Rogojin The Idiot
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 2,969
- 3,392
Baada ya Uvumi mkubwa wa kumhusisha Kinana na Kupinga uwekezaji wa Bandari Kwa DP World, hatimaye afunguka.
Akihutubia mkutano wa hadhara Mkoani Mara Kinana amesema Watanzania wasiwe na Wasiwasi Kwa sababu Rais Samia ameapa kulinda na kuhifadhi Katiba ya Nchi hivyo hawezi kuwauza Kwa kufanya jambo ambalo Halima maslahi Kwa Nchi.
My Take
Hakuna wa kurudisha Wala kukwamisha uwekezaji bandarini
=======
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara, Abdulrahman Kinana amewataka Watanzania kutokuwa na wasiwasi juu ya mkataba wa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai kwani Rais Samia Suluhu Hassan, ameapa kuilinda na kuitetea Katiba kwa maslahi yao.
Kinana amesema hayo leo Jumatano, Julai 26, 2023 wakati akihutibia mkutano wa hadhara, Musoma Mjini, Mkoa wa Mara akiwa kwenye mwendelezo wa ziara zake katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Mara, Simiyu na Tabora.
“Kuna mjadala mkuuuuubwa na mpana wa bandari, mjadala huu umefika wakati unawachanganya Watanzania. Wamuamini nani. Nataka niwahakikishie, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyekula kiapo hawezi kufanya jambo ambalo halina maslahi na nchi yake.
“Kama Rais tangu achukue nchi (Machi 19, 2021), amefanya yote haya, kwa nini auze nchi, ili iweje? lakini mkisikiliza mjadala, wote wanaotetea, wanaoupinga, wanaoukosoa hakuna anayesema tusifanye uwekezaji, hata mmoja, wote wanakubali kuna haja ya kuwekeza ili kuongeza ufanisi na kuongeza mapato,” amesema Kinana
Kinana amesema, Serikali imesema ipatokea kila ushauri na CCM imeitaka Serikali isikilize ushauri, maoni na hoja zinazotolewa. Haya yote yatafanyiwa kazi. Haiwezekani rais akapuuza yote haya na mmemuona Rais tangu mjadala umeanza, amekaa kimya, anapigwa vita.
“Kamanda mzuri wa vita si yule vita inapokuwa hivi anabadili mbinu na mikakati, kamanda mzuri ni yule anayetulia. Nahodha mzuri wa chambo si yule anayeyumbishwa bali anatulia na kuona anakabiliana nayo viti,” amesema Kinana.
Kwa maana hiyo kashfa zilizowahi kutokea zilifanywa na watu wasiokula viapo?