Kinachoendelea Kigoma kuibua wachawi ni udhalilishaji, upuuzi na uchonganishi

Viongozi wote wa kigoma hawalioni hili ?

Tusema viongozi wa CC wamelipitisha, mtu unalazishwa kutoa afu5 na fimbo juu . Asee [emoji119]
Huyo muweka uzi ni muongo. Mtu halazimishwi kutoa fedha. Fedha zinachangwa kwa hiari. Na fedha hizo ni kwaajili ya wanaowasaidia hao wataalamu kufanya shughuli yao. Hao wataalamu hawachukui hata mia mbovu.
 
Wanakijiji wa Kigoma Wana maoni gani? Ikipigwa kura ya maoni Huko Kigoma.

Kwamba kamchape wake au wasije?

Wananchi wengi watakuwa upande gani? Unavyohisi wewe
Wananchi ndio wanawachangia hawa jamaa kwa hiari yao. Hakuna analazimishwa na fedha hizo ni kwaajili ya wanaowasaidia hao wataalamu kufanya shughuli yao. Hao wataalamu hawachukui hata mia mbovu.
 
Tulia wakimaliza Kigoma wataenda mikoa mingine.
Haya ni mambo ya kiroho zaidi Sio kimwili,wewe kama sio mchawi unaumia Nini.
Acha hao wapumbavu waadabishwe
 
Kama wanatoa kwa hiari Yao shida nini,mbona watu wanatoa kanisan kwa hiari
 
Kigoma wananchi wapinga agizo la DC wataka uchawi ukomeshwe.

Hiinili niliona kwenye taarifa ya habari, azamu tv, wananchi wakiandamana kumpinga DC kukataza watu wanaojifanya wanatoa uchawi, muda mwingine wananchi tunawaingiza viongozi kwenye moto, hebu nenda you tube, andika maneno ya hapo juu, uone juhudi za DC kuxuzuia hii.
 
Wanakijiji wa Kigoma Wana maoni gani? Ikipigwa kura ya maoni Huko Kigoma.

Kwamba kamchape wake au wasije?

Wananchi wengi watakuwa upande gani? Unavyohisi wewe
Wengi Wana unga mkono wachapwe
 
Huyo mganga si ayatume majini yake yaende Benki yeyote ya karibu yakachukue hela kuliko kuanza kuchangisha wananchi ambao ni choka mbaya?
 
Haya mambo si ndiyo yalimfanya Ali Hassan Mwinyi mpaka ajiuzulu u Waziri wa Mambo ya Ndani?

Waziri wa sasa naye anafanya nini? Polisi wanafanya kazi gani huko?
 
Huyo mganga si ayatume majini yake yaende Benki yeyote ya karibu yakachukue hela kuliko kuanza kuchangisha wananchi ambao ni choka mbaya?
Bank zote freemason wamezindika hakuna jini Wala mchawi anaweza chukua Hela bank.
Hata mchawi tu ndani achukui Hela akichukua tu hawezi toka ndani ya nyumba anakuwa amekiuka kanuni
 
Kuna mama mmoja mtu mzima mwenye umri mkubwa kuweza kuitwa bibi alichanjwa chale kwa lazima eti uchawi wake ukose nguvu akitaka kuloga. Mama wa watu alivuja damu njingi. Ilikuwa kila nyumba wakipita zingine wanasema hakuna uchawi na zingine wanasema kuna uchawi, wanafukua sehemu fulani ya nyumba wanaibuka na kitu kama pembe ya myama wanasema ni uchawi, mwenye nyumba anakamatwa na kuchanjwa chale kwa lazima
 

Kwa akili hizi Bora bandari iuzwe tu. Bado mpo zama za ujima
 
Mheshimiwa Makamu bila shaka anayajua yanayoendelea huko kwake, atarekebisha.
 
Hivi hii kisheria imekaaje??? Serikali inaruhusu hii kitu kweli??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…