KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Hiyo inakuonyesha kwamba kiongozi wa namna hiyo hakuwa na uchungu na maslahi ya nchi hii. Hata huo mchakato alioruhusu ufanyike haukuwa moyoni mwake kabisa; kwamba anatafuta njia ya kuinufaisha Tanzania.sasa hivi tunaotaka katiba mpya tunachambwa,kusutwa na kutukanwa,yeye kama mzee wa nchi kakausha tu. unaweza kudhani Hii nchi haina wazee
Linganisha hali hiyo na ile ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, hata baada ya kung'atuka.
Hawa wenzetu, uongozi ni kutafuta sifa na kujinufaisha, ndivyo vipaumbele vyao; ndio msukumo wa kusaka uongozi.