Kilio cha Walima Vanilla Kagera kwenda kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Kilio cha Walima Vanilla Kagera kwenda kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Kavurugwa, anyooshe maelezo, hio bei ni kwa kilo moja au gramu moja,
Kuna yule tapeli alietangaza ananunua milion moja kwa kilo sijui hazihitaji hizo,
Hizi Bei ni kwa , 1kg ya vanilla mbichi.
Hao wa Njombe "vanilla village" hawanunui Wala hawauzi.

Wanacho hubili ni kukuendesha kilimo kwenye Kijiji Chao.

Utapewa eneo la,,m5×m7 bila tozo

Utalipia 5,000,000 tsh zakuweka miundombinu, green house, drip irrigation, na kupandikiza Miche, baada ya hapo Kuna gharama za uendeshaji.
Ulifika msim wa kuvuna watakuunganisha na masoko.
 
Huyu jamaa anawapiga sana wazanzibar na anapewa hela na serikali. Lakini hakuna bei hizo. Vanila iliyokaushwa huuzwa laki sita tu na lazima ipitie vipimo vya ubora.
Kama Kuna soko la Tsh 600,000/kg1, kwanini isikaushwe?
 
Tatizo Kagera huwa wanaimani kubwa sana(hadi kupitiliza) juu ya viongozi wa CCM.Hili limewaganda sana vichwani mpaka hawaoni dhuluma.
Saa nyingine nashindwa kuwaonea huruma!
Sio Kweli.

Niwapenda mageuzi sematu, mageuzi hayawapendi.
 
Kwa mtazamo wangu nlichokiona
Hapo kuna style ya kuwachosha jamaa wa vanilla ili watu fulani
Wainunue alafu wao ndy wakauze bei juu.....
Hi8 kitu ipo sana tanzania,nchi kuna watu hawapendi kuona watu wanapata hela

Ova
Kimsingi ubinafsi umekomaa Tz...

Watu ni wabinafsi kupitiliza..

Hadi kwenye ajira..Bosi analipwa 30m huku wafanyakazi na vibarua laki mbili...
Yan watu hawapendi watu wafurahi na kupata hela
 
Kwako Rais Wetu Mpenda.

Nianze kwa kukupa pole na majukumu yako ya kila siku, pia nikushukru jinsi unavyoongoza nchi kwa amani na utulivu. Bila kuacha kukupongeza kwa unavyopambana na miradi ya kimikakati katika kuiinua nchi kuelekea uchumi wa kati.

Sisi wakulima wa vanilla Kagera tumekumbwa na tatizo kubwa sana ambalo limeleta mgogoro sana na mgongano ya masilahi. Wakulima wakagera tuliitwa tarehe 20 Mei 2022 kujadiri mstakabari wa Vanila zetu.

Waliohudhuria ni sisi wakulima pamoja na kampuni zinazonunua vanila. Pamoja na katibu tawala wa mkoa. Kikao kiliisha salama licha ya kuwa na marumbano makali juu ya uhuni unaofanywa na mkurugenzi wa MAYAWA ambao ndio wanunuzi wakuu.

Iko hivi: Mkurugenzi wa Mayawa anatuhumiwa kula njama na kuwashawishi makampuni anayoshindana nayo kutozidi kiwango fulani ili wapate faida kubwa.

Mayawa kwa kutumia makampuni mengine madogo alifanikiwa kushusha bei kilo moja kutoka tshs 32,000/= to tshs 20,000/= wakati yeye akinunua kwa tshs 30,000. Mayawa ilizidiwa wingi wa vanila ikabidi ikope Bank kutoa ADB kulipa wakulima.

Lakini bado wakulima wanadai mil. Mia mbili. Mpaka sasa ajawalipa licha ya kuambiwa na mkuu wa mkoa kwa kauli ya serikali kuwa tarehe 31 May 2022 awe amewalipa. Sasa likichofanyika ni kwamba mayawa amesusa kununua na kushawishi kampuni nyanza zilizokuwa zinanunua kwa bei nafuu nazo zikasusa.

Sasa hivi ni kampuni moja tu NEI LTD kutoka Moshi Makao Makuu ndiyo inayonunua. Kampuni hiyo nayo imezidiwa na imesitisha kwa muda. Wakulima wa sasa hawajui cha kufanya vanila mashambani zimeanza kuharibika.

Tunaiomba serikali kupitia takukuru wachunguze hii kampuni ya mayawa alafu wamuombe NEILTD aendelee kununua vanila zetu tusije kukata tamaa. Kama ikishindikana tunaomba tufunguliwe mipaka tuize Uganda kwani wao wananunua kilo moja kwa tshs 50,000/= vanila mbichi.

Mkoa wa Kagera mwaka huu unazalisha tani mia 4 jambo ambalo watunza takwimu hawana, kwa kuwa nyingi zinatoroshewa nchi za jirani kukwepa mitego ya kampuni zetu za kijanja janja. Pia kampuni kwa sasa hazifuati wakulima kwenye vituo. Hii inatokea kwa sababu ya kukwepa ushuru.

Mwaka jana tu serikali ilikuwa inadai makampuni manne tshs miliioni 20. Kama ushuru hivyo kuitisha kuwapelekea ni njia mojawapo ya kukwepa ushuru.
Mwisho nakuomba umwagize waziri wako kilimo Bashe pamoja na Katibu wake waende kuhitisha kikao cha dharura wawasikilize wakulima wanasemaje kuhusu mambo mabaya wanayotendewa kwenye hii dhahabu ya kijani.

Wako mkulima wa Vanilla Bukoba
Kuna mtu anatangaza vanilla huko Njombe anasema kilo moja wanauza Tsh 800,000. Na anataka watu waende wakalime huko kwa kukodi mashamba. Je vanilla ya Njombe Ina nini cha zaidi hadi iuzwe ghali hivyo?
 
Hii Vanila ndio nilisikia mahala kilo moja Tsh milioni moja!

Au nilikuwa naota huku natembea juani!
Uzi huu hapa unaoungelea hiyo bei ya Tsh 1 Million kwa kilo:

Tunataka katiba mpya ipatikane KWANZA itatoa ulinzi KWA mkulima na sio kumlilia Rais KWA changamoto zao!

Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA!
 
Wale jamaa wa vanilla kilo moja uuzwa milioni moja nyuzi kama hizi awazipendagi
 
Tani 400 ???
Inawezekana...

Maana wilaya ya misenyi na bukoba vijijini kilimo hiki kimeshamiri kweli

Lakin tatizo ni kwamba mauzo hayaonekani na wala faida kwa mkoa haionekani..

Bado kahawa na ndizi...lakin kimapata mkoa haupati kitu mpaka unakuwa wa mwisho kuchangia pato la taifa Tz nzima
 
Kwako Rais Wetu Mpenda.

Nianze kwa kukupa pole na majukumu yako ya kila siku, pia nikushukru jinsi unavyoongoza nchi kwa amani na utulivu. Bila kuacha kukupongeza kwa unavyopambana na miradi ya kimikakati katika kuiinua nchi kuelekea uchumi wa kati.

Sisi wakulima wa vanilla Kagera tumekumbwa na tatizo kubwa sana ambalo limeleta mgogoro sana na mgongano ya masilahi. Wakulima wakagera tuliitwa tarehe 20 Mei 2022 kujadiri mstakabari wa Vanila zetu.

Waliohudhuria ni sisi wakulima pamoja na kampuni zinazonunua vanila. Pamoja na katibu tawala wa mkoa. Kikao kiliisha salama licha ya kuwa na marumbano makali juu ya uhuni unaofanywa na mkurugenzi wa MAYAWA ambao ndio wanunuzi wakuu.

Iko hivi: Mkurugenzi wa Mayawa anatuhumiwa kula njama na kuwashawishi makampuni anayoshindana nayo kutozidi kiwango fulani ili wapate faida kubwa.

Mayawa kwa kutumia makampuni mengine madogo alifanikiwa kushusha bei kilo moja kutoka tshs 32,000/= to tshs 20,000/= wakati yeye akinunua kwa tshs 30,000. Mayawa ilizidiwa wingi wa vanila ikabidi ikope Bank kutoa ADB kulipa wakulima.

Lakini bado wakulima wanadai mil. Mia mbili. Mpaka sasa ajawalipa licha ya kuambiwa na mkuu wa mkoa kwa kauli ya serikali kuwa tarehe 31 May 2022 awe amewalipa. Sasa likichofanyika ni kwamba mayawa amesusa kununua na kushawishi kampuni nyanza zilizokuwa zinanunua kwa bei nafuu nazo zikasusa.

Sasa hivi ni kampuni moja tu NEI LTD kutoka Moshi Makao Makuu ndiyo inayonunua. Kampuni hiyo nayo imezidiwa na imesitisha kwa muda. Wakulima wa sasa hawajui cha kufanya vanila mashambani zimeanza kuharibika.

Tunaiomba serikali kupitia takukuru wachunguze hii kampuni ya mayawa alafu wamuombe NEILTD aendelee kununua vanila zetu tusije kukata tamaa. Kama ikishindikana tunaomba tufunguliwe mipaka tuize Uganda kwani wao wananunua kilo moja kwa tshs 50,000/= vanila mbichi.

Mkoa wa Kagera mwaka huu unazalisha tani mia 4 jambo ambalo watunza takwimu hawana, kwa kuwa nyingi zinatoroshewa nchi za jirani kukwepa mitego ya kampuni zetu za kijanja janja. Pia kampuni kwa sasa hazifuati wakulima kwenye vituo. Hii inatokea kwa sababu ya kukwepa ushuru.

Mwaka jana tu serikali ilikuwa inadai makampuni manne tshs miliioni 20. Kama ushuru hivyo kuitisha kuwapelekea ni njia mojawapo ya kukwepa ushuru.
Mwisho nakuomba umwagize waziri wako kilimo Bashe pamoja na Katibu wake waende kuhitisha kikao cha dharura wawasikilize wakulima wanasemaje kuhusu mambo mabaya wanayotendewa kwenye hii dhahabu ya kijani.

Wako mkulima wa Vanilla Bukoba
Andiko lako limejaa uongo mwingi eidha kwa makusudi au kwa kutokujua. Natamani ningekujibu hapa ukaona ulivyoandika upupu mwingi.
 
Hadi ifikie huo ubora wa mil 1 unafikiri ni rahisi? Au unahisi kila vanilla inanunuliwa hivyo?

Kwanini isifike ubora huo?
Mbona mnajishusha sana ?
Kwani wanaofikisha ubora huo wamechaguliwa wawe wao tu?

Kwa majibu Haya mtabaki nyuma kila sekta
Sio kuwa nahisi na hakuna hisia bali uhalisia naujua kwa sababu nanunua toka Madagascar na hapa nilipo pia na ninayengeneza faida kiasi changu

Hebu nijibu kama wewe ni mkulima au unajibu kwa hisia na wewe
 
Bei nnayoijua hata mm kwa hapa 600,000 sema kna wakat ilipanda mpaka 800,000
Muheza napo si kuna watu wanapanda hii

Ova

Bei nnayoijua hata mm kwa hapa 600,000 sema kna wakat ilipanda mpaka 800,000
Muheza napo si kuna watu wanapanda hii

Ova

Bora wewe unaielewa thamani yake Halafu kuna mdau anasema eti hadi ifike ubora wa milioni unafikiri ni rahisi?

Yaani anafikiri sijui ni kama Ng’ombe [emoji23]
 
Bora wewe unaielewa thamani yake Halafu kuna mdau anasema eti hadi ifike ubora wa milioni unafikiri ni rahisi?

Yaani anafikiri sijui ni kama Ng’ombe [emoji23]
Unapenda kusikia uongo?? Ingekua na hiyo thamani hao wakulima wangekua mamilionea
 
Ni yaleyale ya kuhamasisha watu wafuge sungura wakati soko hakuna. Vanilla nayo walihamasisha na kushawishi wakulima na bei kuwa kilo ni 1,000,000
 
usijibu ilimradi tu.Kama haiingilii soko mbona inazuia kuuza Uganda?
Kabla ya vanila kuwa zao kuu tulikuwa tunakausha tunauza Uganda. Serikali ilikuwa haijui zao hili. Baada ya kuijua sasa maumivu vitisho vikaanza. Mayawa nao wakaitumia serikali kunyonya wananchi kwa kuzuia vanilla isiuzwe Uganda.
 
Back
Top Bottom