Kinachosikitisha wa Tanzania waliozamia SA wemerudi na umaskini

Kinachosikitisha wa Tanzania waliozamia SA wemerudi na umaskini

Mwaka 2010 niliwahi ishi Greece kwa miezi 6..
Kipindi hicho nipo under 30 ..
Athens nilikuta watanzania wengi sn,,wenye maisha mazuri na maisha ya kutubu.
Mimi nilikuwa miongoni mwa vijana ambao walikuwa na maisha magumu sn pale Athens.
Ndipo mzee wng mmoja mtanzania akaniweka chini akanishauri.
Mwandende"wewe bado mdogo sn,,
hapa Greece hapakufai,,utapoteza muda wako bure..
Mimi nina umri wa miaka 50 now,nipo hapa tangu 1998 , najuta kuwa hapa hadi sasa,,
Sina pesa na pia sina family zaidi ya ile niliyoacha Tanzania.
Tanzania nimeacha mke na mtoto mmoja tu,,,
sipendi na wewe yakukute.. natamani kurudi nyumbani Nashindwa.

Nakushauri tafuta maisha pia tafuta na family .
watu wengi wanaoishi ulaya hawana family .
Rudi nyumbani kajipange upya,
Tafuta maisha na tafuta family pia,
Ukikosa maisha unaweza ukapata maisha mazuri kupitia watoto wako hapo baadae...ukiwa hapa hutotengeneza family,.watu wengi hapa wanaishi kisela tu.

Nilimsikiliza yule mzee na kuamua kurudi Tanzania..

Nilichojifunza kwa watanzania wengi wanaoishi Africa kusini,na baadhi ya inchi za ulaya na America kusini zenye maisha magumu.
Wengi hawana maisha na family pia hawana..
Wamekosa vyote...
Mtu yupo south miaka 30 hana mke wala mtoto na ameshakuwa mtu mzima...
Mtu una over 55 umeishi nje zaidi ya miaka 30 hata ukirudshwa Tanzania now utafanya nn?...
Huna maisha na family pia huna.
Kweli mkuu kuanzisha familia nje ya Tanzania ni ngumu kwasababu Tamaduni ni tofauti na Marengo ni tofauti kati ya Watanzania na Raia wa nchi hizi ambazo siyo za Kijamaa, hapa Tanzania kuanzusha familia ni rahisi kuliko Ulaya. Hapa nchi unaweza ukawa unaingiza kipato cha laki tatu na Ukapata Mke mkaanzisha maisha pamoja, Sasa uende Ulaya na Africa kusini utampata Mwanamke gani wa kuanzisha nae Maisha wakati huo bado unajitafuta
 
acha uongo wewe
wewe unaishi ulaya ?
Mkuu watu wanasema Ulaya ni Ulaya tu hata kama anaishi Slovenia, Sisi Watanzania tunajua Ulaya ni Germani. Marekani, France, Belgium, Italy, Denmark, Norway, Canada, Sweden, Switzerland, hizi nchi ndiyo Watanzania tinazipenda na tumezoeshwa na Viongozi wetu.
 
Wazazi wa nani mkuu Elon au maana kama Elon walitengana aliamua kuishi kwa baba yake kisa alikua na Computer na yeye alikua anapenda hizo mambo akiwa bado mtoto..
Basi haujui kitu, mzee wake alikuwa na mawe kishenzi.
Baba yake, Errol Musk, alikuwa mhandisi wa umeme na mitambo (electromechanical engineer), rubani, na baharia. Pia alifanya biashara ya mali isiyohamishika (property developer) na alikuwa mmiliki mwenza wa mgodi wa zumaridi (emerald) nchini Zambia, ambao ulileta utajiri mkubwa katika familia wakati wa utoto wa Elon.
 
Mimi kweli sijui kitu ila mimi naishi na kaburu huku kazi ulizozema sio za mawe kishenzi Mkuu..
Elon kasoma hapo Pretoria boys kwa kaburu kuwa na miradi ni kawaida ila sio ya kusema hiyo ndio imemfanya awe tajiri utajiri wa Elon ni akili yake ndio kafika pale SA ina matajiri wangapi na hakuna mtoto kawa tajiri mazee yule ni talented..
 
Nimekwambia angalia background! Hiyo nayo imempush kwa kiwango kikubwa angwlikuwa na wazazi wasio na elimu kubwa na mawe asingetoboa.
 
Nimekwambia angalia background! Hiyo nayo imempush kwa kiwango kikubwa angwlikuwa na wazazi wasio na elimu kubwa na mawe asingetoboa.
Sio kweli mpe credit jamaa kwa kuwa na akili hapa mzungu Elimu bure mpaka anamaliza anakota wangapi wamefika huko hapa mzungu maisha unayoyawaza wao walishapita kitambo mpaka kesho.
 
Sio kweli mpe credit jamaa kwa kuwa na akili hapa mzungu Elimu bure mpaka anamaliza anakota wangapi wamefika huko hapa mzungu maisha unayoyawaza wao walishapita kitambo mpaka kesho.
Kwa hiyo hata hujui kuwa jamaa alitema masomo? Na yeye mwenyewe anakwambia hakuna haja ya kwenda chuo ili ufanikiwe?

Jamaa kapewa shingapi kwenye kuinvest kwenye issue zake binafsi? Mkuu fstilia vizuri
 
Mkuu nipo busy nafatilia mambo ya Logistics kuleta bidhaa Nchi za East Afrika huko ukipata kichaka tusambaze bidhaa za kutoka hapa itakua muhimu hayo mambo ya watu tuwaachie wasizwa..
 
Kweli mkuu kuanzisha familia nje ya Tanzania ni ngumu kwasababu Tamaduni ni tofauti na Marengo ni tofauti kati ya Watanzania na Raia wa nchi hizi ambazo siyo za Kijamaa, hapa Tanzania kuanzusha familia ni rahisi kuliko Ulaya. Hapa nchi unaweza ukawa unaingiza kipato cha laki tatu na Ukapata Mke mkaanzisha maisha pamoja, Sasa uende Ulaya na Africa kusini utampata Mwanamke gani wa kuanzisha nae Maisha wakati huo bado unajitafuta
Hilo ndy jambo la msingi sn mkuu,
Wengi walio nje ya inchi hawana family Zaid ya watoto waliowaacha Tanzania kabla hajasafiri.
 
Kuuguzwa sio tatizo. Wanaweza wasiumwe. Ila tatizo ni kuishi maisha ya upweke ambayo ni magumu sana

Mkuu ukishazeeka kuugua ni must kwa sababu kinga ya mwili inapungua magonjwa yanakuwa mengi hata kama sio kuugua kwa muda mrefu lakini itahitaji upate mtu wa kukupeleka hospital na kufuatilia maendeleo yako kwa hizo siku kadhaa sasa pata picha una miaka 75 umechoka unafanyaje..? Na nchi zetu hazina vituo vya kulele wazee vilivyo serious kama Ulaya na Marekani.
 
Back
Top Bottom