Kinachomsumbua Dkt. Slaa ni udini na chuki binafsi kwa Rais Samia

Kinachomsumbua Dkt. Slaa ni udini na chuki binafsi kwa Rais Samia

Mjinga wewe tuambie kwanini aliteuliwa marehemu wewe ukaachwa?
Maswali ya kitoto haya. Unafahamu alifariki tarehe ngapi na saa ngapi? Unafahamu kuwa uteuzi hufanyika kabla ya siku ya kutangazwa? Hujawahi kuona barua ikisema uteuzi huu ulianza siku fulani ambapo unakuta ni karibu Wiki moja kabla ya siku ya kutangazwa rasmi kwa uteuzi?
 
Sasa ulitaka Dk.Slaa awe chawa wa Mama?
Kama wakati wa JK (ambaye ni Muislam) Dk.Slaa hakuwa na chuki naye za Udini,inakuwaje awe na Chuki za Udini kwa Mama?
Basi wewe ni msahaulifu sana au ulikuwa haujaanza kufuatilia siasa za nchi hii. Hivi mara hii umesahau vurugu za dkt Slaa wakati wa Mheshimiwa Kikwete?
 
Acha uchawa wa kijinga wewe wenzako wanateuliwa hata wakiwa wameshakua marehemu wewe unaandika maandishi yasiyo na mshiko ndio maana uteuzi utaendelea kukupita
Kwani wapi nimesema kuwa natafuta uteuzi hapa .au wewe upo hapa kutafuta uteuzi.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kama ni Wafuatiliaji wazuri wa siasa za nchi hii mtakubaliani nami na ukweli kuwa Dkt. Slaa amekuwa na Udini mkubwa sana ndani ya kifua chake. Amekuwa na chuki binafsi sana kila inapotokea utawala uliopo madarakani ni wa upande wa pili yaani Uislamu. Amekuwa ni mtu mwenye chuki, vurugu na mzushi wa masuala mbalimbali ili kuwachafua viongozi wetu hasa Rais pamoja na kumchonganisha na Wananchi.

Unaweza muangalia Dkt Slaa wa wakati wa Mheshimiwa Kikwete, wakati wa Hayati Dkt Magufuli na wakati huu wa Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan. Utagundua ya kuwa anaongozwa zaidi na Udini pamoja na chuki binafsi kwa Mheshimiwa Rais.

Hali hiyo imempa upofu wa akili na macho katika kujadili hoja. Ndio sababu unaona anakuwa akizusha mambo mbalimbali ya uongo na uchonganisha kwa lengo la kutaka kuifanya serikali ichukiwe na wananchi. Jiulize kama umewahi kumuona au kumsikia Dkt Slaa akikosoa kitu chochote kile katika utawala uliopita. Unafikiri ni kwanini? Jibu ni Udini tuu ndio muongozo wake. Ndio maana kwa Udini wake yupo tayari kuzusha lolote na kusema uongo wowote ule ili serikali ichukiwe na kuleta taharuki pale inapokuwa ikiongozwa na muislamu.

Lakini ni huo huo Udini wa Dkt Slaa anaweza kufumbia macho kitu chochote kile na kutetea kila jambo ikiwa tu ni wa upande wa Dini yake. Ndio maana katika uzushi anaoongea huwezi ukaona akiweka ushahidi wa aina yoyote ile mezani kuthibitisha madai yake ya uzushi na uongo. Hawezi akaweka nyaraka yoyote ile kuthibitisha maneno yake.

Watanzania tunapaswa kumpuuza na kukataa kabisa kuingia katika mtego wa Dkt Slaa wenye lengo na ajenda ya chuki binafsi na Udini kwa kutunga vitu vya kizushi na uongo. Tumkatalie zidi ya ajenda zake chafu za kumchafua Mheshimiwa Rais na tumkemee kwa nguvu zote. Tumwambie kama ana ushahidi wa lolote lile anapokuwa akizungumza hadharani basi atuwekee kwanza ushahidi.

Napenda kumalizia kwa kusema kuwa dkt Slaa hata fanikisha ajenda zake za Udini na chuki binafsi kwa Mheshimiwa Rais, na wala hatafanikiwa kumchafua kwa namna yoyote ile kama ambavyo amekuwa akifanya jitihada za kutaka kumchafua Rais wetu na kumjengea taswira mbaya kwa wananchi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wala si kweli,ni sawa kabisa Samia kusemwa,anafanya mambo ya ajabu sana,infact analidhalilisha Taifa,kama huoni hivyo,basi wewe ni kilaza.Watu wanaiba tu hakuna hatua zinazochukuliwa,wananchi wamekuwa wageni katika nchi yao,dhuluma imetamalaki kwenye taifa,wananchi hawapati haki zao za msingi,uovu umetawala nk.nk.watu wamsifie,na si tutakuwa vilaza basi.

Halafu of late kafanya jambo la ajabu sana, Rais unakuwa summoned kama mtoto na Rais mwingine!Hata Traore Rais mdogo kabisa wa Burkina Faso aliona ni upuuzi, wa kwetu kaona ni fursa,shameful indeed. Rais unatembelea nchi nyingine unakaa for seven days!Disgusting and despeacable.
 
Maswali ya kitoto haya. Unafahamu alifariki tarehe ngapi na saa ngapi? Unafahamu kuwa uteuzi hufanyika kabla ya siku ya kutangazwa? Hujawahi kuona barua ikisema uteuzi huu ulianza siku fulani ambapo unakuta ni karibu Wiki moja kabla ya siku ya kutangazwa rasmi kwa uteuzi?
Kwahiyo mpk mnatangaza mlikuwa hamjui kama ni marehemu? kama mnashindwa kujua vitu vidogo hivi mtaweza kujua mambo makubwa kama mikataba ya nchi na nchi ndiyo maana maza alimteua DG wa bandari Mwenyekiti wa UVCCM, usivyo na akili japo upo UWT hujui mtu yoyote anayeteuliwa na Rais kabla ya kutangazwa anakuwa kwenye uangalizi wa DSO lakini huna akili wala hujui maana ya vetting, mshamba mkubwa wewe.
 
Wala si kweli,ni sawa kabisa Samia kusemwa,anafanya mambo ya ajabu sana,infact analidhalilisha Taifa.Watu wanaiba tu hakuna hatua zinazochukuliwa,wananchi wamekuwa wageni katika nchi yao,dhuluma imetamalaki kwenye taifa,wananchi hawapati haki zao za msingi,uovu umetawala nk.nk.Halafu of late kakanya jambo la ajabu sana, Rais unakuwa summoned kama mtoto na Rais mwingine!Hata Traore Rais mdogo kabisa wa Burkina Faso aliona ni upuuzi, wa kwetu kaona ni nafasi. Yaani Raisi wa natembelea nchi na kukaa for seven days! Dispeakable.
Ni mambo ya hovyo kabisa hata hii aibu ya kwenda kukaa siku 10 kwenye nchi ya watu serious na kuanza kuteua utadhani uteuzi ni jambo la dharura kama vile hatorudi tena nchini.
 
Nani ampe uteuzi mtu asiejua kujibu facts.Nilimtafuta kwa thread flan hivi kama anaweza aweke facts niweke.
Akakimbiza mkia wake.

Dr.Slaa ameshavuka level za udini huyu mtu.
Alikua tested akapata ubarozi akasaliti mapambano ila kwa udini namtetea kabisaa.
Unaweza niwekee video hata ya Dakika moja ikimuonuesha dkt Slaa akikosoa jambo lolote lile katika awamu iliyopita?
 
Kwahiyo mpk mnatangaza mlikuwa hamjui kama ni marehemu? kama mnashindwa kujua vitu vidogo hivi mtaweza kujua mambo makubwa kama mikataba ya nchi na nchi ndiyo maana maza alimteua DG wa bandari Mwenyekiti wa UVCCM, usivyo na akili japo upo UWT hujui mtu yoyote anayeteuliwa na Rais kabla ya kutangazwa anakuwa kwenye uangalizi wa DSO lakini huna akili wala hujui maana ya vetting, mshamba mkubwa wewe.
Kweli wewe akili yako imepofuka kabisa eti uangalizi wa DSO.
 
Back
Top Bottom