Mkuu nimeshawahi kukaa Kasulu mwezi 1 Kikazi, sasa nalala Kasulu, shughuri zangu nafanyia Vijijini, kuna siku nikawa na Mwenyeji tukatembea kwenye Kijiji kimoja.... Nakuta Nyumba zisizoisha, Maghofu, ila ukiangalia unaona House plan ya kimjini kabisa, namuuliza mwenyeji wangu, mbona hiki Kijiji watu hawamalizii Nyumba zao..!!
Akaanza kunionyesha kila Ghofu la Nyumba, unaona lile Ghofu pale, mwenyewe alikua anaishi Dar, akapata pesa akaja kujenga kwao, Nyumba ilipofikia vile akaumwa Ghafla akafa.....
Unaona lile Ghofu paleee, mwenyewe alikua kijana tu akiishi Mwanza, akarudi kijijini kuja kujjenga, nyumba haijaisha akafa, Wastani wa Nyumba 10 hivi, zote Vijana walikufa walipoenda tu kijijini kwao kujenga....!
Watu wa Kigoma wanajua wanachokifanya, wanajua matatizo yao, na ubaya nj kwamba Kesi ya Uchawi huwezi kwenda kushtaki Police!
Wacha wa deal nao kwa namna yao.