Kikwete na Magufuli walishindwa kuingusha CHADEMA lakini Rais Samia ndani ya miaka minne ameshamaliza anachofanya ni kuinyonyoa manyoya


 
Uchaguzi ujao ni kheri asitie mguu maana hajawahi Kutokea mfano wake.

Tusubiri

Yaani CCM inaishambulia CHADEMA kutokea ndani ya CHADEMA.

Zamani walikuwa wanatupiana mashambulizi kila Mmoja Akiwa kwenye eneo lake lakini sasa hivi CCM imefanikiwa kuingia kwenye eneo la CHADEMA.

Yaani ni Kam marekani anayepigana kwenye

Aiseeh
 
Baada ya huu uchaguzi wa mwenye kiti hakuta kua na mtu wa kumnyooshea tena kidole, so atakaa tu hadi aamue mwenyewe ya kwamba sasa inatosha na atamuweka yule anaemuona anafaa.
 
kuua chadema ni kuua demokrasia, ni wajinga tuu ndio wanafurahia au kufanya haya mambo, tushindane kwenye uchaguzi sio fitna na wizi wa kura
 

Kumsingizia Samia wakati mwenye kukifikisha chama hapa anajulikana hakusaidii.

Kwani hata public opinion imeshindikana kusomeka?



Kwamba imekuwa Je?
 
Hiko chama kimeshajiua rasmi wamepiga chafya kwenye kibatari na kiberiti kimeisha.
 
Heriel ukisema umepewa kazi hiyo sawa,ila bado sana,kuku hanyolewi akiwa hai,na pia kuku hanyonyoji bila maji ya moto.Chemsha kwanza maji yakichemka acha kuwanyonyoa hao.
 
Mama Samia ni gwiji la siasa za nchi hii. CHADEMA imeshafikia tamati.
 
Mkuu hizo ni ndoto, kuiua Chadema ni vigumu kwa sasa tumechelewa na haitawezekana tena.
 
Kumsingizia Samia wakati mwenye kukifikisha chama hapa anajulikana hakusaidii.

Kwani hata public opinion imeshindikana kusomeka?

View attachment 3195147

Kwamba imekuwa Je?

..uongozi wa Chadema una nafasi yake ktk kukizorotesha chama.

..Raisi na Dola wana mchango wao ktk dhuluma dhidi ya vyama vya siasa, ikiwemo Chadema.

..mjadala ulioko mbele yetu ni hoja ya Robert Heriel Mtibeli akimsifia Rais Samia kwa kubomoa demokrasia, na kuisambaratisha Chadema.
 
Kuna mwalimu wangu aliwahi kuniambia kuwa ukitaka kufikisha ujumbe mgumu kwa mwanaume basi mtumie mwanamke. Mbowe anajulika ni mdhaifu sana kwa wanawake. Samia alitumia uana-ake wake ku-interract na Mbowe na kumlainisha. Mbaya zaidi akapenyeza na rupia. Hakuna combination mbaya inayoweza kumfanya mwanaume apagawe kama mwanamke na fedha. Hapo sijaweka na ahadi ya madaraka. Summary: Upande mmoja amekaa rais mwanamke wa kizenji, mwenye sauti ya ushawishi na macho ya kurembua na upande wa pili amekaa mwanamme wa kichaga toka Machame, mpenda vimwana na fedha bila kusahau madaraka. Unategemea nini? Magufuli alikuwa anatumia ubabe na pia hakuogopa wapinzani kwani alikuwa anatumia dola wakati wa uchaguzi. Kikwete alikuwa anauma na kupuliza na alitaka upinzani uwepo kwa faida ya nchi.
 
Watch_Hundred is the famale version of JIWE.

Mikakati yote aliyoifanya JIWE ,Watch_Hundred alikuwa naye ni mmoja wa Planner ndiyo maana "MAKALAI" yote yalioyounga mkono juhudi kipindi cha JIWE ,Sir100 amewa-retain.

Adui muombee njaa atanyoosha mikono juu hata kama alikuwa shujaa(Afande Sele) ,JIWE aliwaletea njaa maadui zake kisha akawawekee "sahani ya ubwabwa" wakaunga mkono juhudi hapo ndipo walipoanza kuwamaliza.

Sir100 kupitia Abdul naye anasambaza mabilioni.
 
Siasa chafu za Afrika, zimepitiliza hata uchafu wenyewe. Hata watu wake wanafurahia namna wanasiasa wanavyofitiana, finally kufitiana kunaleta fitina hata kwenye maendeleo. Ndio maana maendeleo yao yanafanana na mipasho, nakshinakshi, ushambenga n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…