Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Maandamano ni Haki ya Kikatiba eti yakipigwa Marufuku

Naona impact ya Maandamano ya Chadema imeanza kuwaingia mliita Jogging sasa imekuwaje
 
1.Kwanini Wabunge wa Zanzibar huwa wanajadili bajeti za Wizara zisizo za Muungano, Kama Wizara ya Kilimo?

2. Kwanini kwenye Baraza la Wawakilishi hakuna Wabunge toka Tanganyika kulinda Maslahi ya Tanganyika?

3.Kwanini Wazanzibar wanakuwa Wakuu wa Wilaya Tanganyika ilihali Watanganyika hawawezi kuwa Znz,assumption kwamba TAMISeMI ipo nchi ya Rais?

4.Kwanini Rais wa Jamhuri akitaka kugawa eneo labda Mkoa au Wilaya,Tanganyika anagawa tu,ila Kwa Zanzaibar ni lazima ashauriane na rais wa Zanzibar?
5.Idadi kamili ya wapiga kura ilikupata Jimbo la Mbunge wa bunge la JMT ni ngapi?

6.Kwanini Sukari bei chini Znz?

7.Kwanini Leseni ya udereva ya Tanzania haikubaliki Znz?

8.Kwanini Mh Rais hakubinafsisha bandari za Znz?..Znz hawataki Ufanisi?

9.Kwanini Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hatambuliki Znz ilihali ni wa Tanzania nzima?

10.Kwanini Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halijawahi kuwa na Spika wala Naibu Spika toka Zanzibar?
 
Ameongea pumba. Eti Samiah ndio kaleta uhuru. Very stupid old man.
 
Kinana amepatwa na nini? Ama uzee? Huyu si kinana niliyemfahamu katika kujenga na kuchambua hoja!!

Ameongea vitu ki jumla jumla sana na amepigwa KO na Lissu vibaya mno...
Kupangua hoja za Lissu ambazo nyingi ni za kisheria na kikatiba si kazi ndogo kaka. Mhe. Kikwete alinukuliwa miaka ya nyuma akisema kwamba ni bora akose uraisi kuliko Lissu kuwa mbunge. Akawa mbunge, nadhani ukifuatilia session zake bungeni utaona madini aliyokuwa anatema mle. Kinana ni mfaidika wa mfumo huu, hwezi kupangua hoja hizi kirahisi
 
Bora wangekuwa wanamsema,Sasa wanamtukana.Hata Sasa akiamua kupiga marufuku maandamano hakuna wa kunyanyua mdomo.
Apige marufuku hata muda huu kwani nani anamuda naye?. Shida mnafanya Rais kama mungu. Acheni hizo
 
Tanganyika tutaendelea kuonekana wajinga tu siku zote, eeh ndo tunavyoonekana.
 
Rais huyu wanayemsema, Rais Samia na mtakubaliana na mimi ndiye aliyeleta uhuru ulioko sasa hivi nchini, uhuru wa kusema, kushutumu, kuandamana, uhuru wa mikutano ya hadhara, nina hakika watajibu watasema lakini ipo kwenye katiba, kwani huko nyuma waliponyimwa katiba haikuwepo? Walikwenda barabarani?
Akumbuke uhuru walio nao ni wa kikatiba siyo hisani
 

"KATAENI JUHUDI ZINAZOFANYWA ZA KUJENGA CHUKI DHIDI YA RAIS"*

""Wanasema (CHADEMA) Rais Samia ni mzanzibar na hana nia njema na sisi (Tanzania Bara); hayo maneno hayana ukweli hata kidogo. Watanzania kataeni sumu hiyo (sumu ya utengano) inayotaka kujengwa miongoni mwetu."

Komredi Abdulrahman Kinana, Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC) - Dodoma.

Mkutano wa Wananchi wa Mkoa wa Dodoma, 05 Mei 2024
 
Ni za Bara kwa kuwa kodi wanatoa watu wa Bara. Yeye alitaka hospitals, shule na miundo mbinu ikajengwe Zenji kwa pesa ya Bara tu? Atulie ajibu maswali ya Lissu
 
kwanza SGR alianzisha MAGUFULI na angekuwa hai leo ingekuwa imeisha hadi mwanza. sa100 hawezi kuchukua credit kwenye mradi wowote manake hakuna mradi aliuanzisha. kama upo tajeni.
 
Back
Top Bottom