Kilichonitokea kituo cha Daraja la Salenda baada ya kushuka kwenye daladala saa nne usiku

Kilichonitokea kituo cha Daraja la Salenda baada ya kushuka kwenye daladala saa nne usiku

Daaah...
Mkuu Kiasili kabisa , binadamu hatujaumbiwa kutoana uhai...na ikitokea ukafanya, itakutesa mno...
Matokeo yake ndo kama hayo , kujiua au kudata...
Alimpiga denti wa zanaki akazimia.Basi akajua kaua,akaenda home akajiua.Nadhani ilikua mwaka 1992 au 1993 kama sikosei mkuu.Way back enzi hizo tambaza wapo o level students
 
Wanasemaga kuna majini lakini nishawahi kupita hapo mara 2 saa 3 na saa nne usiku hakuna maajabu niliyoona.

Siku ya mwisho nilitoka Upanga, wakati narudi usafiri ukaharibika kwenye mataa. Nikasubiri kama dk 20 hakuna usafiri, nikaamuua kuunga ila nilikuwa napita katikati ya barabara hadi stanbic pale nikabahatisha bajaji.
 
Mkuu ni kweli ila sasa hivi ulinzi umerudi mkuu,kuna askari wa doria wanaweka kambi mle ndani kwenye mianzi siku moja moja.

Hata vibaka wakiiba waga hawakimbiilii mle ndani kwenye vichaka. Nenda pale kinondoni makaburini kwenye kituo cha daladala za mwananyamala, utakutana na vibaka waastaafu watakupa update za hiyo njia ya salender bridge siku hizi ipoje.Ukiona kibaka anaiba hapo ucku bas ujue akimbilii kule kwenye vichaka wanaogopa asikari.
"wanaweka kambi mle ndani kwenye mianzi siku moja moja", unaongelea daraja la Salenda la wapi! Hiyo mianzi imetoka wapi? Daraja la Salenda nilijualo lina mikoko tu.
 
Alimpiga denti wa zanaki akazimia.Basi akajua kaua,akaenda home akajiua.Nadhani ilikua mwaka 1992 au 1993 kama sikosei mkuu.Way back enzi hizo tambaza wapo o level students
Nakumbuka Mkuu, si mpaka waliifunga kwa muda hiyo miaka? ...
Na ndo matokeo pia ya kufuta O level...
Kulikuwa na ukorofi mwingi mno pale Tambaza
 
Wanasemaga kuna majini lakini nishawahi kupita hapo mara 2 saa 3 na saa nne usiku hakuna maajabu niliyoona.
Siku ya mwisho nilitoka upanga, wakati narudi usafiri ukaharibika kwenye mataa. Nikasubiri kama dk 20 hakuna usafiri, nikaamuua kuunga ila nilikuwa napita katikati ya barabara hadi stanbic pale nikabahatisha bajaji.
Hiyo tabia ya kupita katikati ya barabara ni mimi mtupu mkuu...
Mi hutaona usiku wa maneno hasa usiokuwa na watu nikapita pembeni ya barabara...hahaha
Umenikumbusha mbali sana. , siku moja nilienda kumtembelea ba mdogo , pale mnazi mmoja ilikuwa siku ya mkesha wa Krismas , kwahiyo tulitoka church kwenye mkesha mida mibovu, nafikiri kwenye saa saba...
Mi nikaforce niende Mbezi ile night, sasa kutoka pale mnazi mmoja kuitafta fire, nikawa napita katikati ya barabara, nilipovuka pale D.I.T kwa mbele nikamuona muhuni ananoa panga kwenye lami...nikajisemea huyu kima ningekuwa napitia pembeni nilikuwa halal yake Leo...
Nilikuwa najipanga, akianza kunisogelea tu... nakata mbio za kufa mtu mpaka kituo cha fire...pale watu walikuwa hawalali...[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Uandishi wa hovyo ambao mtu mzima hapaswi kuandika.

"sikumbuki nini kilitokea ila nilijikuta ile njia ya muhimbili nipo kwenye kituo karibu na chuo sijui ndo mzumbe nasubiri gari ya kutoka kariakoo nirudi masaki"

Kichwa cha Habari:

"kilichonitokea jituo cha daraja la salenda baada ya kushuka kwenye dala dala saa nne usiku"​

Swali:

Ni nini kilikutokea?
Kazoea kuvuta Bangi ya Mvuke wa Nnya kutoka Kwetu Tarime Mkoani Mara ( Musoma ) Tanzania ila kwa alichokiandika ambacho ni Maluweluwe ( Pumba ) tupu atakuwa Kavuta Kitu cha Blantyre cha nchini Malawi kilichochanganywa na Mvuke wa Gongo na Chembe chache cha Kinyesi cha Mnyama a.k.a Mwanadamu.
 
Nakumbuka Mkuu, si mpaka waliifunga kwa muda hiyo miaka? ...
Na ndo matokeo pia ya kufuta O level...
Kulikuwa na ukorofi mwingi mno pale Tambaza
Na mabishoo wengi walikua wanatokea pale tambaza na shabani robert miaka hiyo.Watoto wa kishua unawakuta tanganyika international.
 
"wanaweka kambi mle ndani kwenye mianzi siku moja moja", unaongelea daraja la Salenda la wapi! Hiyo mianzi imetoka wapi? Daraja la Salenda nilijualo lina mikoko tu.
Ndio hiyo hiyo mikoko mkuu ndani ya ile hifadhi ya maliasili kuna bango lao pale la kukataza watu wasifanye shughuli yoyote mle ndani🤣🤣🤣Sijasoma biology so sijui kutofautisha mimea mkuu.
 
Back
Top Bottom