Kinachoendelea Tanzania kuhusu mfumuko wa bei ni hatari kwa ustawi wa maendeleo ya wananchi na usalama wa nchi

Hao asilimia 24% ndio pamoja na viwanda vinavyotengeneza bidhaa muhimu za ujenzi ambazo zinalalamikwa kupanda sana bei.
 
Mfumuko wa bei unasababishwa na serikali iliyopo ama kutatuliwa na serikali iliyopo.
Magufuli ,if any , "alisababisha uchumi kusinyaa" nasiyo inflation yani mfumko wa bei.
Mfumuko wa bei unasababishwa hasa na vitu hivi:
1. Serikali kushindwa ku control na ku regulate soko na ndiyo maana serikali ina regulatory authorities kila sehemu.

2. Production cost imeongozeka sana hadi kumfikia mlaji na msababishaji hapa ni serikali pia, mfano wameongeza kodi, wameongeza tozo, umeme unakatokakatika, ulipaji wa wafanyakazi mshahara umeongezeka nk.

3. Demand imekuwa kubwa kuliko production hii ndo huamualiwa na soko huria.

Ila ukiangalia kwa Tanzania inflation ni sababu ya namba moja na mbili. Serikali legelege isiyojali.

Nini serikali inachoweza kufanya na ku control inflation.
1. Serikali ina subsidies ktk imported goods ambazo ni basics kama mbolea na mafuta na gas nk.

2. Serikali inapunguza ama kufuta kabisa kodi na tozo zinazosababisha artificial inflation.

3. Serikali kuhakikisha umeme haukatiki ili kupunguza productions cost.
Zingine utaongezea.
 
Mwaka jana serikali ya Marekani ilikuwa inatoa pesa na chakula kwa wananchi wake ili kuwasaidia katika kipindi cha lockdowm. Sidhani kama taifa letu tutakuja kufika kwenye level hizi. Sometimes najiuliza je ni kwa hatuna wataalamu wazuri wa masuala ya uchumi wakamshauri Rais?
Au urais ndiye amegoma kushauriwa
 
Kwingine kote uko sahihi kasori sababu ya kwanza. Regulatory authorities hasa zinapoingilia bei ndizo zimekuwa chanzo kikubwa cha kuchangia kuharibu uchumi. Kuna madhara nakubwa sana kwa EWURA, TCRA n.k kujiingiza katika upangaji wa bei za bidhaa na huduma.

Regulatory authorities zinatakiwa ziwe kwa ajili ya kuhakikisha ushindani fair wa kibiashara unakuwepo,utunzaji mazingira, afya za walaji zinazingatiwa na mambo mengine ya aina hiyo, sio kupanga bei au kutoa miongozo ya bei, uchumi wa soko huria hauendeshwi hivyo.
 
Mkuu nakubaliana nawewe

Lakini soko huria si kwamba mnaachiwa mjipangie bei tu mnavyotaka. Maana ya regulatory authorities siyo kuhakikisha tu fair competition among the vendors or competitors bali pia service provided is fair game kati ya mlaji na mtoaji huduma yani price offered is reasonable as per price list.
Samahani kwa kuchanganya vilugha ndani.
 
Kwani Chadema ndiyo wameleta mfumko wa bei?
 
Regulatory authorities haziwezi kujua na kuamua bei reasonable kamwe. Bei reasonable ni ile mnunuzi anayoamua kulipa mwenywe akiwa na taarifa sahihi bila kulazimishwa. Serikali ikiweka mazingira mazuri yanayovutia wafanyabiashara kuwa wengi bei zitashuka tu na kuwa reasonable.
 
Ukiacha sababu za kisiasa ,Hali hii inachangiwa na mwenendo wa uchumi wa Dunia kiujumla.

NChi zote kuna mfumuko wa bei ,si Afrika,Ulaya wala Marekani.

Hii inatokana na athari za covid 19 na haielekei kutengamaa kwa miaka ya karibuni.

 
Soma kitu kinaitwa price controls, just for simplicity is that: price controls are government mandated minimum or maximum for goods and services.
 
Unajielewa kweli wewe!
Unamahaba ya kingese kweli..

Jpm anahusika vipi na hii hali.
Huyo bibi ako amekaa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…