Kilimanjaro: Naomba tumsaidie Mwanafunzi Sifika Daniely Ruben apate haki yake na arudi shule

Kwa walichokufanyia naamini unaona ni sawa mzee alivyogomea misimamo yao
Si sawa kwa walicho nifanyia, mtoto hawezi kupewa adhabu kwa makosa ya wazazi wake. Ingawaje mimi ni RC, lakini sikubaliani na ile rushwa waliyoniomba. Miaka ya 1994, ilikuwa fedha ndefu hadi bibi yangu ikabidi auze mali zake huku dingi amekaza shingo.

Nachosema ni kwamba, huyo binti anahitaji msaada wa hali na mali na hiyo ya yeye kwenda kutafuta u house girl ni njia mojawapo ya kutatua changamote zake.

kwangu mimi, niliponda kokoko, nikauza maembe, machungwa, mananasi, nikapalilia mashamba ya watu na kuuza vitumbua na vubaragashia vya ndizi na unga wa sembe ( kama ulisha wahi visikia) lakini bado sikufua dafu. Ila kwa kuwa nilikuwa determined, niliweza kutoboa kwa nguvu zangu binafsi na msaada kidogo wa bibi yangu (RIP) aliyeuza baadhi ya mali zake ili tu nipewe joining instructions.

Haya ya dingi, sikukubaliana na misimamo yake maana alitakiwa kuweka mbele maslahi ya watoto wake mbele na wajibu huo wazazi wengi hawautaki, ni maslahi yao kwanza. Baada ya hapo akaoa tena mke wa pili na kufyatua watoto lukuki na sasa anataka msaada wa kuwasomesha toka kwangu. Jibu langu huwa ni rahisi sana... Mbegu ya haradari iliyotupwa juu ya miamba huwa haizai.... pambana na hali yako mzee maana uliniacha na hali yangu. Ni hayo tu. mauvimu ni mengi kwa kweli, kama hujapitia maisha ya kuponda kokoto, kuuza matunda, kupika vibaragashia, we acha tu ndugu, shukuru Mungu alikuepusha na maisha hayo.
 
Imani na dini ni vitu viwili tofauti, wengi wana dini,lakini Imani hawana kama huyo Padri aliyekupiga pin kisa life style ya Dingi wako, alafu kama wwe umeamua kufanyia ibada zako kwenye nyumba za Ibada kwa nini ulazimishe na wengine hadi vikwazo vya kiuuchumi kuwekeana!!??
 
Ulikosa shule za serikali?
Nilivuka madarasa kwa uwezo wangu wa darasani na hivyo mitihani ya darasa la saba haikuwa bado. Kwa maana nyingine, nilifanya mtihani wa seminari nikiwa darasa la sita - mwaka mmoja kabla ya wa serikali LY . Yote kwa yote, sababu ya kuvuka darasa ni ili nikwepe elfu 40 ya wakati ule maana dingi alikwisha telekeza familia ya watoto 10 na kutafuta familia nyingine. Mama alikuwa ni mkulima tu.
 
Hakikisha na yeye hajakudanganya.
Sio tunasumbua watu kumbe mtoto hataki shule ama alifeli kabisa.
 
Jambo la imani ni gumu sana ndugu yangu, laniki nimejifunza kitu. Tangu siku hizo mpaka sasa, Mungu hajawahi kunitupa ktk ombi lolote ninalomuomba (baya au Zuri) hata bila kwenda kanisani. Shukrani kwange yeye Muumba aliye ndani ya nafsi yangu ayasikiaye maombi yangu bila kuchoka na kunipa matamanio yangu kila nimkimbiliapo... usicheze na maombi ukiwa umenuia. Mungu ni msikilizaji mzuri sana.. jua tu namna ya kuongea naye na si lazima kwenda kanisani , hata kimoyomoya anakusikiliza na kujibu tu.
 
0788174071
Namba ya waziri wa elimu hiyo mpigie . Duh Kuna watu wanyama kiasi hicho Karne hii aisee
Usihngaike kumpigia Mkenda huwa hapokei Simu!! Kila wakati Simu yake imezimwa hataki usumbufu!! Hao ndio mawaziri wa Samia.
 
Uongo mkubwa.

1.Matokeo gani yanaanza na SP?

2.Angalieni namba za usajili za taarifa ya yeriko na taarifa ya haya matokeo. Namba 2 tofauti. Hizi ni shule mbili tofauti.
 
Akaniambia amemaliza Form Four, Ana Division One ya 10, Nikamuuliza Kwanini hujaenda shule, Akasema shule aliyopangiwa wameuza jina lake, Alipoenda kuripoti aliambiwa nafasi yake haipo. [emoji3064][emoji3064][emoji3064]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu kama hicho, uuze jina la mtu ili iweje!?,acheni kutupanda kichwani,cheti cha form 4 kina picha na sura ya mhusikae,huyo aliyenunua jina atapata wapi cheti cha form four baada ya kuhitimu form six!?
Hili nalo neno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…