hilo jibu halihitaji JK, hata Mimi nitakujibu
Prof Assad kaunga Mkono Mkataba kashambuliwa Mdini,
sasa hivi kila Mtu akipinga Mkataba anaonekana Mkristo na kila anaeunga Mkono anaonekana Muislam,
kwanza inaua Principle za uhuru wa kujieleza kiasi kwamba Mkristo ataona shida sana kuunga Mkono Mkataba hata kama kwa nafsi yake na Taaluma yake ataona inafaa kwa kuwa anaonekana anapingana na Imani yake na Mwislam nae atajihisi jama kulitumikia Kanisa akipinga Mkataba
Kuvuruga Amani ya Nchi ni jambo rahisi sana sana na huwa inaondoka kimchezo mchezo
kuna watu wanadhani ni mchakato wa miaka na miongo kadhaa
Tuendelee kunyanyapaa Viongozi wanaopandikiza Chuki na mifarakano kwny Jamii
the same kwa
Wewe acha zako hizo, ni wapi Profesa Asad alitoa facts au majibu ya vipengele vinavyolalamikiwa!? Yeye aliishia kutoa conclusion huku akisema tuwasikilize wanasheria wa uwekezaji tu huku akisahau kwamba yeye katoa maoni (kwanza bila facts) lakini kasikilizwa.
Kauli juu ya kwamba aliitwa mdini labda ilitokana na kutotoa facts zozote na kuishia kuunga mkono tu mkataba.
Huu ujinga mnaoleta sasa ati dini na siasa, sasa hiyo dini itakuwa na maana gani kama haimkomboi mwanadamu juu ya rasilimali zake na kuzipigania? Kwanini mnakimbilia tu sentensi legevu "dini na siasa" badala ya kujibu hoja na vipengele vyenye utata!?
Kwa hiyo, kwa kauli yako, ni bora kila tulichonacho tumpe mgeni alimradi tu tukipinga, amani itatoweka. Yaani bora tuwe na amani na utulivu huku tukiwa watumwa kwenye nchi yetu, au sio!? Nooo man!
Sikiliza kuwa Rais au kuwa Rais mstaafu haikupi kibali kwamba unauzalendo sana kuliko wengine, na hivyo tukuamini hata pale tunaposoma wenyewe tumeliwa!!! Mataifa mangapi duniani yameuzwa na viongozi wao waliokuwa marais kabisa... Huko West Africa, mapinduzi yanatokea kila leo kwa sababu marais wao wameuza nchi, ndiyo maana. Kwa hiyo, hatusikilizi wala kutazama urembo wa sura wa mtu, tunatazama facts zilizopo kwenye mkataba, hatuutaki muelewe... Nimemshangaa sana Kikwete, kwa mfano, alioutoa wa Zanzibar. Yeye na chama chake wamekuwa kinara wa kuwaibia chaguzi zao Zanzibar, alitegemea nini kwenye dhulma kama ile!? Sasa akae ajue kwamba sauti za watu zinahitaji kusikika... Ati udini udini, yeye alipotangazwa kwamba ni chaguo la Mungu na Kardinal Pengo, mbona hakukemea? Au inafaa pale tu inapokuwa upande wao!!!!