Kinachoendelea Kigoma kuibua wachawi ni udhalilishaji, upuuzi na uchonganishi

Kinachoendelea Kigoma kuibua wachawi ni udhalilishaji, upuuzi na uchonganishi

Usikie tu uchawi na wachawi, hawafai kutengamana na jamii. Hukumu ya mchawi ni kuuwawa. Hawa ndiyo visababishi vya umasikini. Utakuta wanaroga watoto wanashindwa kwenda shule. Wachawi wanakwamisha maendeleo ya watu. Kwa maoni yangu washughulikiwe kwa nguvu ili waache uchawi. KAMCHAPE OYEE
Witch hunt/ witch purge ni mambo yaliyofanyika ulaya zama za giza, miaka ya 500-1500.
 
Kwenye umaskini mwingi, magonjwa, vifo vya kutatanisha, umri mdogo wa kuishi na matatizo mengine ni jambo la kawada kabisa, wala hakuna mahusiano na uchawi.
Watu wanateseka sana kwa kufiwa na wapendwa kwenye vifo vya kutatanisha,kwa hao wachawi acha tu kamchape wafanye kazi Yao, uzuri ni kazi wanaifanya mchana kweupe mbele ya watu na hakuna Cha Kuficha na mtu kama ni mchawi kweli anasema bila hata kulazimishwa na anatoa mauchawi yake na anataja yeye mwenyewe na thamani ya uchawi huo ,Mimi naunga mkono ndoo maana zaidi ya asilimia kubwa ya wananchi wanaunga mkono isipokuwa wachawi au familia zao .Niko kigoma ambapo zoezi linafanyika watu Wana furahi sana.
 
Narudia tena ni Udhalilishaji, Upuuzi, Ushenzi, Uchonganishi na Utapeli.

Nimefika mkoa wa Kigoma Tokea Majuzi nilicho Kikuta huku Sielewi Huku ninchi Nyingine au ni Tanzania hii hii !

Kuna kitu kinaitwa  KAMCHAPE, hawa wapuuzi nani kawaleta, Hili kweli nani kalipa Baraka kufanyika karibu mkoa mzima wa Kigoma?

Kinachofanyika Ni Udhalilishaji na Uchonganishi kwa jamii.

Kwanza Wanachangisha Tsh 5,000 kila kaya kwa lazima sio ombi.

Kisha Wanapita kila nyumba Eti wanatoa Uchawi na wachawi! Tena utake usitake lazima.

Wakifika kwako wanasema hapa kuna uchawi Lazima uchapwe kisha unanyolewa Nywele Mbele ya umati wa watu kisha kunyweshwa Kile wanachoKiita Dawa hautakuwa mchawi tena!

Nimefuatilia kinachofanyika pale ni Mazinga Ombwe na Kujipatia Pesa kwa Utapeli!

Wakati Yakifanyika hayo Kijiji Jirani, Nyie mnaanza jiandaa na kama mwenyekiti hata Wakaribisha hao watu au kuchangisha hizo pesha kila kaya naye Anajumuishwa kwenye Kundi moja la Wachawi !

Kuna vitu vya Ajabu sana Vinafanyika mpaka nimeshikwa na Butwaa. Nimeuliza nikaambiwa Serikali Ndio Imeruhusu hili Lifanyike Mkoa mzima kweli?

Mbona Sioni Dodoma na Mbeya Kwanini Kigoma?

Kwasasa zoezi limepamba Moto Vijiji vya Nyarubanda, Kalinzi, Mukigo, Muhinda, Nyaruboza, Rukoma, Igalula, Mgambo, Katumbi, Kalya Nk.

Huko kumechafukwa hali ni mbaya na lisipofanyiwa kazi na kuacha litaleta shida kwa watu


Pia soma
- Mfahamu 'Kamchape' mkamata wachawi na shughuli zake kwa ujumla kutokea hapa Mkoani Kigoma
Huo mkoa mm naona ni kama wanaishi maisha ya mwaka 2000 wakati now ni 2023.
Sijui ni ujuaji na ubishi wa kijinga ndio unawaponza sijui hata ni nn?
 
Mbn hujatuwekea picha ya wanaodhalilishwa au hata wewe unaleta uzi uli uzue taharuki ktk jamii?

Hapa niko wilaya moja ya Mkoa wa Kigoma lkn hilo sijaliona kbs
 
We fanya yako mkuu...acha nao wafanye yao..
 
Lengo la hiyo operation ni kuondoa huo uchawi,amini nakwambia uchawi umetajwa hadi kwenye vitabu vitakatifu,kwa hiyo upo.Ambaye familia yake ni wachawi ndoo wanalalamika na hii operation.
Nchi inaongozwa kwa katiba na sheria, sio hivyo vitabu vyenu vitakatifu.
 
Inaonekana unaongea kitu ambacho haujui sisi wenyeji wa hayo maeneo tunajua kiundani zaidi vifo vya kipuuzi sana vinavyotokea huko.
Vifo vya kipuuzi ni kwa sababu ya umaskini uliotopea, jamii zote masikini wastani wa umri mdogo wa kuishi ni jambo la kawaida kabisa.
 
Wako vizuri tu, kuutoa uchawi, make wachawi wanakera sana kwenye jamii, kama wanajitolea kila kaya, 5,000 kwa hiari sawa tu, huwezi kulinganishwa na utapeli unaofanyika makanisani, wachugaji wanawatapeli sana, wananchi maskini, lakini hamsemi, kisa kimeazishwa na wazungu, mchugaji ananunua gari, la milioni 200. kwa sadaka za waumini wake alafu wao wanakosa hela ya chuvi tu hamuoni kama, huo nao ujinga,?
Huyo anayeutoa huo uchawi ni nani ??
Yeye mwenyewe sio mchawi au mshirikina??
 
Nyie mnaopinga hiyo Operation mnajua mateso wanaopitia watu huko inakofanyika hiyo Operation?

AFRIKA HAIENDELEI SABABU MACHAWI YANANENEPEANA TU KILA SIKU CHA KUSHANGAZA KUNA WATU WANAWATETEA HUMU!
Africa ndilo bara linaloongoza kwa raia kuwa na imani za kidini tofauti na China, Japan, Marekani au Ulaya.
 
Nyie mnaopinga hiyo Operation mnajua mateso wanaopitia watu huko inakofanyika hiyo Operation?

AFRIKA HAIENDELEI SABABU MACHAWI YANANENEPEANA TU KILA SIKU CHA KUSHANGAZA KUNA WATU WANAWATETEA HUMU!
Africa haiendelei kwa sababu ya uongozi mbovu, uvivu, elimu duni na mawazo kama ya haya ya zama za giza.
 
Hao viongozi ni sehemu ya raia wa Tanzania, na raia wa Watanzania wengi wetu tulishawahi kusikia neno uchawi, hivyo hao viongozi wanawaunga mkono hao kamchape wakiamini uchawi ni kikwazo cha maendeleo Kigoma.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Wakurugenzi, wakuu wa wilaya na mikoa wa Kigoma wauze mashangingi yao, wachimbe visima vya maji safi, wajenge hospitali karibu na vijiji na waweke barabara za vijijini lami waone kama watu watakufa vifo vya ajabu ajabu tena.
 
Kuna siku mdau mmoja alileta nyuzi hujo Ujerumani ilifanya operesheni ya kuwaua wachawi wote kwa sababu ni kikwazo cha maendeleo.

Sasa wewe unapendekeza njia zipi zitumike kuwamaliza wachawi huko Kigoma?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Wazungu wenyewe wanikiita hiko kipindi ni cha zama za giza/za ujinga na upumbavu, na wanajutia sana mpaka leo walivyokuwa wajinga enzi hizo.
 
Mtoto wa kaka yangu aliponeshwa na hawa watu amini usiamini

Unajua ilikuwaje..........

Mtoto wa bro. alikuwa mwenye afya njema hadi alipotimiza miaka 2 ndipo akaanza kuugua na kukonda huku akijisaidia kinyesi cheusi

Alikonda na kubakia mifupa hospitali alitumia dawa lakini hakupata unafuu,

Siku hao jamaa walivamia kijiji na walipofika kwenye kaya ya bro. alibainika mama mdogo alihusika na kumchezea huyo mtoto....

Uji ukatengwa kwenye jikoni na huyo mama mdogo aliukoroga huo uji kwa mkono wake hadi ulipoiva bila kuungua mikono yake.....

Baadae aliamriwa kumnywesha mtoto ule uji , tokea hapo mtoto alipata unafuu na kupona kabisa hadi leo hii ana familia yake.


Sasa nyie kama mnahisi kwamba serikali yenu hii fisadi itawasaidia kwenye mambo haya ya kiroho......nawashangaaa


Ya kaisari mwachie kaizari
Sasa hapo umethibitisha vipi huyo mama mdogo ndiye aliyemchezea mtoto wa kaka yako??

Mbona watoto wengi tu wanaumwa muda mrefu na kupona bila kupelekwa hospitalini!
 
Nipo zangu masanga garden nakula k vant njoo tule maisha Chief
Dah masanga jamani, Mimi ni product ya huko sema tu hivyo enzi nakuja huko kijiwe ilikuwa just in town ipo njia ya airport sijui Kama bado IPO na kule mlimani mesi kule kilimahewa
 
Back
Top Bottom