Kilio cha Walima Vanilla Kagera kwenda kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Kilio cha Walima Vanilla Kagera kwenda kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Magendo ukirisk lazima utoboe
Tushawaona wangapi wakifanya hiyo
Kuna watu tunawafaham walifanya magendo wakapiga hela hadi sahv wameingia kwenye siasa wnaitwa waheshimiwa
Hii dunia uwanja wa fujo ukifanya kufata mstari hutoboi,utabakia msindikizaji tu kuwatajirisha wengine

Ova
Kabisa bila kubadilisha mbinu za kivita watakuwa wanawanufaisha wajinga wachache
 
Huyu alikuwa tapeli. Ameiba fedha za watu akajifarikisha na kupotea ktk dunia ya Njombe.
Mbona yupo zanzibar anawapiga kwa kuwajengesha greenhouse na wanatumia gharama kubwa sana. Pence kutumia million 2 zinatumika kumi na miche inadumu muda mfupi. Mimi nina technology ya kuishi miaka 20
 
Aliyekaribu na Rais atusaidie. Mh. Bashe alikuja kwenye mkutano wa kuiinua Kagera baada ya hotuba yake, akapiga picha na viongozi kadhaa akaondoka. Hakuuliza wajumbe baadhi ya mambo ambayo yanakwamisha mkoa huu. Watu walikuwa wamejiandaa kuongelea mambo mengi lakini hatukupata muda. Ndio maana vilio vyetu havikupata kumfikia Waziri wa Kilimo wala rais.
 
Hizo bei za 32000,30000,50000 ni za nn katuwekea

Ova
30,000-32,000 ndo zilizokua zinanunuliwa na huyo mayawa akafanya manouver bei ikawa 20,000 kwa kg ila Uganda wao wananunua 1 KG 50,000 tshs ila kuna wale jamaa wa Njombe wao wananunua 1 KG 1,000,000 aisee bi mkubwa wangu alinipigia simu ananiambia habari hii ya 1 KG 1m...nikamwambia mama hakuna hela rahisi duniani kama unataka utapeliwe nenda kawekeze kwenye mashamba ya vabilla huko...😀😀😀
 
Bora wewe unaielewa thamani yake Halafu kuna mdau anasema eti hadi ifike ubora wa milioni unafikiri ni rahisi?

Yaani anafikiri sijui ni kama Ng’ombe [emoji23]
Nilishakwendaga huko nilifanya research kubwa tu,kama kawaida sisi wengine ni wazee wa kuingia chimbo
Siyo mtu anakaa kufanya research mtandaoni tu shamba,maeneo hayajui

Ova
 
Hacha ukabira nyau ww,ww angalia dhumuni la kuandika Uzi wake humu,anyooshe maandishi kwani yeye anafanya kazi BAKITA?
Mwambie mwambie mkulima anajua jembe trekta na magunia ya kujaza mavuno kwenda kwa wachuuzi tu. Lugha aende BaKITA
 
Hacha ukabira nyau ww,ww angalia dhumuni la kuandika Uzi wake humu,anyooshe maandishi kwani yeye anafanya kazi BAKITA?
Wahaya wanajibu tu. 😁😁 poleni wakulima wa vanila bei elekezi ni mil.1 kwa kilo from vanila village.
 
Kwako Rais Wetu Mpenda.

Nianze kwa kukupa pole na majukumu yako ya kila siku, pia nikushukru jinsi unavyoongoza nchi kwa amani na utulivu. Bila kuacha kukupongeza kwa unavyopambana na miradi ya kimikakati katika kuiinua nchi kuelekea uchumi wa kati.

Sisi wakulima wa vanilla Kagera tumekumbwa na tatizo kubwa sana ambalo limeleta mgogoro sana na mgongano ya masilahi. Wakulima wakagera tuliitwa tarehe 20 Mei 2022 kujadiri mstakabari wa Vanila zetu.

Waliohudhuria ni sisi wakulima pamoja na kampuni zinazonunua vanila. Pamoja na katibu tawala wa mkoa. Kikao kiliisha salama licha ya kuwa na marumbano makali juu ya uhuni unaofanywa na mkurugenzi wa MAYAWA ambao ndio wanunuzi wakuu.

Iko hivi: Mkurugenzi wa Mayawa anatuhumiwa kula njama na kuwashawishi makampuni anayoshindana nayo kutozidi kiwango fulani ili wapate faida kubwa.

Mayawa kwa kutumia makampuni mengine madogo alifanikiwa kushusha bei kilo moja kutoka tshs 32,000/= to tshs 20,000/= wakati yeye akinunua kwa tshs 30,000. Mayawa ilizidiwa wingi wa vanila ikabidi ikope Bank kutoa ADB kulipa wakulima.

Lakini bado wakulima wanadai mil. Mia mbili. Mpaka sasa ajawalipa licha ya kuambiwa na mkuu wa mkoa kwa kauli ya serikali kuwa tarehe 31 May 2022 awe amewalipa. Sasa likichofanyika ni kwamba mayawa amesusa kununua na kushawishi kampuni nyanza zilizokuwa zinanunua kwa bei nafuu nazo zikasusa.

Sasa hivi ni kampuni moja tu NEI LTD kutoka Moshi Makao Makuu ndiyo inayonunua. Kampuni hiyo nayo imezidiwa na imesitisha kwa muda. Wakulima wa sasa hawajui cha kufanya vanila mashambani zimeanza kuharibika.

Tunaiomba serikali kupitia takukuru wachunguze hii kampuni ya mayawa alafu wamuombe NEILTD aendelee kununua vanila zetu tusije kukata tamaa. Kama ikishindikana tunaomba tufunguliwe mipaka tuize Uganda kwani wao wananunua kilo moja kwa tshs 50,000/= vanila mbichi.

Mkoa wa Kagera mwaka huu unazalisha tani mia 4 jambo ambalo watunza takwimu hawana, kwa kuwa nyingi zinatoroshewa nchi za jirani kukwepa mitego ya kampuni zetu za kijanja janja. Pia kampuni kwa sasa hazifuati wakulima kwenye vituo. Hii inatokea kwa sababu ya kukwepa ushuru.

Mwaka jana tu serikali ilikuwa inadai makampuni manne tshs miliioni 20. Kama ushuru hivyo kuitisha kuwapelekea ni njia mojawapo ya kukwepa ushuru.
Mwisho nakuomba umwagize waziri wako kilimo Bashe pamoja na Katibu wake waende kuhitisha kikao cha dharura wawasikilize wakulima wanasemaje kuhusu mambo mabaya wanayotendewa kwenye hii dhahabu ya kijani.

Wako mkulima wa Vanilla Bukoba
20000 bado unapiga kelele tu du Wahaya bhana!
 
Wahaya aka Nshomile akili nyingi ila maarifa 10%! Ngoja niwape mbinu ambazo wenzenu Moshi wanazidi kutajirika kwa kupeleka Mahindi, Kahawa, Tanzanite nk hapo jirani Kenya.
Kuishi mpakani ni fursa ya kipekee, Lukunyu, Mashanga(Bugabo) ni nchi jirani hiyo hakuna janja janja ya akina Bashe! au nimwambie na njia ya kufika hapo bila kukamatwa? Njoo inbox!
CCM elabakozile bintungwa, nimwija kufa ne'enaku kamutashazile agalabayamba!
Mhaya kiukweli anatambwe hiza wengi sana kuliko uhalisia wa maisha anayoishi.
Nimefanyia kazi huko na mambo ya ajabu nimejionea mengi!
Watu wa mpakani wapo tayari kununua redio kwa upande wa Tz kuliko ile iliyovushwa(Uganda vitu vingi vipo chini).
Hii yote eti asionekane mtu wa dili!
Saa nyingine baadhi(hasa wakuja) hujitahidi kuvusha vitu lakini hawewezi kudumu muda wanakamatwa kisa kuna wajuaji huwachongea kwa wenye mamlaka na wenye mamlaka wakipata dili kama hizo,mizigo hutaifishwa na isijulikane imeenda wapi.
Mnanuksi sana ukijumlisha na lichama lenu acha muonje joto la Tanzania akili itawanyooka!
 
Kwako Rais Wetu Mpenda.

Nianze kwa kukupa pole na majukumu yako ya kila siku, pia nikushukru jinsi unavyoongoza nchi kwa amani na utulivu. Bila kuacha kukupongeza kwa unavyopambana na miradi ya kimikakati katika kuiinua nchi kuelekea uchumi wa kati.

Sisi wakulima wa vanilla Kagera tumekumbwa na tatizo kubwa sana ambalo limeleta mgogoro sana na mgongano ya masilahi. Wakulima wakagera tuliitwa tarehe 20 Mei 2022 kujadiri mstakabari wa Vanila zetu.

Waliohudhuria ni sisi wakulima pamoja na kampuni zinazonunua vanila. Pamoja na katibu tawala wa mkoa. Kikao kiliisha salama licha ya kuwa na marumbano makali juu ya uhuni unaofanywa na mkurugenzi wa MAYAWA ambao ndio wanunuzi wakuu.

Iko hivi: Mkurugenzi wa Mayawa anatuhumiwa kula njama na kuwashawishi makampuni anayoshindana nayo kutozidi kiwango fulani ili wapate faida kubwa.

Mayawa kwa kutumia makampuni mengine madogo alifanikiwa kushusha bei kilo moja kutoka tshs 32,000/= to tshs 20,000/= wakati yeye akinunua kwa tshs 30,000. Mayawa ilizidiwa wingi wa vanila ikabidi ikope Bank kutoa ADB kulipa wakulima.

Lakini bado wakulima wanadai mil. Mia mbili. Mpaka sasa ajawalipa licha ya kuambiwa na mkuu wa mkoa kwa kauli ya serikali kuwa tarehe 31 May 2022 awe amewalipa. Sasa likichofanyika ni kwamba mayawa amesusa kununua na kushawishi kampuni nyanza zilizokuwa zinanunua kwa bei nafuu nazo zikasusa.

Sasa hivi ni kampuni moja tu NEI LTD kutoka Moshi Makao Makuu ndiyo inayonunua. Kampuni hiyo nayo imezidiwa na imesitisha kwa muda. Wakulima wa sasa hawajui cha kufanya vanila mashambani zimeanza kuharibika.

Tunaiomba serikali kupitia takukuru wachunguze hii kampuni ya mayawa alafu wamuombe NEILTD aendelee kununua vanila zetu tusije kukata tamaa. Kama ikishindikana tunaomba tufunguliwe mipaka tuize Uganda kwani wao wananunua kilo moja kwa tshs 50,000/= vanila mbichi.

Mkoa wa Kagera mwaka huu unazalisha tani mia 4 jambo ambalo watunza takwimu hawana, kwa kuwa nyingi zinatoroshewa nchi za jirani kukwepa mitego ya kampuni zetu za kijanja janja. Pia kampuni kwa sasa hazifuati wakulima kwenye vituo. Hii inatokea kwa sababu ya kukwepa ushuru.

Mwaka jana tu serikali ilikuwa inadai makampuni manne tshs miliioni 20. Kama ushuru hivyo kuitisha kuwapelekea ni njia mojawapo ya kukwepa ushuru.
Mwisho nakuomba umwagize waziri wako kilimo Bashe pamoja na Katibu wake waende kuhitisha kikao cha dharura wawasikilize wakulima wanasemaje kuhusu mambo mabaya wanayotendewa kwenye hii dhahabu ya kijani.

Wako mkulima wa Vanilla Bukoba
Si nilisikia bei ya Vanila kilo 1 ni milioni moja au siyo nyie?
 
Inawezekana...

Maana wilaya ya misenyi na bukoba vijijini kilimo hiki kimeshamiri kweli

Lakin tatizo ni kwamba mauzo hayaonekani na wala faida kwa mkoa haionekani..

Bado kahawa na ndizi...lakin kimapata mkoa haupati kitu mpaka unakuwa wa mwisho kuchangia pato la taifa Tz nzima
Hii siyo Kweli , napinga nani tazidi kupinga. hakuna ton 400 labda kama ni 40, Nazo Sina Imani kama zinafika.
 
Bora wewe unaielewa thamani yake Halafu kuna mdau anasema eti hadi ifike ubora wa milioni unafikiri ni rahisi?

Yaani anafikiri sijui ni kama Ng’ombe [emoji23]
Kiukweli hiyo mdau unaweza kumshangaa, lakini Khali ilivyo kwa kagera ningumu kupata ubora unao kizi viwango vya ubora.

Kwanini nasema hivyo.

Baada ya kujitokeza waranguzi kutoka nchi jirani , kuliibuka wimbi la wizi wa Vanilla mashambani.

Wezi hao hawajui kama imekomaa au haijakomaa wao wanacho jua ni kuiba TU wakati mwingine hung'oa hata miche, matunda watachambulia mbali.

Ili kukabiliana na hiyo Khali ulibuniwa mfumo wa mauzo kwa minada.

Minada inaendeshwa huko vijijini kwa wakulima.

Siku ya kuchuma inakua moja nasiku hiyohiyo wanauza.

Mfumo huu hautoi nafasi yakuchuma kwa kufuata matunda yaliyo iva tu, bali ni kuchuma yote ,kwa sababu ni siku ya kuuza.
 
Back
Top Bottom