Mkuu unatakiwa kujua kwamba sio kila mwenye bunduki lazima akufyatulie ndo ujue kama anayo au hana.
Aidha sio kila penye mabomu yanapaswa kuripuka kama mbagala na gongo la mboto ili uamin kwamba kambi za jeshi kuna ghala za mabomu au laa.
Hilo ulilosema ni BIG NO, wananchi wananguvu na wanaweza kukushangaza haijalishi wanaandamana au wako kimya.
Jambo la msingi ni kwamba msiwadogoshe kihiivyo.
Bali tushukuru kuwa na taifa lenye raia wenye hekima, utulivu na uvumilivu na sio kuwaita waoga na wanafiki.
Yaani kama ikifika mahali tuamini kwa kuona reaction tunayofikiri kwamba ndo kigezo cha kumaanisha kwao, bhasi ujue saa hiyo utakuwa unajipigania nafsi yako, utakuja kushtuka hau na familia yako uliyopenda kuwa nayo karbu. Utakuja jikuta unalala porino au ndugu zako wa kike wanabakwa n. K.
Tuache utomaso au ule utoto wa kuchezea kijinga cha moto tuamin tuu kwamba moto una unguza wala tustaman kujaribia kwa kujichoma sehemu za siri tutaacha makovu ya aibu.
Wananchi wanapaswa kupongezwa kwa kuto kureact katika visa vya namna hiyo ila ukweli nkwamba wanajua mengi kama siyo yote yanayofanywa na wanasiasa yenye kuumiza, kuwaliza, kuwakatisha tamaa, kuwapa tumaimi na kufurahisha pia, kuhusu nchi yao na baba zao.