- Thread starter
- #201
Acha hizo,mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Mzee Kinana ni msema kweli na anajua maisha. achilia mbali tuhuma za wildlife, ukiweka pembeni, huyu ni mtu mwenye akili na diplomasia ya hali ya juu. na wengi huwa wanamtukana kwasababu tu ana asili ya somalia, bila kujua kuwa ametumikia taifa hili kwa ubora kuliko wao. hapa Tanzania ukizaliwa hapa kabla ya 1961 katiba inasema wewe ni Mtanzania mzawa hata kama ungekuwa mzungu au mhindi. yeye ni Mtanzania Mzawa, ameshashika vyeo jeshini hadi kuwa kanali kama sikosei. na hata kipindi cha magufuli, jamaa alikuwa anasema vitu vya maana kama hivi akikemea vijana kuwa na kiburi, ila hawakumsikia. hao kina sabaya na makonda walishaonywa ila hawakusikia zaidi sana walimshughulikia. makonda ni chukizo la uharibifu kabisa hapa Tanzania na uwepo wake kwenye uongozi wowote ni dhihaka kwa watanzania.
Angekuwa na HEKIMA, Msemakweli, angekishauri chama chake kuhakikisha tunapata Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya kuingia uchaguzi 2025!!