Kikawaida wanaohonga Wanawake ni wanaume dhaifu na Maskini

Kwa Zama hizi kila mtu ajitunze mwenyewe.
Tukianza kuishi au kumuoa nitahudumia.

Ninyi wazee wa zamani Kanuni zenu kwa sasa nyingi ni irrelevant
Huenda uaminifu miongoni mwenu Vijana umekuwa changamoto.

Sisi zamani ilikuwa unaweza hata kumpeleka mchumba wako Shule ukamlipia ada hadi anamaliza Masomo.

Akimaliza ndiyo mnafunga Ndoa na kuanza kuishi pamoja

Nyie Vijana najua hamuwezi kufanya hayo
 
Katika hiyo hiari ndiyo kuhudumia kwenyewe hapo

Hata kama utakuwa unamjazia mtungi gesi, ndiyo kuhudumia kwenyewe huko

Hiyo kuchapiwa ni jambo mtambuka

Hata kama umuhudumue milioni 100 Kwa Mwezi akiamua kucheat anacheat tu

Pia unaweza kutokumtunza ndiyo ikawa sababu ya kukucheat Kila Siku maana atakuwa anapewa hizo huduma ambazo humpi.

Hoja yangu, suala la kumuhudumia mpenzi wako lipeni umuhimu ili kumnyima mpenzi wako sababu za kukucheat
 
Kijana huyu anafikirisha Sana
Niliwahi kujiuliza hivi inakuwaje Mwanaume anahonga

Lakini nimegundua ukiona mtu anasema hawezi kuhonga ujue huyo hana hela

Kuna jamaa hapa DSM amemjengea binti mmoja hivi Nyumba ya Ghorofa

Wakati wewe roho yako inakuuma kisa umempa demu shilingi 50,000 yako ya ngama, Kuna jamaa hapo Mbezi Kwa Msuguri amemjengea binti ghorofa ya zaidi ya shilingi milioni 250
 
😁😁😁 aisee hiyo Kama yule jamaa waziri wa mambo ya mitutu alimjengea mchipuko kisima cha mafuta karagwe (kagera)
 
Moja ya dalili zinazomtambulisha Mwanaume dhaifu ni kuhonga wanawake. Hata siku Moja huwezi kuta mwanaume Kamili anayejiamini na Alpha Male akahonga Wanawake.
Bunga Bunga parties za Silvio Berlusconi je?

Silvio Berlusconi Waziri Mkuu wa Zamani wa Italia alijulikana kama mtu assertive asiye na udhaifu na alikuwa Billionea. Huyo bwana alikabiliwa na madai mengi sana ya kuhongahonga wanawake, hususani kwenye party zake za Bunga BungaπŸ˜€




au hawa hawahusiki? Tunaelimishana.
 
Hiari na lazima ni vitu viwili ambavyo haviwezi kukaa pamojaa.

Neno lazima ni command mkuu halina mbadala kabisa.Mchumba akikuambia ges imeisha unaweza ukamwambia sina hela.Jambo hilo nitofauti kwa mke wako hata kama mnaishi wawili tu itakuwia ulazima ukakope hela hiyo ili gesi ijazwe.

Mchumba ni jukumu la wazazi wake kumuhudumia wewe ni extra tu hata kama anaishi geto maana yake ana chanzo cha mapato ndio maana kapanga na umemkuta kapanga.

Iwapo ukamtoa sehemu na kumpeleka sehemu nyingine huyo ni mke maana atakutegemea kwa kila kitu hata akiumwa simu ya kwanza niwewe na utawajibika kulipia gharama zote.
 
Umeiweka vizuri hiyo Mkuu

Vijana wajitahidi kutokuwa na multiple partners ili kuweza kutunza kibunda Chao
 
Muda huo wewe ukiwa unaishi wapi sasa?πŸ€”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…