Makosa huwa yanatokea, na kila binadamu hufanya makosa, lakini mwanadamu mwenye busara huwa hapendi kuona makosa yanajirudia, ikiwa unaweza kumuonea huruma binti asiyekuhusu vipi kutomsaidia mtu anayekuhusu?Si sawa kwa walicho nifanyia, mtoto hawezi kupewa adhabu kwa makosa ya wazazi wake. Ingawaje mimi ni RC, lakini sikubaliani na ile rushwa waliyoniomba. Miaka ya 1994, ilikuwa fedha ndefu hadi bibi yangu ikabidi auze mali zake huku asomesha toka kwangu. Jibu langu huwa ni rahisi sana... Mbegu ya haradari iliyotupwa juu ya miamba huwa haizai.... pambana na hali yako mzee maana uliniacha na hali yangu. Ni hayo tu. mauvimu ni mengi kwa kweli, kama hujapitia maisha ya kuponda kokoto, kuuza matunda, kupika vibaragashia, we acha tu ndugu, shukuru Mungu alikuepusha na maisha hayo.
Hao ndugu zako hawana kosa kama wakihitaji msaada na wewe unauwezo wasaidiye ili waje kujisaidia wenyewe, maisha haya yana changamoto nyingi, shukuru wewe umefanikiwa lakini umepitishwa kwenye njia ngumu, ndiyo naweza kusema waokozi wa watu huwa wanapitia magumu sana na inavyoonyesha wewe ndiye mwokozi wa familia yenu.
Katika maisha mzazi si mtu wa kuzinguana naye jinsi itakavyokuwa ni mzazi wako tu, tambua nawe ni mzazi au utakuwa mzazi yanaweza kukutokea makubwa kuliko baina yako na mzee wako, hivyo rudisha moyo wako kwa kumsamehe mzee wako na wasaidiye ndugu zako utaona jinsi maisha yako yatakavyobarikiwa.