Mshaurini dkt Slaa aache Udini na chuki binafsi kwa Mheshimiwa Rais. Embu nikuulize swali hilo. Je umewahi kumsikia Dkt Slaa akikosoa chochote kile katika utawala uliopita?
Broo huijui hii nchi wala Siasa za ndani na za kimataifa kama Dr. Slaa.
Hujui falsafa ya ukristo wala uislam kama Dr. Slaa.
Huijui CCM wala upinzani kama Dr. Slaa. Hujui Diplomasia wala Demokrasia kama Dr. Slaa .
Humjui Dr. Samia na Serikali yake kama Dr Slaa
Mwisho kabisa Dr Samia hakujui kama anavyomjua Dr. Slaa.
Iko hivi:-
Nchi za magharibi wakishirikiana na nchi Tajiri za Kiarabu zenye ushirika wa karibu na nchi za kimagharibi hasa Marekani wakishirikiana na Wafanyabiashara wakubwa wa silaha duniani , waporaji wa rasilimali za Afrika na kwingineko, wauza madawa ya kulevya na wawekezaji wahuni na walaghai wote wanatengeneza ugaidi kupitia Dini na Kabila. Kongo kwenye wakristo wengi na wapagani wengi hawa Wahuni wa kishetani na mashoga na adui wa Kizazi cha Mwanadamu waefanikiwa kuwaangamiza mamilioni ya Waafrika kupitia Ukabila.
Iko wazi kuwa Kwa sasa Wahuni hao na mawakala wa setani duniani wanatumia uislam maeneo yenye waislam wengi kutengeneza ugaidi kwa baadhi ya nchi za Afrika na Asia . Kwa nchi za Afrika zaidi wanatumia Ukabilla.
Kwa nini Marekani na maswahiba zake wanatumia Uislam kwenye nchi zenye waislam wengi, ? Jibu ni kwa sababu wanajua kuwa uislam ni dini iliyojengwa kiitikadi tangu utotoni. Yaani uislam unajengwa kama mfumo wa maisha kisiasa ,kijamii na kiuchumi.
Ni rahisi kumrubuni mtu aliyejengika kiitikadi tangu utotoni katika misingi ya kuona kuwa hakuna zaidi ya kila anachokiamini.Ndio maana sehemu kama Tanzibar hakuna Lugha za makabila zaidi ya kiswahia hawaamini katika ukabila zaidi ya uislam.
Karne zilizopita Ugaidi ulifanywa zaidi na Wakristo hasa Wakatoliki huko Ulaya na Amerika ya kusini kutokana na jinsi dini iilivyokuwa imejengwa kiitikadi. Kwa sasa hali imebadilika wala Mabepari wanaona ukristo umegawanyika na hauna tena wafia dini.
Ni wazi kuwa kwa sasa CCM haikubaliki bila kutumia dini. Kuna magroup mengi ya whasap watu wanatumia siasa za hovyo za kusema kuwa Eti Dr. Samia anapingwa kwa sababu ni muislam.
Na kwa sababu wale Wahuni na wezi wa kimataifa wamefanikiwa kutudanganya kwa kutumia fedha na misaada kwenye taasisi na NGOs wanaaminika kwa haraka mana wale wasubiri misaada wanaona kazi ni nzuri mana pesa za bure zinapatikana sasa bila kujua kuwa uhalifu wa kimataifa hupitia fedha za misaada.
Watu wamempinga Magufuli Mpaka wakapigwa Risasi na bado wanaendelea kumpinga Mama Samia bila kujali ni Dini gani. Watu wanapigania Rasilimali za Taifa hili alizoziumba Mungu na sio Mama Samia.
Sasa hivi ameaminisha watu kuwa yeye ndiye ameiumba ardhi na utajiri wa Tanganyika na watu wanampigia magoti. Mungu hakuwa mjinga kuwaweka kila watu kwenye eneo lao na rasilimali za kutosha . Ukiwa Rais ni lazima ukubali kukosolewa na hata kutukanwa.
Kinacholeta uchawa huu ni Katiba mbovu . Watu wanajipendekeza kwa sababu katiba inamfanya Rais kuwa zaidi ya Mungu. Anaweza akaamka asubuhi akamtajirisha mtu na kumpa cheo kikubwa na kumvurugia mwingine maisha kama anavyoona yeye bila kuulizwa.
Lakini pakiwa na katiba bora mambo ya udini,ukabila ,uchawa na uchama yatapungua sana.
Hawa wanaoeneza hisia za udini wanatafuta uteuzi tu. Kenya palikua na ukabila sana lakini umeanza kufutika baada ya katiba mpya. Siasa zinajijenga kwa misingi ya hoja sio dini na ukabila.
Dr. Slaa amefanya kazi na Serikali ya CCM Dr.Samia akiwa Makamu wa Rais. Serikali sio Samia yeye ni kiongozi na mtawala . Akikosea atasemwa na serikali yake.
Dr Slaa ni mwanasiasa na mwanaharakati sijawahi kumsikia akizungumzia mambo yanaayohusiana na itikadi za kidini. ?
Wakristo tangu Mwalimu Nyerere walimpinga sana mpaka wengine wakahama nchi . Mwinyi hivyohivyo ,mkapa hivyohivyo aliambiwa na Mrema kuwa ameuza Migodi na wenyeji wakafukiwa kwenye mashimo wakiwa hai. Akaja Kikwete hivyo hivyo akapingwa alipouza Gesi na kuwapiga kwa mabomu Watu wa kuisini kisha gesi kupewa wageni na mpaka leo nchi ni maskini na tozo ndizo zinajenga mashule na barabara badala ya gawio la gesi kama tulivyoambiwa na tukawalaumuwamakonde na kufurahia walipokua wanavunjwa miguu.
Ugaidi ukaanza kutengenezwa. Magufuli akakuta hali ya ugaidi iko juu karibu na kuvuruga nchi. Yote chanzo ni mikataba ya hovyo na misaada saada.
Dr. Slaa ana haki ya kuhoji masuala yanayohusu Tanganyika mana ndiyo nchi yake pekee. Mama Samia ana nchi mbili Zanzibar na Tanganyika na ni Rais wa Tanganyika kwenye koti la Muungano au Tanzania .
Ni wazi kuwa Mleta Mada unachochea Chuki za kidini lakini mwisho wake utashindwa kwa sababu kizazi hiki hata huko Uarabuni hawapiganii maslahi ya mtu mmoja wala dini yake bali uhuru wao na maslahi ya Taifa kwa manufaa ya wengi.
Wawekezaji waje wajenge viwanda ,sio malori ya kubeba mizigo na mabasi na Bandari ,wanyama ambao wapo bure porini hawana hata kazi kubwa ya kuwatunza kama ngombe au kuku. Tunawapa misitu ili wafanyeje? Tunawapa ardhi kubwa ambayo ndio urithi wa maskini kwenye nchi waliyoumbiwa na Mungu. Halafu watu wakae kimya.
Yaani umffukuze mmasai mwenye nyumba ya matope na Ngombe halafu umlete Mwarabu mwenye Magari ,Mandege ,mabunduki, Mahoteli n.k eti ndiye anayetunza mazingira . ?
Inakuja kweli kwenye akili ya dini ya mtu au ni janga la kitaifa kwa miaka ijayo.
Mikataba yote mibovu imeleta madhara makubwa kwa watu maskini na wazawa. Kuanzia kwenye migodi mpaka kwenye hifadhi.
Wewe Mleta mada hebu Jiulize Kama JPM alipingwa na kwa kiwango kikubwa alilinda sana Rasilimali za nchi na kupinga sana ufisadi maisha yake yote tangu akiwa waziri wa ujenzi kwa watawala waliokuwa wamejimilikisha magari ya umma na kuweka namba za kiraia huku wakiwa wanatumia madereva wa serikali na kafuta ya serikali kwa shughuli binafsi JPM angesafiri na kuuza rasilimali za nchi kama ilivyo leo kelele zake zingekuaje ukiunganisha na Kelele za kipindi cha Kikwete?
Huoni kuwa JPM ameiokoa sana CCM mpaka leo ina watu kama Majaliwa , Makonda,Polepole,Ndugai,Mpina,Chalamila, na hata wabunge kama Mdee aambao wanaweza kutoa hoja zenye kufikirisha ?
Yaani JPM angeendeleza mbinu zile zile za kupiga bakuli na kugawa rasilimali za umma kwa mawakala wa mashoga duniani ! Hali ya CCM ingekuwa mbaya sana na uchumi ungeporomoka sana kipindi cha Korona .
Tusisingizie udini kwenye maslahi ya nchi. Lisemwalo lipo na Dr. Slaa hajawahi kukosea katika kutoa hoja zake juu ya ufisadi .