Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Wakati Mwingine tunapenda kulaumu mno bila kujua UNDANI WA MAMBO....

Serikali ipo kwa ajili ya kuwahudumia watanzania...kwani na hao wanaoiendesha ni watanzania hawahawa....

Si kila wakati serikali inafanya mambo KUKIFAIDISHA CHAMA TAWALA......
Ishu ni kwanini wameanza sasa baada ya kukataliwa kupeleka wanafunzi kwenye mkutano wa kampeni wa CCM?

Hilo ndilo swali kuu
 
Wakati Mwingine tunapenda kulaumu mno bila kujua UNDANI WA MAMBO....

Serikali ipo kwa ajili ya kuwahudumia watanzania...kwani na hao wanaoiendesha ni watanzania hawahawa....

Si kila wakati serikali inafanya mambo KUKIFAIDISHA CHAMA TAWALA......
Hili sakata lina siku ngapi mpaka sasa? Serikali iko wapi kutoa ufafanuzi? Ukiona kimya ujue kuna kitu hakipo sawa!

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Hivi umesoma ukaelewa?
Wanafunzi wote wanaosoma hapo 100% hawalipi ada wanalipiwa na wafadhili

Kodi inatoka wapi hapo.
Siamini kama Serikali inaweza tu kufanya uonevu wa kuwalipisha hiyo kodi bila kuchunguza,shule nyingi za private za kidini zipo business oriented Ila hujificha kupitia kivuli cha misaada wanayoitoa kwa baadhi ya wanafunzi
 
Mkuu this happened only because they refused to take their students to Sheikh Amri Abeid stadium. To cheer up Magufuli and also to increase number of people on the ground to ful Meko.
 
Siamini kama Serikali inaweza tu kufanya uonevu wa kuwalipisha hiyo kodi bila kuchunguza,shule nyingi za private za kidini zipo business oriented Ila hujificha kupitia kivuli cha misaada wanayoitoa kwa baadhi ya wanafunzi
Kama msaada unatolewa kwa 100% na hela sio za kwenu. Iyo business inakuadhiri vipi wewe na serikali yako?
 
Hii shule ni ya zamani sana..tangu mwaka 2007 nakumbuka..kwanini iwe leo ndio waangalie suala la kodi mlima hivyo..
Hawakupeleka wanafunzi uwanjani kipindi cha kampeni.
 
Mkuu unanishawishi sana niachane na hii kazi ya ufundi nikasome Sheria.

Pamoja na umri wangu kusogea sana.
 
Elimu kwa Watanzania ni jukumu na kazi ya Serikali JMTZ na siyo Mzungu wa sijui Australia, kwani huko kwao hana matatizo ? ...
Tunajua huu ni mpango wenu wa kuwanyima wa TZ masikini elimu bora,ili muendeleze udharimu wenu
 
Mkuu this happened only because they refused to take their students to Sheikh Amri Abeid stadium. To cheer up Magufuli and also to increase number of people on the ground to ful Meko.
NImeona watu wengi wakizungumzia hii hoja, na timing yake ina-make sense!!

Kama suala ni la tangu 2012, huku shauri la mwisho likiamriwa 2018, WHY NOW?!

Kutokana na hilo, kuna kila dalili kwamba hapa kuna kukomoana bila kujua wanaemkomoa hapa ni mwananchi maskini aliyekuwa ananufaika na huu mpango!!!
 
Halafu we jamaa sijui kwanini tags zako huwa zisionagi... kama hii hapa nimeiona just by chance!! All in all, I missed hizi nondo, sijui ulipotelea wapi though I still remember mara ya mwisho ulivyokuwa umesema unachukua likizo in politics, nami nikakusudia kufanya hivyo though sijawa successful!!

Sema dah, it's good umeingia ndani zaidi kisheria! Halafu unajua niliposoma ile hukumu na kukuta mambo ya Bank Interest nikabaki kucheka mwenyewe, na kujiuliza ina maana mimi ndo sijui, au?!

Anyway, hivi bank interest huwa inakatwa Corporate Tax au ina-attract withholding tax?!

And for what I know, when it comes to Withholding Tax on Bank Interest, ni ngumu kutolipa hii kodi kwa sababu banking system automatically inashikilia (withhold) amount charged na kisha bank husika kuandika cheque to TRA baada ya ku-DR the said withheld amount!!

Halafu hili suala la kupunguziwa kodi miradi mikubwa hivi serikali waneelewa impact yake kweli?! I wish wangefahamu kwa vitendo ni kwanini kwenye Project Management watu huwa wanafanya appraisal ya Cost-BENEFIT-Analysis na sio Cost-PROFIT-Analysis!! Hapa ndo tunarudi kwenye miradi kama Bandari ya Bagamoyo!!!

Benefits za Mradi kama ule ni kubwa maradufu kuliko VAT "Profit" from imported materials ambazo zingetumika kwenye ujenzi wenyewe!!
 
Hii ndio tofauti ya Tz na Nchi za ulimwengu wa kwanza. Kuna kipindi makampuni ya Hispania yalikua na madeni makubwa na kutaka kuporomoka ila serikali hiyo hiyo ikayakopesha na yale malimbikizo ya kodi wakapewa schedule ya kulipa taratibuu kwa miaka zaidi ya 10.

Hapa waliangalia spillover effect..... Yes tunawadai na wakilipa wanafilisika. Je one time payment ya 500M na watu zaidi ya 1000 kupoteza ajira za direct na indirect ipi ni hatari kwa mapato?

Well..... Kuna wanafunzi wanasomeshwa bure je hiyo human capital inayokuja kusaidia taifa linaenda wapi kma shule ikifungwa? Je hamuoni thamani ya wanafunzi ni zaidi ya 500m in the long run?

Sio spain tu hata marekani huwa wanafanya hivi mara kibao tu linapokuja suala lenye maslahi mapana ya uchumi au jamii yao. Sisi hku tumekalia kuangalia sheria tu inasemaje bila kujali context.
 
Uko sahihi,ndio maana ni lazima sana kupata madai ya upande wa TRA ili Kuweza kusema ni uonevu ama la
Kiutaratibu walitakiwa wapate kibali toka kwa kamishina wa TRA wa kodi.
Swali je walipata kama walipata ni sababu zipi TRA wamefungia akaunti zao.
Kuna uwezekano sio wote waliosomeshwa ni watoto wasio na uwezo tumeshuhudia mikopo ya elimu ya juu ililenga watoto wasio na uwezo lakini wanufaika wakubwa ni wale wenye uwezo inabidi tupate taarifa ya. Upande wa pili kabla ya kukimbilia kuhukumu
 
Kwanza kuweka pesa mifukoni mwa private entities zenye kuhudumia umma ni swala debatable..inafanyika yes.. is it fair and okay "No".

Taasisi zinazaliwa zinakuwa na hatimaye zinakufa..kuinject mafedha hakuifanyi iendelee ni kuweka kwenye life support tu.. once you plug out its dead.. wanafanya sikatai ila siiungi mkono.. maana ikifa it will open a door for new ventures that are more resilient to form.

Tuachane na hilo.. swala la taasisi hii jaribu kuliangalia kwa upana wake.. akina nani wamesoma ST Jude!? Ni kweli wanatoka kwenye Familia Duni!?

Au ndio ile mnaokotwa 100 kwenye 2000 halafu taasisi inaqualify Kuwa inasomesha watanzania 2000 bure!? Kuna sehemu mbili nimekaa wanataja kwenye tovuti yao huwa wanaenda kufanya "rigorous process" ya kuwapata hao watoto.. I can guarantee you sijui kama TASAF wanajua ambao wangewapoint kwenye uhitaji..

Isije Kuwa (my opinion) ni kagroup la wajanja wachache wanachukua vijana wao wanawapeleka for a fee (substantial) wasome bure..

Wewe ungeambiwa this school inatoa elimu bure kwa budget za Bablo na Haichukui faida that means inawekeza milioni 6 zote kwa mtoto kwa mwaka.. ukiombwa mil 10 one time payment hulipi!? 🙂

Lakini wenzetu huko kwao wanapata tax relief kwa fedha wanazospend kwenye charity work. Sasa inaweza kuwa wanaandika gharama kuuubwa za uendeshaji wa hizi charity huku.. ili kule kwao wapate tax deductions kubwa pia..

Au inawezekana wanapokea na fedha za ndani pia.. zinazoendesha shule hata kama sio ada(basi michango) ila unakuta kwa ishu ya mapato wanakwepa na all the money inakuwa regarded as foreign funds. Hapo sio fair..

Najaribu kujihoji kama layman kwenye haya maswala maana haina mashiko kusema TRA na serikali hawajui cost benefit analysis.. yaani ni wajinga wa kiwango cha mwisho kabisa..

Bado nasisitiza, waliosoma ST Jude na wote walioko Vyuoni wanaolipiwa na ST Jude kwanini hawajafika uzi huu!? Kwanini wamekaa kimya!? Kuna kitu hakiko sawa
 
Mkuu hizi allegations ndio zimeletwa na TRA? Issue hapa ni kodi hayo ya wanafunzi kuwa sio wahitaji halisi ni kwenda out of context. Wao wamedai kodi kutoka kwa taxable income fulani walioiona na sio udanganyifu wa wanafunzi otherwise ingekuwa na kesi tofauti.... So tusihame kutoka kwenye mada.

2. Wanafunzi kutokujibu hakumaanishi ndio allegations zako zinakuwa kweli. Otherwise wangejitokeza ww ungedai kwamba ni PR stunt ama damage control strategy na ungeshauri "waache kiherehere, wawe wapole wasubiri due process''. So mie nadhani tusitengeneze zero sum game hapa bali compromise ndio ingefaa wakati huu. Hatumkomoi mtu hapa otherwise watakaoumia sio management ya shule bali wafanyakazi (Familia zao) na Watoto yatima, pamoja na Taifa ambalo litakosa wataalamu maelfu kwenye sekta mbalimbali in the long run.
 
Sijui hata nicomment nini
Kimsingi shule zote ambazo hazipo kibiashara, hazitakiwi kulipa kodi yoyote zaidi ya PAYE. Ndivyo ilivyokuwa awamu zote za Serikali zilizopita. Lakini awamu hii, imekuwa tofauti. Na hilo halijatokea kwa shule hiyo tu bali ni kwa zote za namna hiyo.

Wengine hawajajitokeza humu. Wanapoamua kufunga, TRA ndiyo huja na kuwaambia wasifunge, na kuwataka walipe kodi japo kidogo.

Tupo kwenye laana. Badala ya Serikali kuwa msaada inakuwa mkomoaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani wewe mkuu! Huu ukimya haukufanyi ujihoji!? Honestly!

Mie tangu Jana nimetoa angalizo waliosoma Jude waje Watueleze what's what!

Kwa ajili ya uzi huu nimejua zaidi ya Kodi.. na diagnosis inabidi iendelee.. kupata fursa ya kujua zaidi sio kitu kibaya.. mie si mtaalam wa Kodi na katu siwezi kuingilia ninachopinga ni kuaminishwa kamba hawa wataalamu wetu (TRA) ni mambumbumbu kiasi kwamba haya yanayojadiliwa hapa na wataalamu wa JF wao hawayajui kabisa.. hilo tuu
 
Kuna Hali Halisi na What's on paper. Mfano Ukienda Sinza kila kiwanja kina maduka.. na maeneo mengi watu wanatoka nje wanajenga frame ...bila vibali wala nn..

Siku vikivunjwa au wakiletewa mafaini makubwa watalalamika hivi hivi. Nachosema ni yawezekana kile walichosema wao watakuwa sio kile walichokuwa muda huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…