Kilimanjaro: Naomba tumsaidie Mwanafunzi Sifika Daniely Ruben apate haki yake na arudi shule

kwa mfano wa yule aliyeiba mitihani Galanosi na kukimbilia Forest, makalai matupu- kwa hisani ya Job Ndugai huko alipo....na tabia hii ya udokozi hakuna mwenye kutaka kuikemesha. Hawa vilaza wamechekewa sana. sasa na wanyongwe si tu miaka 10 jela.
 
Haya mambo mbona yapo, itakuwa hujaishi vijijini wewe , Kuna Ile issue ya binti wa kiislamu mkoa wa Pwani ilikuwa hivi hivi mpaka serikali ikaingilia kati na dogo akaenda shule.
 
Michezo hii ilikuwepo sana zamani...hadi waziri mmoja alishafanya na alishajitetea sana hapa ...
Mtoto huyu anahitaji msaada zaidi ya huo wa kurudishwa shule maana anatokea familia masikini sana..
Nilishafanyiwa huu mchezo Ila ilikuwa darasa la Saba..
Hivi ndivyo tunalalamikia serikali, uongozi wa juu ukiwa mkali watumishi wanakuwa na nidhamu.
Ile nidhamu ya SIMBA wa yuda ndio ilileta nidhamu.
Halafu unakuta aliyeuziwa nafasi baadae anakuwa kiongozi analetea dharau watanzania.
 
Ungekua yeye ungefanyaje?
Ndugu, we acha tu. Binafsi hali hiyo ilikwisha nipata. Nilinyimwa joining instructions ya Makoko seminari kule Musoma kisa tu baba yangu hafuati misingi ya ukatoliki. Siwezi sahau tukio lile. Niliponda mawe, nikauza kokoto na kupata fedha ili nitoe rushwa ya kumuhonga mtu wao (anaitwa Padre Masaga)... sijui siku hizi yuko wapi. Huyu Kiumbe nilimchukia hadi sasa kwa jinsi alivyonifanyia ili nipate joining instruction ya makoko seminari kisa tu makosa ya baba yangu kuto kukubari misimamo ya RC. Nimefauli lakini naadhibiwa kwa makosa ya mzee wangu. Siwezi sahahu.
 
Kwa kweli huu ni uhuni wa kuharibiana maisha, huyu binti anahitaji msaada wa fikra na mali, mpaka inafikia atafute kazi ya ndani ni kweli ameshikika, inavyoonyesha hakuna mtu wa kumshauri na kumtetea katika familia yao vilevile hali zao za kiuchumi ni duni. Mamlaka husika ifuatilie nini hasa kilichotokea ili haki ipatikane. Ikiwa hakuna kitakachofanyika basi wana JF watamsomesha huyo binti mpaka pale atakaposema inatosha.
 
Kwa walichokufanyia naamini unaona ni sawa mzee alivyogomea misimamo yao
 
Hii kitu ipo sana katika shule za serikali,kama shule imepelekewa wanafunzi 70 walimu usubiri watakaoshindwa kuripoti kwa wakati kuwachomeka wanafunzi wengine
 
Wenye akili za matope kama nyinyi hamuwezi kukosekana.

Mwandiko wenyewe kama wa mume wa zamaradi
 
Dah ila kapasua kinoma,asaidiwe ana kitu.
 
Ulikosa shule za serikali?
 
Muheshimiwa Dr Gwajima popote ulipo,pls ingilia kati swala hili pls nakuomba,tia mkono wako ili lifanyiwe kazi faster na mammlaka husika!! Dhuluma ya aina yoyote ile haikubaliki ndani ya jamii iliyo staraabika na tunaishi kwa misingi ya.sheria!!
 
Mtu nafasi yake inauzwa afu anaenda kuwa hausigel,hayuko serious huyo
Hataki shule
Usizani kila mtu anaupeo mkubwa kama wako huzulumiki haki yako maana unajua the all procedure ya kupata haki yako, kuna wengine kweli hawajui, na wnaishia kumuachia Mungu!! Alafu kumbuka pia mdada kafunguka mwenyewe kwa the New Boss, na Boss ndiyo akalileta humu kwa msaada zaidi kwa Binti apate haki yake!!
 
Kama kuna ushahid wa kweli asikilizwe,huwenda Jinai ikibuka hapo kama kweli kitengo kikiaamua kufanya kazi bila ya double standard!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…