Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Duniani Mbali Kenya Tu haimilikiwi na Rais..
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Kenya Ni Vigumu Rais Kuimilikk kwa sababh upatikanaji wake Unafanya Iwe vigumu kwa Rais kuwa na maamuzi nayo...

Kingine Tlaatlaah mkumbushe Mwenyekiti wetu kuwa..

Rais Gorge Bush (Bush Jr ) hakugombea na Hillary Clinton uchaguzi wa 2004 na wakapelekana hadi Supreme court kama alivyosema....

George Bush Jr aligombea Mara ya Kwanza Urais wa Marekani mwaka 2000 na Albert Anorld Gore Jr ( Al gore ) na uchaguzi wa 2004 aligombea na John Kerry.


Nimeweka Record sawa
 
Rubbish
 
Ina maana wabunge wa Zbr wamefilisika hoja ndiyo maana wakaletwa wengi na hata kuingia kujadili mambo ya wizara zisizowahusu?
 
1. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe watano wa Tume wanateuliwa na Rais. Katika mfumo uliopo Rais ni Mwenyekiti wa Chama Tawala.
2. Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watatokana na mapendekezo ya Kamati ya Usaili.
3. Wajumbe wa kamati ya Usaili ni:
a. Mwenyekiti wake ni Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huyu ni mteule wa Rais.
b. Jaji Mkuu wa Zanzibar. Huyu ni mteule wa Rais wa Zanzibar.
c. Mwenyekiti na makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hawa ni wateule wa Rais
d. Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Rais kwa kuzingatia jinsia.
4. Metendaji Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambae ni mteule wa Rais.

Wajumbe watano wa Tume ya Uchaguzi South Africa wanateuliwa na Rais kutokana na majina yaliyopendekezwa na Bunge. Majina yanayopendekezwa na Bunge yanatokana na Kamati Huru nje ya Bunge. Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ndio wana appoint Mtendaji Mkuu wa Tume.

Wajumbe saba wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya wanateuliwa na Rais na wanathibitishwa na Bunge.

Wajumbe watatu wa Tume ya Uchaguzi India wanateuliwa na Rais kutoka majina yaliyopendekezwa na Kamati inayoundwa na Waziri Mkuu, Mkuu wa Chama Kikuu cha Wapinzani Bungeni na mmoja kutoka kwenye Union Council of Ministers. Tume ndio inayo appoint Mtendaji Mkuu.

Ukiangalia kwa wenzetu, ingawa Mkuu wa Serikali anahusika lakini hana absolute power ya kuthibitisha wajumbe wa Tume na watendaji wake. Hii ni tofauti na hapa kwetu.

Amandla...
 
wenzenu wap ndugu,

asie na absolute power?

ni katika serikali ya kidini au kisiasa ndio hana absolute power 🙄
 
Yaani ni aibu kabisa kuona watu wanakusanywa halafu mtu anajibu hoja kirahisi rahisi namna hii
 
Bure kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…