S.M.P2503
JF-Expert Member
- Nov 25, 2008
- 2,421
- 4,344
Si sawa kwa walicho nifanyia, mtoto hawezi kupewa adhabu kwa makosa ya wazazi wake. Ingawaje mimi ni RC, lakini sikubaliani na ile rushwa waliyoniomba. Miaka ya 1994, ilikuwa fedha ndefu hadi bibi yangu ikabidi auze mali zake huku dingi amekaza shingo.Kwa walichokufanyia naamini unaona ni sawa mzee alivyogomea misimamo yao
Nachosema ni kwamba, huyo binti anahitaji msaada wa hali na mali na hiyo ya yeye kwenda kutafuta u house girl ni njia mojawapo ya kutatua changamote zake.
kwangu mimi, niliponda kokoko, nikauza maembe, machungwa, mananasi, nikapalilia mashamba ya watu na kuuza vitumbua na vubaragashia vya ndizi na unga wa sembe ( kama ulisha wahi visikia) lakini bado sikufua dafu. Ila kwa kuwa nilikuwa determined, niliweza kutoboa kwa nguvu zangu binafsi na msaada kidogo wa bibi yangu (RIP) aliyeuza baadhi ya mali zake ili tu nipewe joining instructions.
Haya ya dingi, sikukubaliana na misimamo yake maana alitakiwa kuweka mbele maslahi ya watoto wake mbele na wajibu huo wazazi wengi hawautaki, ni maslahi yao kwanza. Baada ya hapo akaoa tena mke wa pili na kufyatua watoto lukuki na sasa anataka msaada wa kuwasomesha toka kwangu. Jibu langu huwa ni rahisi sana... Mbegu ya haradari iliyotupwa juu ya miamba huwa haizai.... pambana na hali yako mzee maana uliniacha na hali yangu. Ni hayo tu. mauvimu ni mengi kwa kweli, kama hujapitia maisha ya kuponda kokoto, kuuza matunda, kupika vibaragashia, we acha tu ndugu, shukuru Mungu alikuepusha na maisha hayo.