Kinachomsumbua Dkt. Slaa ni udini na chuki binafsi kwa Rais Samia

Kinachomsumbua Dkt. Slaa ni udini na chuki binafsi kwa Rais Samia

Ni mzushi tu. Kwanini hakutafuta ushahidi ili aje aweke? Naomba uniwekee video hata ya Dakika moja tu ya dkt Slaa akikosoa jambo lolote lile katika utawala uliopita.
Mpaka uwekewe ina maana wewe huna kumbukumbu? Yaani unataka mtu awe ametunza video clips za zaidi ya miaka 10 iliyopita kwa matarajio kuwa kuna wakati watakuwepo watu ambao hupoteza kumbukumbu vichwani mwao kila wakati.

Wenye akili timamu, ma wenye kumbukumbu wote wanafahamu namna Dr. Slaa alivyokosoa utawala wa Mkapa kwenye masuala ya madini. Mwalimu Nyerere naye pia alikosoa utawala wa Mkapa kwenye ubinafsishaji. Alimkosoa pia Mwinyi kwa kutozingatia katiba.

Pia wenye kumbukumbu nzuri wanafahamu namna TEC ilivyoukosoa vikali utawala wa Magufuli kwenye masuala ya haki za watu. Lakini pia TEC wamekosoa vikali jinsi utawala wa Samia kwa kuwapa wageni bandari kupitoa IGA ya hovyo kabisa, kuliko yoypte ile katika Ulimwengu huu. Sambamba na ukosoaji wa chama cha wanasheria nchin, chamba ambacho kina wanachama wa imani zote
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kama ni Wafuatiliaji wazuri wa siasa za nchi hii mtakubaliani nami na ukweli kuwa Dkt. Slaa amekuwa na Udini mkubwa sana ndani ya kifua chake. Amekuwa na chuki binafsi sana kila inapotokea utawala uliopo madarakani ni wa upande wa pili yaani Uislamu. Amekuwa ni mtu mwenye chuki, vurugu na mzushi wa masuala mbalimbali ili kuwachafua viongozi wetu hasa Rais pamoja na kumchonganisha na Wananchi.

Unaweza muangalia Dkt Slaa wa wakati wa Mheshimiwa Kikwete, wakati wa Hayati Dkt Magufuli na wakati huu wa Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan. Utagundua ya kuwa anaongozwa zaidi na Udini pamoja na chuki binafsi kwa Mheshimiwa Rais.

Hali hiyo imempa upofu wa akili na macho katika kujadili hoja. Ndio sababu unaona anakuwa akizusha mambo mbalimbali ya uongo na uchonganisha kwa lengo la kutaka kuifanya serikali ichukiwe na wananchi. Jiulize kama umewahi kumuona au kumsikia Dkt Slaa akikosoa kitu chochote kile katika utawala uliopita. Unafikiri ni kwanini? Jibu ni Udini tuu ndio muongozo wake. Ndio maana kwa Udini wake yupo tayari kuzusha lolote na kusema uongo wowote ule ili serikali ichukiwe na kuleta taharuki pale inapokuwa ikiongozwa na muislamu.

Lakini ni huo huo Udini wa Dkt Slaa anaweza kufumbia macho kitu chochote kile na kutetea kila jambo ikiwa tu ni wa upande wa Dini yake. Ndio maana katika uzushi anaoongea huwezi ukaona akiweka ushahidi wa aina yoyote ile mezani kuthibitisha madai yake ya uzushi na uongo. Hawezi akaweka nyaraka yoyote ile kuthibitisha maneno yake.

Watanzania tunapaswa kumpuuza na kukataa kabisa kuingia katika mtego wa Dkt Slaa wenye lengo na ajenda ya chuki binafsi na Udini kwa kutunga vitu vya kizushi na uongo. Tumkatalie zidi ya ajenda zake chafu za kumchafua Mheshimiwa Rais na tumkemee kwa nguvu zote. Tumwambie kama ana ushahidi wa lolote lile anapokuwa akizungumza hadharani basi atuwekee kwanza ushahidi.

Napenda kumalizia kwa kusema kuwa dkt Slaa hata fanikisha ajenda zake za Udini na chuki binafsi kwa Mheshimiwa Rais, na wala hatafanikiwa kumchafua kwa namna yoyote ile kama ambavyo amekuwa akifanya jitihada za kutaka kumchafua Rais wetu na kumjengea taswira mbaya kwa wananchi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Hizi taka taka sijui kwanini wanapewa simu.
 
Habari wakuu Mimi Nina certificate ya laboratory technician pia Nina experience ya miaka 3 kuhusu laboratory technician, laboratory analysis, QC,QA pia blending oparetor au syrup oparetor pia naweza kufanya kazi popote pale penye maabara au panapozalishwa bidhaa .yeyote atakaye nisaidia kupata connection ya job nipo tayri kuingia naye mkataba awe anakata 10% ya mshahala wangu ndani ya miezi 12.asanteni
Unamaanisha mineral laboratory technician?
 
Mpaka uwekewe ina maana wewe huna kumbukumbu? Yaani unataka mtu awe ametunza video clips za zaidi ya miaka 10 iliyopita kwa matarajio kuwa kuna wakati watakuwepo watu ambao hupoteza kumbukumbu vichwani mwao kila wakati.

Wenye akili timamu, ma wenye kumbukumbu wote wanafahamu namna Dr. Slaa alivyokosoa utawala wa Mkapa kwenye masuala ya madini. Mwalimu Nyerere naye pia alikosoa utawala wa Mkapa kwenye ubinafsishaji. Alimkosoa pia Mwinyi kwa kutozingatia katiba.

Pia wenye kumbukumbu nzuri wanafahamu namna TEC ilivyoukosoa vikali utawala wa Magufuli kwenye masuala ya haki za watu. Lakini pia TEC wamekosoa vikali jinsi utawala wa Samia kwa kuwapa wageni bandari kupitoa IGA ya hovyo kabisa, kuliko yoypte ile katika Ulimwengu huu. Sambamba na ukosoaji wa chama cha wanasheria nchin, chamba ambacho kina wanachama wa imani zote
Swali fupi na dogo lakini wewe unajaza pumba tupu. Nimesema niambie Dkt Slaa alikosoa kitu gani na jambo gani katika utawala wa awamu ya Tano? Uzi na andiko langu yalihusiani na habari za TEC. Au unataka kuniambia kuwa mawazo ya Dkt Slaa huwakilisha kanisa la katoliki ambalo yeye binafsi alishakiuka viapo vyake vya upadri?
 
Tunahitaji mtu wa kukosoa mambo kwa hoja na ushahidi na siyo mtu anayeonekana kuongozwa na Udini pamoja na chuki binafsi. Dkt Slaa amekuwa mtu wa kusukumwa chuki binafsi na Udini.ndio maana hajawahi kuonekana akikosoa chochote kile katika utawala uliopita.
Poa. Mange yeye alimkosoa na Magu.
Tumsikilize yupo part 6 sasa hivi
 
Umehamia kwenye udini kama ndugu yako Ally Hapi baada ya jitihada nyingine kushindikana? Udini unakata kotekote, hauna manufaa...
Ndio maana nawapinga sana watu naowaona wakitaka kuleta Udini na chuki binafsi zinazochochewa na ubaguzi.
 
Ndio maana nawapinga sana watu naowaona wakitaka kuleta Udini na chuki binafsi zinazochochewa na ubaguzi.
Wakemee basi na hao akina Ally Hapi na Mashehe wote waliosema waislam waichague CCM kwa sababu ya Uislam wa Samia. Au tukuletee ushahidi hapa?
 
Mheshimiwa Rais hajawahi kuwa mdini wala kumbagua mtu kwa misingi ya aina yoyote ile. Lakini dkt Slaa amekuwa na chuki kubwa sana na utawala huu tangia uingie madarakani. Kinachomsumbua ni Udini na chuki binafsi tu ndio maana amekuwa akizusha vitu vya uongo na uchonganisha kwa lengo la kumchafua Mheshimiwa Rais
Unaweza ukathibitisha kwa ushahidi ili na sisi wengine tufaidike ambao hatujawahi kumsikia Dr. SLAA akizusha uongo juu ya Raisi?!
 
Lakini ni huo huo Udini wa Dkt Slaa anaweza kufumbia macho kitu chochote kile na kutetea kila jambo ikiwa tu ni wa upande wa Dini yake. Ndio maana katika uzushi anaoongea huwezi ukaona akiweka ushahidi wa aina yoyote ile mezani kuthibitisha madai yake ya uzushi na uongo. Hawezi akaweka nyaraka yoyote ile kuthibitisha maneno yake.
Mbona na wewe unatembea kwenye nyayo hizo hizo unazosema Slaa anazo?
Unashindwa hata kuweka mifano tu ya tuhuma anazozusha?

Umekuwa ukitapatapa sana; lakini sasa naona huku kutapatapa kwenu kunaanza kuwa ni kurusha mateke, na hatimae mtakata roho tu, hakuna namna nyingine.
Umekuwa mashuhuri wa "kububjikwa machozi"; lakini sasa machozi yanageuka kuwa damu. Hamponi ng'o safari hii.
 
Napenda kumalizia kwa kusema kuwa dkt Slaa hata fanikisha ajenda zake za Udini na chuki binafsi kwa Mheshimiwa Rais, na wala hatafanikiwa kumchafua kwa namna yoyote ile kama ambavyo amekuwa akifanya jitihada za kutaka kumchafua Rais wetu na kumjengea taswira mbaya kwa wananchi
Kwa hiyo kama hali ni hii, kinachokuhangaisha humu ni kitu gani?
Ninapomwona chizi, na kumbatiza kwa jina hilo, huwa sikosei hata mara moja.
 
Umenena vema kuwa siyo muislam. Na inawezekana pia siyo mkristo, bali una jina la Kikristo.
Wanajulikana vizuri humu JF waliojipachika majina kwa lengo maalum. Huyu ni mmoja; akina Steve Ntamusana nao wamo.
 
Back
Top Bottom