Haujioni mwenye hatia unapowaona watoto wako mashoga, mateja, waathirika, na hata wakifungwa kifungo cha maisha?
Hayo ni matokeo ya maisha, na kuna watu wana watoto wa hivyo na wa nawapenda watoto wao vizuri sana,
Tuanze kuchambua
1. Mashoga- ni changamoto ila familia nyingi zimejifunza kukubali watoto wa hivyo maana hao watoto hawakuchagua kuwa hivyo. Na mifano ipo baada ya kuwa kubali watoto hao wapo wengi waliofanikiwa walipokuwa wa kubwa, miongoni mwa watu waliofanikiwa mafanikio makubwa duniani wamo hao mashoga. Suluhisho la mtoto shoga ni kukubali kuwa yuko hivyo maana hakuna namna nyengine na sio yeye wakwanza wala wa mwisho kuwa hivyo alivyo.
2. Mateja, kama nilivyosema ni changamoto tu ya maisha, wapo watu walijiingiza katika uteja na wakapona na wanaishi maisha yao mazuri tu, sitaki kuorodhesha majina ya watu maarufu walioweza kujinasua baada ya kutumia madawa maana siwajui personally
3. Uathirika ni tatizo tu la kimaisha, na binadamu kaumbiwa matatizo
4. Kufungwa kifungo cha maisha-hilo halipaswi kukuumiza wewe mzazi maana mpaka mwanao kafikia hapo ni shauri lake, kwanini kafanya kosa la kufunga maisha. Mfano mwanao kaua kwa kudhamiria, hivi ye hajui kuwa hilo ni kosa???
Halafu kama una imani ya Mungu utafahamu kuwa binadamu tunaukomo wa kupata tunachotamani ama kukipenda lazima ufike hatua uinue mikono juu uombee tu Kile kinachokushukia maishani, kwa sababu huwezi kucontrol kila kitu asilimia mía ikiwemo kizazi chako