Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Mfanyakazi anahusiana nini na kodi ya shule! Yeye analipa kodi ya mshahara wake tu. Vitabu! Jipange uandike
Na huyo mfanyakazi ataendelea kulipa hiyo kodi hata atakapo poteza ajira kwa sababu shule haina pesa za kumlipa?
Na wewe pia ni msomi!

Amandla...
 
Wapumbavu wanasema kuwa eti shule ilikataa kupeleka watoto kujaza uwanja wakati wa kampeni za urais. Watu sijui wakoje!! Mimi nimewaambia watafute sababu nyingine
 
Actually ukisoma na kuelewa andiko la St. Jude utabaini kuwa kinachofanywa na shule ni sawa na kinachofanywa na TASAF ispokuwa St. Jude wanatumia the best strategy and advanced approach for sustainable eradicating of poverty from communities wakati TASAF wanatumia elementary rudimental strategic approach for eradicating poverty from communities. Ila cha kushangaza pesa wanazotumia TASAF hazikatwi kodi wakati St. Jude wanashurutishwa kulipa kodi!
 
Misaada hainaga tozo ya Kodi.
Leo hii sirikali wanaleta hoja za kodi, thus y kuna huo mgogoro.
 
Hifadhi ushoga wako. Nilichokupa ni fact. Na nimeifanyia kazi by 100%. Ndegelec
Matusi ya nini mkuu,

Wewe una research yako na mimi nina yangu kwani ni lazima nikubali mawazo yako
Naamini research yangu
Matusi ni ishara ya malezi mabovu, upungufu wa ufahamu na maadili.
 
Who projects? a fool of ua caliber takes such oaths. Don’t derail the truth abnoxiously . Looks idiotic.
Tf is "Truth" you referring to!?

Get over your struggles with Homosexual-OCD kwanza maana that's the "Fact/Truth" you can take to the Bank!

No Homo! Just a brother looking out for you!
 
Kimsingi kama PAYE haikuwahi kulipwa huko nyuma hapakuwa na haja ya kukwapua mil 500 za uendeshaji wa shule kwa kuwa tu walimu walikuwa hawakatwi PAYE.

Shule kwa kuwa msingi wake ni donations, TRA ingeweka waiver ya kutokuwadai kilichopita na kuanza kudai sasa.

Barrick na ACACI tulijua wanatupiga, yet tulikaa nao mezani.
Bart Airtel hali kadhalika.

Sasa haya mambo ya kubanana namna hii sio sawa.
TRA hawajui how it takes kuandika proposals kupata donor funding.

Unaweza kuandika propose 100 ukapata 1 au ukakosa. Kama kuna watu wamejua kuna uhitaji, forex inakuja Tz na inakuwa spent kwa manunuzi ya chakula, kulipa walimu/wafanyakazi wasio walomu mishahara na kukarabati shule; iwepo busara ya hali ya juu maadam kinachoingia kiko proven sio kwa ajili ya kutengeneza faida but charitable.

Kwenye hilo nalo mpaka JPM atoe maelekezo kweli??

Labda kama kuna mambo hayajakaa sawa kwenye uendeshaji wa taasisi, ni vema yakawa addressed yenyewe bila kuingilia mkondo wa fedha za matumizi ya kawaida.

TRA wawe na weledi wa hali ya juu. Na kama sheria ya waiver haipo itafutwe. Donation zikikata, watoto wetu watakosa kusoma na hiyo amounts inayokuja ikikata, hata zile indirect taxes zinazopatikana via spending nazo zitakata.
 
Nimependa mtazamo wako katika hii kesi. Vipi juu ya hoja ya TRA kuwa hii shule haikuomba/haikuwa na Ruling ya CG ambayo ndio KIBALI haswa cha Taasisi tajwa kuwa Charitable Organisation?

Kwanini uendeshe jambo kwa DHAHANIA? (bila kufanya Compliance na sheria husika)
 
Non profit organization inalipaje kodi.? Kwanza Kodi maana yake nini tuanzie hapo
Ki msingi kuna Kodi ambazo zinapaswa kulipwa Kama PAYE lkn Kama nilivyosema tuosubiri upande wa pili ambao ni serikali watufunulie pazia.lifting the veil.
 
Nitakununulia Kahawa urejee leo... Kuna kitu unatakiwa utupatie hapa!
 
Nadhani shida ni mgonano wa kimaslahi ndo unaotesa taasisi na miradi mingi hapa nchini,kutakuwa na wakubwa wana shule yao huko Arusha na wameona St.Jude ni tishio kwa uhai wa shule yao,hivo wafanye figisu kuifungia lengo shule yao ipate wateja,wanamadai ya kodi,kama ni kodi leo ndo wameiona?.
Kuna shule ilikuwa Kongowe kule chini barabara ya kuelekea Kigamboni pia ilifanyiwa figisu kuwa iligushi usajiri watoto wakaondolewa wote wakati ilikuwa na miaka kibao tangu ilipo jengwa na kupokea watoto.
Wananchi tufikirie kiundani na siyo kushabikia mambo ya kiuonevu
 
Elimu kwa Watanzania ni jukumu na kazi ya Serikali JMTZ na siyo Mzungu wa sijui Australia, kwani huko kwao hana matatizo ? ...
Huku ndo kukosa maarifa.mpaka leo hujui maana ya private sectors na umuhimu wake kea nchi hii?kwamba serikali inaweza fanya kila kitu bila private sectors ku chip in.Hatari Sana kama kuna wtz wenye akili Kama hizi.
 
Watanzania wengi ni aidha ni wavivu wa kusoma au wanapotosha makusudi, utakuta jitu zima limeng'ang'ana kulaumu Serikali ya Awamu ya tano au jingine linasema hawakupeleka watoto uwanjani kwenye kampeni ndio maana TRA wamewafuata!

Pamoja na maelezo mazuri na ushahidi maridhawa wa msingi wa madai yenyewe tangu mwaka 2009 na kesi ya msingi ya mwaka 2012 ambayo imewekwa kwenye uzi huu bado kuna mapopoma yanalaumu Serikali ya awamu ya 5.

Ujinga mwingine ni pale jitu linaingiza chuki za kikanda na kikabila kwenye ishu huu mfano hili jamaa Zanzibar asp na hili Salary Slip
 
Porojo tu za TRA shule from the outset ilisajiliwa as a ‘limited by guaranteed company’ kupitia Brella na vibali vyote vimewekwa kwenye post number 1 ya hii mada na vielelezo vingine vimewekwa kwenye kesi.

Kwa maana hiyo mgogoro wa kuamua shule ni charity or not that is not issue in this matter, kuna ushahidi wa kutosha it’s a charity.

Mzozo ni kodi za 2009 and 2010 kuhusu allowable expenditures claimed during that period (ambazo TRA inapinga in some) and income surpluses which their sources are allowable based on charity organisation operation be it they might be subjected to capital gain tax; rather than cooperate tax.

Just get proper accountants in TRA sio kuweka watu tia maji, tia maji and use qualified judges to decide on tax matters.

Asubuhi njema, I need a rest.

Ila tatizo lilipo based on the evidence there is enough evidence of sharing blame. More on TRA side for their incompetence.

Off to sleep, laters 👋
 
Kazi kwelikweili!
Nadhani pia wazazi ambao watoto wao wanasoma katika shule hizo Wana kitu wanachokijua au kinachoendelea hata hao wanaofadhiliwa ni kweli wanastahili kudhaminiwa?Kitu vitu viko chino ya pazia napenda kusikia kutoka upande wa pili pia watueleze kilichojiri.
 
[emoji122][emoji122]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…