Kila siku wako Misikitini na Makanisani wakihubiri siasa lakini wa kwanza kusema tusichanganye dini na siasa

Kila siku wako Misikitini na Makanisani wakihubiri siasa lakini wa kwanza kusema tusichanganye dini na siasa

Wakuu Mimi n maamuma TU katika sheria lakn nashangaa Sana katiba yetu inasema kila mtanzania Ana haki ya kutoa maoni kwa Jambo lolote lihusulo nchi yetu

Wiki hii kanisa katoliki limetoa maoni kupitia baraza la MAASKOFU yaani TEC na wameorodhesha vifungu Tata vya mkataba ambavyo wao wanaona Kama vinafaa kurekebishwa maajabu anatokea mtu anasema Ni udini TU unaowasumbua hawa MAASKOFU

Mm nilitegemea watajibu kadiri ya maswali yaliyoulizwa juu ya vipengele Tata lakn mtu anakimbilia kusema udini

USHAURI wangu n vema wakajibu hoja iliyopo mezani kuliko kujikita kwenye udini
 
Wapi nimesema hayo ? Kwanza elewa ninacho kiandika hapa.

Mimi masheikh zangu hawajaongelea suala hilo la Bandari, na kama ikitokea Kuna haja ya kumkosoa kiongozi au kuhoji, Hawa hoji kwenye majukwaa au misikitini, bali wanaandika barua iende kwake au wanamfata kwa Siri, akikubali kukosolewa ni jambo jema kwake, asipokubali basi wajibu wao wanakuwa wameufata na kuutimiza.

Ila masheikh zetu sisi wametumihiza juu ya kuwapinga wale wote wenye kuchochea uvunjifu wa amani, na tusiwasikilize kama wafanyavyo Maaskofu, huu ni uchochezi na wanaonyesha ni kwa namna gani Wana akili ndogo na Wana mihemko. Ukiangalia tu huo Waraka, una makosa madogo ya kiuandishi halafu mnakuja kutuambia ni wasomi na watu makini, wakati Waraka unaonyesha Wana pupa na chuki za kijinga.
Huyu ni shehe au sio shehe.

TEC wamepinga kwa hoja na kuainisha vifungu wasivyokibaliana navyo, udini unaingiaje hapo? Kwamba maaskofu hawaruhusiwi kutoa mawazo yao juu ya mambo ya kitaifa?

Je huu mkataba unanufaisha waislam ndiyo sababu wanautetea? Au waislam hawapendi Rais muislamu akipingwa?
Yaani ni ajabu sana kwa kweli jk kakosea sana
 
Huyu ni shehe au sio shehe.

Huyo Sheikh kwa uhakika wake. Masheikh lazima wafate mafundisho sahihi ya Mtume.
 
hilo jibu halihitaji JK, hata Mimi nitakujibu

Prof Assad kaunga Mkono Mkataba kashambuliwa Mdini,

sasa hivi kila Mtu akipinga Mkataba anaonekana Mkristo na kila anaeunga Mkono anaonekana Muislam,

kwanza inaua Principle za uhuru wa kujieleza kiasi kwamba Mkristo ataona shida sana kuunga Mkono Mkataba hata kama kwa nafsi yake na Taaluma yake ataona inafaa kwa kuwa anaonekana anapingana na Imani yake na Mwislam nae atajihisi jama kulitumikia Kanisa akipinga Mkataba

Kuvuruga Amani ya Nchi ni jambo rahisi sana sana na huwa inaondoka kimchezo mchezo

kuna watu wanadhani ni mchakato wa miaka na miongo kadhaa

Tuendelee kunyanyapaa Viongozi wanaopandikiza Chuki na mifarakano kwny Jamii

the same kwa
Walioanzisha utetezi wa dini kwenye mkataba huu ni CCM, sijui walitaka kumtisha nani na kwa faida ya nani?
 
TEC wamepinga kwa hoja na kuainisha vifungu wasivyokibaliana navyo, udini unaingiaje hapo? Kwamba maaskofu hawaruhusiwi kutoa mawazo yao juu ya mambo ya kitaifa?

Je huu mkataba unanufaisha waislam ndiyo sababu wanautetea? Au waislam hawapendi Rais muislamu akipingwa?
Nahitimisha kusema hivi hawapendi raisi muislamu kupingwa
 
Dini na siasa vyote mlaji wao ni mwananchi unavitenganishaje?
Dini na siasa unazitenga vipi? Tuchukulie walioleta dini walijitenga na siasa? Kwa upande wa Waislamu, Mtume Muhammad alipigana vita vingi vya Badr, Uhud, Khandak na Hunayn, je alichanganya dini na siasa? Kwa Wakristo Yesu alikemea maovu ya watawala mpaka akasulubiwa, je alichanganya dini na siasa? Kwa kifupi dini na siasa unazitenga vipi?
 
Kikwete atueleze je udini unaingiaje katika kupinga mkataba wa bandari? Na je ni dini gani itanufaika na huu mkataba wa DPW na TPA?

Tunataka tuelezwe uzuri au ubaya wa mkataba huu na siyo kujificha nyuma ya kichaka cha siasa na dini!
Kazi kweli kweli
 
Jifunze kujenga hoja na kukosoa hoja. Waraka wenu umeonyesha ni kwa namna gani Ukatoliki hauna misingi, inakuwaje wanarejea katiba kama msingi wa hoja yao ? Sasa hapo ndipo utaona umbumbu wa Maaskofu yaani hawana tofauti na Wanaharakati na Wanasiasa.

Ukija wakati wa kuwazungumzia Masheikh tutawazungumzia, masheikh wangu Mimi hukuti wakifanya hivi, sababu wao wanafata misingi ya uislamu na kuna taratibu ambazo alizielekeza Mtume wetu namna ya kuwakosoa Viongozi hasa wale viongozi madhalimu. Hili ukifika wakati wake tutaliweka wazi. Hapa tunawaongelea viongozi wenu ambao hawana misingi sahihi ya kuegemea katika jambo lao, zaidi ya kufata upepo wa Wanasiasa na kuandika mambo ya uongo na uzandiki.

Masheikh wangu Mimi wameandika vitabu na vitabu kuikosoa Demokrasia na kuonyesha ya kuwa Demokrasia ni ushetani, ila ukiwasoma viongozi wenu ambao hawafati mafundisho ya Yesu utawaona wanaipigia chapuo Demokrasia na kunukuu ibara katika katika ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Wana tofauti gani na Wanasiasa na Wanaharakati ? Huoni wanaiiingiza dini kwenye siasa na kuonyesha dini yenu haijakamilika ?

Wapi Yesu alifundisha Demokrasia na kuiunga mkono ? Hata wakiona Paulo wapi wakifanya haya wanayo fanya Maaskofu ? Halafu mnajiita wasomi ?

Waislamu sisi hasa Mimi na masheikh hatuna mpango wa kuujua huo mkataba, ila tunakemea wale wachochezi wenye kuwakosea heshima viongozi na kuwatukana, hakuna mitume ambao waliwatukana viongozi wao hata kama walikuwa waovu hakuna mitume ambao walikuwa wachochezi na waongo ?!

Haki wanayo, swali wanahoji kwa misingi gani na kwa njia gani ? Dini yenu haijatoa mafundisho ya namna gani uhoji ? Basi kama haijafundisha siyo dini ya kufata. Yesu aliwafundisha nini juu ya kuhoji au kuwakosoa Viongozi ?
Ebo! Kwa hiyo ulitaka katika kuhoji wasitumie katiba kama reference! Hujui katiba ndiyo mwongozo uliokubalika katika kuendesha siasa na utawala wa nchi hii!

Sasa kama nyie waislam hamtaki kujua yaliyomo katika mkataba mnapata wapi uhalali wa kuhoji waraka wa maaskofu ambao unakosoa mkataba?

Ukweli ni kuwa mashehe wenu walio wengi hawana elimu ya kutosha hata kuelewa mkataba wenyewe na ndiyo sababu wamebaki kulalamika kuwa kuna udini wakati hoja ni kuwa mkataba ni mbovu na wa kifisadi! Maaskofu wanapojaribu kuwaelimisha namna serikali ilivyopotoka mnaona ni uchochezi dhidi ya serikali!

Ningefurahi kama wewe ingejikita katika kujadili vifungu vya mkataba badala ya kutaka kujadili mafundisho ya Yesu Kristo!

Mtu ye yote ambaye anaamini kuwa dini na siasa havitangamani basi hajui anachojua. Nchi zote zinazotawaliwa kwa Sheria ya kiislamu zinachanganya dini na siasa mfano Iran, Iraq, Pakistan, Saudi Arabia, Afganistan nk.
 
Ebo! Kwa hiyo ulitaka katika kuhoji wasitumie katiba kama reference! Hujui katiba ndiyo mwongozo uliokubalika katika kuendesha siasa na utawala wa nchi hii!
Sahihi kabisa unajua maana ya kufata dini ? Maana lazima utumie misingi ya dini yako kama muongozo katika kuyaendea mambo. Maana yake kutumia katiba kama marejeo wewe unakuwa hufati dini sababu katiba no matokeo ya maoni ya watu ambayo yana mapungufu mno.

Usiwe unakurupuka kijana, tumia akili kuhoji mambo.

Umekubalika na kina nani ? Kwanini Kuna dini ? Maana ya dini ni nini ?

Kwahiyo nyinyi Wakristo muongozo wenu ni Katiba au Biblia ?

Ndio maana nasema hivi Maaskofu akili ndogo sana.
 
hilo jibu halihitaji JK, hata Mimi nitakujibu

Prof Assad kaunga Mkono Mkataba kashambuliwa Mdini,

sasa hivi kila Mtu akipinga Mkataba anaonekana Mkristo na kila anaeunga Mkono anaonekana Muislam,

kwanza inaua Principle za uhuru wa kujieleza kiasi kwamba Mkristo ataona shida sana kuunga Mkono Mkataba hata kama kwa nafsi yake na Taaluma yake ataona inafaa kwa kuwa anaonekana anapingana na Imani yake na Mwislam nae atajihisi jama kulitumikia Kanisa akipinga Mkataba

Kuvuruga Amani ya Nchi ni jambo rahisi sana sana na huwa inaondoka kimchezo mchezo

kuna watu wanadhani ni mchakato wa miaka na miongo kadhaa

Tuendelee kunyanyapaa Viongozi wanaopandikiza Chuki na mifarakano kwny Jamii

the same kwa
Maoni yako ni mazuri Sana lakini wakati CCM inajifungamanisha na Dini hamkusema.
 
Kikwete atueleze je udini unaingiaje katika kupinga mkataba wa bandari? Na je ni dini gani itanufaika na huu mkataba wa DPW na TPA?

Tunataka tuelezwe uzuri au ubaya wa mkataba huu na siyo kujificha nyuma ya kichaka cha siasa na dini!
Kikwete ni mtu asiyejali chocho ndo maana alingia mikataba ya hovyo hovyo ,halafu anataka mpaka karne hii tuendele na haiyo na iana hiyo ya mikataba kwa kuwa yeye na wajukuu. Wake wana uhakika wa maisha
 
Sahihi kabisa unajua maana ya kufata dini ? Maana lazima utumie misingi ya dini yako kama muongozo katika kuyaendea mambo. Maana yake kutumia katiba kama marejeo wewe unakuwa hufati dini sababu katiba no matokeo ya maoni ya watu ambayo yana mapungufu mno.

Usiwe unakurupuka kijana, tumia akili kuhoji mambo.

Umekubalika na kina nani ? Kwanini Kuna dini ? Maana ya dini ni nini ?

Kwahiyo nyinyi Wakristo muongozo wenu ni Katiba au Biblia ?

Ndio maana nasema hivi Maaskofu akili ndogo sana.
Sasa kama maaskofu wamerejea katiba katika hoja zao ni vipi mnabwabwaja kuwa wameingiza dini katika siasa?

Dini zipo ili kutoa miongozo ya kiroho kwa binadamu na kila mtu ana dini yake. Uislamu ni dini yako na si ya watu wote.

Wakristo wanafuata vyote biblia kwa mambo ya kiroho na katiba kwa mambo ya utawala na maendeleo. Bahati mbaya kwenu waislamu mambo yenu ya kutaka kutumia Sharia hayana nafasi Tanzania hivyo lazima mfuate katiba. Ndiyo sababu Sheikh Mselemu alifungwa na Kikwete na hamkufurukuta mpaka alipoachiwa na Samia baada ya kusota zaidi ya miaka 7.

Nakushauri wewe ndiye unapaswa kutumia akili kuihoji serikali na siyo kutumia Sharia ambazo hazina nafasi katika utawala wa nchi hii!
 
Kikwete ni mtu asiyejali chocho ndo maana alingia mikataba ya hovyo hovyo ,halafu anataka mpaka karne hii tuendele na haiyo na iana hiyo ya mikataba kwa kuwa yeye na wajukuu. Wake wana uhakika wa maisha
Kikwete ni mtu wa hovyo sana anajali tumbo lake tu!
 
Kama ni kusali nenda kasali ukipewa nafasi ya kusalimia waumini toa fungu la biblia au msitari wa Quran lkn ukianza kuongelea siasa au kuwananga wanasiasa kwenye kibweta na wewe unaingiza siasa kanisani. Nyerere kila Jumapili alikuwa anahudhuria misa St. Peter’s lkn ilikuwa nadra sana kupanda kwenye kibweta na kuanza kuwananga wanasiasa. Leo hivyo hivyo ya kesho yanafurahisha.
Screenshot_20230821-151455.png
 
Back
Top Bottom