..tatizo kubwa zaidi ni Wasomi wa Kitanzania, waandishi mahiri kabisa, wanapoamini kwamba Maraisi wetu wanapaswa kusifiwa wanapotumia vyombo vya dola kuhujumu demokrasia na mifumo ya uchaguzi.
..Na tukienda mbali kidogo, tujaribu kuangalia nchi nyingine zilipoongozwa na viongozi wanawake kama India, wakati wa Indira Ghandi, au Uingereza, wakati wa Margareth Thatcher. Je, ni mambo gani kina mama hao walisifiwa nayo?
..Hivi kweli sifa ya kudhulumu haki ni jambo la kumsifia mwanamke wa Kitanzania, tena ambaye ni kiongozi?