Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,391
JOBO which is whichJobu'
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
JOBO which is whichJobu'
Kwa ilani inasemaje?Huku athari za Kimbunga hicho 'Jobu' zikiwa zimeanza huko Mkoani Mbeya kwa Mvua Kubwa na yenye Upepo Mkali kunyesha mpaka Kuharibu barabara kwa 'Kuitenganisha' na nchi ya Malawi.
Akiongea na BBC Dira ya Dunia muda si mrefu Afisa wa Kituo cha Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Ndugu Samuel Mbuya aliyekuwa akizungumza na Mtangazaji Regina Mziwanda kasema Siku ya Jumapili tutegemee 'Maafa' makubwa Mikoa ya Dar es Salaam na Mafia japo Mikoa ya Mtwara na Lindi pia wanaweza Kukumbana nayo.
Ndugu Samuel Mbuya amesema hivi sasa Kimbunga hicho kipo umbali wa Kilimeta 236 kutokea Mafia na kwamba Siku ya Jumapili ndiyo 'Kitapiga' rasmi Mkoani Dar es Salaam kikiambatana na Mvua Kubwa sana na Upepo Mkali mno.
Taarifa ambazo Generalist nimezipata hivi punde tu ni kwamba tayari Balozi kadhaa nchini Tanzania zimewaonya Wafanyakazi wako kuchukua 'Tahadhari' zote cha Kimbunga hicho 'Jobu' ambacho hakijawahi kutokea nchini Tanzania ndani ya miaka 70.
Haya kila mwana JF achukue tahadhari.
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA yatoa tahadharisha kwa watanzania wote kwa uwezekano wa kimbunga jobo kuwepo Tanzania.
TMA imewataka wananchi kujihadhari na uwezekano wa kimbunga jobo kuanzia April 24 mwaka huu kupiga Tanzani hasa katika mikoa ya pwani.
Wameskia imeripotiwa CNN wakaona nawao watie chumviSawa kama TMA ndio wametoa hiyo taarifa basi haina mashiko maana mitambo yao ni ya kubahatisha kwa kiwango kikubwa tu.
Wameskia imeripotiwa CNN wakaona nawao watie chumvi
Ndo nchi yetu hii yaani haieleweki hatariHahahaa Wamekipa promo sana wakati hakitoleta madhara yeyote ni sawa na upepo mwingine tu.
Salini kama mlivyofanya kwenye Covid-19.Utabiri wa hewa umebaini kuwa kuna tropical cyclone storm iliyoitwa jina la Jobo inayoelekea pwani ya Dar es Salaam na Zanzibar. Kimbunga hiki sasa hivi kiko Madagascar na inakadiriwa kufika Tanzania jumapili tarehe 25 April 2021 kwa utabiri wa watalaamu wa hali ya hewa.
Jee wananchi wa Dar es Salaam na Zanzibar wameandaliwa ya kutosha ikiwa kweli gharika hili kama litatokea? Madhara ambayo yanaweza kusababishwa na ghalika la kimbunga hiki ni pamoja na:
1. Kukosekana kwa umeme kwa kipindi kirefu.
2. Kukosekana kwa huduma mhimu kwa sababu ya mafuriko na mvua kubwa. Chakula sokoni hakitapatikana au hakitafikika. Simu zitaishiwa chaji. Mafuta ya magari hayatapatikana au kufikika. Gesi ya kupikia chakula haitapatikana au kufikika. Vituo vya matibabu havitafikika. Njia za kupata habari kama TV na redio zinaweza kuwa za shida na kadhalika.
3. Wananchi kujeruhiwa au kupoteza maisha.
4. Wananchi kukosa makazi kutokana na nyumba kuezuliwa paa au kubomoka na kusombwa na mafuriko ya mvua kubwa na bahari kufurika.
Tumuombe Mwenyezi Mungu atuepushe na kimbunga hiki kama alivyotuepusha na kile cha Msumbiji mwaka jana.
Wanasindwa na wenye na Bar at least wanawaandaa wateja waoUtabiri wa hewa umebaini kuwa kuna tropical cyclone storm iliyoitwa jina la Jobo inayoelekea pwani ya Dar es Salaam na Zanzibar. Kimbunga hiki sasa hivi kiko Madagascar na inakadiriwa kufika Tanzania jumapili tarehe 25 April 2021 kwa utabiri wa watalaamu wa hali ya hewa.
Jee wananchi wa Dar es Salaam na Zanzibar wameandaliwa ya kutosha ikiwa kweli gharika hili kama litatokea? Madhara ambayo yanaweza kusababishwa na ghalika la kimbunga hiki ni pamoja na:
1. Kukosekana kwa umeme kwa kipindi kirefu.
2. Kukosekana kwa huduma mhimu kwa sababu ya mafuriko na mvua kubwa. Chakula sokoni hakitapatikana au hakitafikika. Simu zitaishiwa chaji. Mafuta ya magari hayatapatikana au kufikika. Gesi ya kupikia chakula haitapatikana au kufikika. Vituo vya matibabu havitafikika. Njia za kupata habari kama TV na redio zinaweza kuwa za shida na kadhalika.
3. Wananchi kujeruhiwa au kupoteza maisha.
4. Wananchi kukosa makazi kutokana na nyumba kuezuliwa paa au kubomoka na kusombwa na mafuriko ya mvua kubwa na bahari kufurika.
Tumuombe Mwenyezi Mungu atuepushe na kimbunga hiki kama alivyotuepusha na kile cha Msumbiji mwaka jana.
Yaani ubongo unatetemekaMamlaka za hali ya hewa zimeendelea kutaka wananchi wachukue tahadhari dhidi ya kimbunga JOBO ambacho kwa sasa kipo umbali usiozidi km 400 kutoka mwambao wa Bahari ya Hindi.
Kamisheni ya Maafa Zanzibar imetoa tahadhari kwa wavuvi na wamiliki wa vyombo vya usafiri baharini kutokana na uwepo wa kimbunga hicho.
Kamisheni ya Maafa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) wanaendelea kufuatilia kimbunga na wataendelea kutoa taarifa.
Kwa jinsi kinavyoelezewa kuwa Kimbunga Jobo kitakuja kuna Uwezekano kikaleta MAAFA makubwa mno ya Vifo, Uharibifu na mengineyo hivyo basi Serikali ili Kurejesha hali ya Kawaida kutokana na Uharibifu huo itabidi iachane na Mpango wa Kuwaongeza Mishahara Watumishi wake kwa mwaka labda mpaka mwakani au hata baada ya 2025.Jamani,hiki kimbunga si kije baada ya Mei mosi? Mbona kinataka kumfanya Samia S.H asitamke yale 'mema' ambayo watumishi wanayasubiri kitambo?
Tena ndiyo huenda 'Kitatuua' sana Wakazi wa Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Kisiwa cha Mafia kuliko hata wale 'Waliofariki' kwa Ugonjwa wa Corona ( Covid-19 )Mkuu usitutishe, cha kwetu hakitakua na kasi iyo, japo tunapaswa kuchukua tahadhari.
Kuondoka kwa AMRI ya Israeli kwa Hayati Rais Dkt. Magufuli na kuja kwa Rais Samia ni sawa sawa tumetolewa ICU sasa tunapelekwa Mochwari.Kimbunga(Hurricane)Jobo kinatokea Madagascar na kitapiga hodi maeneo ya Pwani ya Zanzibar na Daresalaam.Hiyo ni kudra ya Mwenyezi Mungu.Isitoshe ni kutokana na Tabia Nchi (Climate Change).Hao wendawazimu wanaodai kuna mtu kapatia kuhamia Dodoma hajui lolote.Hii Tabia nchi pia inaleta ukame wa ajabu.Ndani ya miaka michache Huko makao makuu kutatokea Ukame ambao haujawahi kutokea nchini,na Ardhi yake kugeuka Jangwa.Viongozi Duniani wanajadiliana kuhusu suala hilo.Sijui kiongozi gani anatuwakilisha.Its very Important.
Na jinsi walivyo Waoga na wanavyotaka Sifa huenda Kesho tarehe 25 April, 2021 Siku ya kutokea Kimbunga Jobo chenyewe wakatukatia 'Umeme' hadi tarehe 25 December, 2021.Kama nawaona Tanesco watavyo kata umeme kabla hata hilo bogi halijatua...
Mwaisela na Kibasila zote ni Muhimbili.JOBO which is which