Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Duniani Mbali Kenya Tu haimilikiwi na Rais..
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Kenya Ni Vigumu Rais Kuimilikk kwa sababh upatikanaji wake Unafanya Iwe vigumu kwa Rais kuwa na maamuzi nayo...

Kingine Tlaatlaah mkumbushe Mwenyekiti wetu kuwa..

Rais Gorge Bush (Bush Jr ) hakugombea na Hillary Clinton uchaguzi wa 2004 na wakapelekana hadi Supreme court kama alivyosema....

George Bush Jr aligombea Mara ya Kwanza Urais wa Marekani mwaka 2000 na Albert Anorld Gore Jr ( Al gore ) na uchaguzi wa 2004 aligombea na John Kerry.

Nimeweka Record sawa
 
sawa kamanda,
ila kinana ni balaa sana :pedroP:
Sheria za Uchaguzi anazozitetea Kinana hizi hapa, hivi huyu Mzee anadhani sisi ni wajinga kiasi gani?

Screenshot_2024-05-05-14-01-34-1.png
 
Wanasahau muungao huu ni wa nchi huru, tumeunganisha nchi mbili, na huu Tunakubali na kukiri hizi ni nchi mbili tofauti zilizoamua kuungana kwa hiyari, zikiwa na ukubwa ardhi tofauti, ukubwa wa uchumi tofauti na ukubwa wa watu tofauti, tukiungana lazima tukubali kuwe na uwakilishi wa kutoka pande zote mbili. Usipime watu kwa udogo wao na ukubwa wao, wapime kwa walivyo, walikuwa huru tukaungana nao. Nchi ya Seychelles wako 100,007 wana wabunge 35, Lesotho ina watu 2,300,000 wana wabunge 130, lakini ndivyo walivyojipanga, Switzerland ina watu 1,700,000 wabunge wa 246 sawa na Tanzania ambapo sisi ni milini 60 na wabunge 300, ndivyo walivyokubaliana uwakilishi wao, Sweden 10,500,000 wana wabunge 349 kwanini hatuwaulizi? Kwahiyo hoja hii ya CHADEMA haina maana, ni hoja ya kuzua, kukotroga vichwa vya watu, kuchanganya watu, kuleta, uhasama, uchochezi. Haya yote wanayoongea hayaondoi umasikini wala kuleta maendeleo, basi tu tuvurugane, mimi naamini muungano huu utadumu.
Rubbish
 
Ubunge hauwakilishi idadi ya watu, ubunge unawakilisha hoja, matakwa ya watu, maoni, na mahitaji ya wnanchi. Wabunge hawaendi bungeni sababu ya idadi ya watu, wanaenda kwa uzito wa hoja, kuzungumza matatizo ya wananchi, kuzungumza juu ya shida za nchi yetu sio idadi, idadi sawa itafikiriwa lakini sio msingi pekee.
Ina maana wabunge wa Zbr wamefilisika hoja ndiyo maana wakaletwa wengi na hata kuingia kujadili mambo ya wizara zisizowahusu?
 
1. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe watano wa Tume wanateuliwa na Rais. Katika mfumo uliopo Rais ni Mwenyekiti wa Chama Tawala.
2. Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watatokana na mapendekezo ya Kamati ya Usaili.
3. Wajumbe wa kamati ya Usaili ni:
a. Mwenyekiti wake ni Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huyu ni mteule wa Rais.
b. Jaji Mkuu wa Zanzibar. Huyu ni mteule wa Rais wa Zanzibar.
c. Mwenyekiti na makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hawa ni wateule wa Rais
d. Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Rais kwa kuzingatia jinsia.
4. Metendaji Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambae ni mteule wa Rais.

Wajumbe watano wa Tume ya Uchaguzi South Africa wanateuliwa na Rais kutokana na majina yaliyopendekezwa na Bunge. Majina yanayopendekezwa na Bunge yanatokana na Kamati Huru nje ya Bunge. Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ndio wana appoint Mtendaji Mkuu wa Tume.

Wajumbe saba wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya wanateuliwa na Rais na wanathibitishwa na Bunge.

Wajumbe watatu wa Tume ya Uchaguzi India wanateuliwa na Rais kutoka majina yaliyopendekezwa na Kamati inayoundwa na Waziri Mkuu, Mkuu wa Chama Kikuu cha Wapinzani Bungeni na mmoja kutoka kwenye Union Council of Ministers. Tume ndio inayo appoint Mtendaji Mkuu.

Ukiangalia kwa wenzetu, ingawa Mkuu wa Serikali anahusika lakini hana absolute power ya kuthibitisha wajumbe wa Tume na watendaji wake. Hii ni tofauti na hapa kwetu.

Amandla...
 
wenzenu wap ndugu,

asie na absolute power?

ni katika serikali ya kidini au kisiasa ndio hana absolute power 🙄
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM anazungumza na waandishi wa habari na wanaCCM katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma. Kikwete anategemewa kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kujibu shutuma mbalimbali zilizoibuliwa na upinzania ambazo CCM wameziita ni za kibaguzi dhidi ya Muungano.

Abdulrahman Kinana

CHADEMA wametutuhumu CCM, Serikari na Rais kwa mambo ya uongo. Hatukatai kukosolewa na kusahihishwa, lakini hatukubali kuzuliwa wala kushtumiwa kwa mambo ambayo hayapo au ni ya kutunga. Kubwa walilofanya kwenye mizunguko yao ni kujenga chuki na mfarakano miongoni mwa Watanzania.

Hoja zao na ufafanuzi wa Chama cha Mapinduzi
1. Katiba
Wanasema wanataka Katiba Mpya na kutushawishi katiba mpya ni muhimu - Mwaka jana 2023 tumekubali hoja ya katiba mpya, na wanatanzania wanaitaka katiba mpya, tunachobishania ni lini, wao wanataka ipatikane leo. Rais Samia wakati anandoa zuio la mikutano ya hadhara alikubali pia kuhusu suala la katiba. Haya mambo yanahitaji muda na tafakuri, lakini wenzetu wanasema hapana, katiba inahitajika sana.

Katiba yetu imepokea mabadiliko mara 14, na ukitazama madailiko hayo mara nyingi yalilenga siasa, madaraka na uchaguzi, hata msukumo wa sasa wa CHADEMA lengo lake ni uchaguzi. Serikali imetunga sheria tatu za uchaguzi ambazo zimepita bungeni na Rais kutia saini, sheria ambazo zilitolewa maoni na wadau mbalimbali ikiwemo mpaka bungeni kwa siku nne, ambapo hoja za msingi zilikubaliwa lakini CHADEMA hawakuridhika, bado wasema Rais asihusishwe kwenye uchaguzi wa viongozi wa Tume, sijaona nchi ambayo Rais hahusishwi kwenye maamuzi mfano China, India, Kenya, Afrika Kusini kote Rais anakuwa na mamlaka fulani juu ya Tume. Hakuna Tume ya Uchaguzi Duniani ambayo Rais hana Mamlaka.

CHADEMA walitaka suala la Katiba liwe la CHADEMA na CCM kama chama kikuu cha upinzani na chama tawala, hili haliwezi kufanyika, sababu katiba sio suala la vyama hivi viwili pekee.

Kwa sheria hii nawahakikishia Tume hii itakuwa Huru na kufanya kazi kwa uadilifu, Mweyekiti, Makamu na watendaji watakula kiapo kufanya hiyo kazi, labda kama tunataka malaika kufanya hizo kazi, lakini kazi hizi lazima zifanywe na binadamu.

Katiba na Sheria ya Uchaguzi siyo njia pekee ya kushinda uchaguzi, Sera nzuri, Kukubalika kwa chama chako, Kukubalika wagombea wako na kujipanga ipasavyo kwenye uchaguzi kuna mchango mkubwa sana kwenye ushindi.

2. Muungano
CHADEMA wamekuja na hoja hizi;
  • Zanzibar ni ndogo wakati ina wabunge wengi
  • Rasi samia ni Mzanzibari hana nia njema na sisi - uongo ukirudiwa rudiwa usiposahihishwa unageuka kuwa ukweli, ndicho wanachotaka kuaminisha Watanzania, Watanznia kataeni sumu hiyo inayojaribu kujengwa miongoni mwenu. Kama zanzibar ingekuwa na wnanchi milioni 40 au 60 sawa na sisi je, swali hilo lingekuja? Jibu ni hapana, swali linakuja sababu wako 1,400,000!
Wanasahau muungao huu ni wa nchi huru, tumeunganisha nchi mbili, na huu Tunakubali na kukiri hizi ni nchi mbili tofauti zilizoamua kuungana kwa hiyari, zikiwa na ukubwa ardhi tofauti, ukubwa wa uchumi tofauti na ukubwa wa watu tofauti, tukiungana lazima tukubali kuwe na uwakilishi wa kutoka pande zote mbili. Usipime watu kwa udogo wao na ukubwa wao, wapime kwa walivyo, walikuwa huru tukaungana nao. Nchi ya Seychelles wako 100,007 wana wabunge 35, Lesotho ina watu 2,300,000 wana wabunge 130, lakini ndivyo walivyojipanga, Switzerland ina watu 1,700,000 wabunge wa 246 sawa na Tanzania ambapo sisi ni milini 60 na wabunge 300, ndivyo walivyokubaliana uwakilishi wao, Sweden 10,500,000 wana wabunge 349 kwanini hatuwaulizi? Kwahiyo hoja hii ya CHADEMA haina maana, ni hoja ya kuzua, kukotroga vichwa vya watu, kuchanganya watu, kuleta, uhasama, uchochezi. Haya yote wanayoongea hayaondoi umasikini wala kuleta maendeleo, basi tu tuvurugane, mimi naamini muungano huu utadumu.

Ubunge hauwakilishi idadi ya watu, ubunge unawakilisha hoja, matakwa ya watu, maoni, na mahitaji ya wnanchi. Wabunge hawaendi bungeni sababu ya idadi ya watu, wanaenda kwa uzito wa hoja, kuzungumza matatizo ya wananchi, kuzungumza juu ya shida za nchi yetu sio idadi, idadi sawa itafikiriwa lakini sio msingi pekee.

Sheria ya Uchaguzi
Kuligawa taifa katika majimbo

Yaani ni aibu kabisa kuona watu wanakusanywa halafu mtu anajibu hoja kirahisi rahisi namna hii
 
Bure kabisa!
 
Back
Top Bottom