kwakweli , kwa wanawake sishangai kwao kawaida tuna kautofauti ,
 
Mh
Wabeba zege ni nyie msiofanya Graduation kubwa, kwa sababu uwezo hamna.... Sasa kama kaweza kufanya Graduation kubwa, anashindwa vipi kupata pesa ya Kufungua biashara ya maana.... Mwenye pesa ni mwenye pesa tu, acha kujifariji na maneno ya kimaskini,
Mhaya katika ubora wake😂😂
 
Angalau uliomuonyesha Unamjali ila, dhiki zimeandama nawe, ndiyo maana hujafanya pakubwa.
Nilikua na dhiki ya muda tu mkuu.
Nilikua tight na kazi,
Kiasi mambo ya kuandaa party muda haukuwepo.
Ingawa nilienda kugraduate na kijana boss alimind.
Kanipa 2 hrs.
Namimi niliporudi wala sikutaka maswali nilichukua vyangu nikatimka.
Kusema ukweli siku hiyo niliumia sana kutopata ule muda zaidi kumpongeza kijana wangu.
Ningepata hata Disco tungeongozana.
Ila that lunch time together na company kiasi ilitosha sana na zawadi alipata za kiwango tu.
Na niliacha kazi siku hiyo hiyo.
Jamaa kafurahi nimerudi anasema aah unameremeta imeenda sawa.
Mi namwambia ndio ila kazi na wewe mwisho hapa.nimefata mikoba yangu tu.
Kabaki anatoa macho
 
Degree kwa kijana ni Jambo kubwa na Hakuna utajiri unaozidi MAARIFA ukiwa na maarifa utaushinda umasikini
Utaushinda ujinga
Chuki wivu na visasi

Binafsi Mtu anayefanikiwa Kupata degree anabidi kufanyiwa sherehe kubwa Sana endapo PESA ipo hata kama Haipo unaweza kukopa ilimradi Utimize lengo


Vita ya kuushinda ujinga na kuwa na MAARIFA sio Vita ya kubezwa hata kidogo

Binafsi nimekaa mtaani Ila mtaani bila Elimu ya chuo kikuu kwa kijana Mdogo bado unapoteza sight na insight


MAARIFA ni utajiri mkubwa acha kijana ale Bata na afurahie matunda ya jasho lake .

✌️✌️✌️✌️ Victory belong to no one ila Mungu tu.
 
Halafu unakuta dude lenyewe ni likilaza la ma sapu , c zakumwaga siku likitoboa kimazabe ndio utashangaa limekusamya ukoo mzima halafu linarudi nyumbani pamoja na mbwembwe zote ajira chwee linakuwa lipo nyumbani tuu kuendesha magari ya mshua
Si ndio wanaokuongezea nchi yako hao, akitoka hapo ni kazi ya matawi ya juu bila usaili...
kubali yaishe...
 
,🤣🤣afu graduation ya kilaza mwenye gpa ya 2.0 🤣🤣pulizz debe tupu haliachi kutika
Ila msamehe kwenye ukoo wao wote yeye ndo kasoma Jordan University 🤣🤣🤣

We unaishi gizani unadharau chuo Cha Jordan wakati Elimu ya chuo kikuu ni universal wanachosoma udsm ndo hicho wanasoma hapo Jordan

Tukija katika GPA Kuanzia 2 maana yake Kafaulu

Then kufanikiwa Maisha Kuna hitaji mambo Mengi ikiwemo
Connection
Self-esteem
Discipline
Hard working
Passion plus goals
Saving plus networks with peoples .

So kwa hii Dunia tuliopo sio ile ya kumcheka Mtu au kumchukia Mtu kisa kafanya Jambo fulani hizo tabia wanazo Masikini wa fikra ambao most of them wapo employed with mirgle salaries .


Kudharu au kubeza MAFANIKIO ya Mtu ni dalili Mojawapo Kuwa wewe ni mtu Masikini wa fikra ,uchumi, na Afya ya akili You need to reprogram ur Subconscious mind ili kuwa Binadamu kamili.

Binafsi nampongeza huyo kijana hata Kama kapata GPA ndogo Naamini atafanikiwa maana Hakuna kilaza hapa Duniani kila mtu ana Akili.
 
Back
Top Bottom